TANZIA Jenerali Tumainiel Kiwelu afariki Dunia, kuzikwa Mbezi Loius Dar

Kwanini anazikwa Dar na wakati kwao ni Moshi?
Huyu mzee kwanini wanamzika Dar? kwa nini asipelekwe kwao Moshi? Maana serikali inaweza kugharimia.
Anyway, maybe ni wish yake azikwe Dar. But I find it strange.
Nafsi yake ipumzike alipoandaliwa na mola wake.
Kijijini kwake Mamba Kokirie ni eneo dogo sana naona aliamua azikwe karibu na Miradi na mashamba yake kwani alishika maeneo makubwa na kuwekeza eneo kubwa kuliko hicho kijiji alichozaliwa, nasikia huko Bukoba na Morogoro ni maeneo makubwa, sasa akilinganisha na kupelekwa huko Kijijini mazishi hapangetosha
naona jibu zuri analo YEHODAYA
 
Uko sahihi Lupogo alikuwa namba mbaya kwenye MK yaani Medani ya kivita ni anzijua hadi basi Ukianzisha vita Mzee enzi hizo kijana alikuwa akiangua kicheko!! Sijawahi ona mtanzania asiyeogopa Vita kama Lupogo Anapenda vita hadi basi kustaafu tu jeshini ilikuwa shida alikuwa hataki hata bila kulipwa chochote alitaka abaki tu jeshini akisema yeye anachotaka kukitokea vita aatumiwe bure hahitaji hela hata mia .Ndio serikali wakampa Kazi ya mkurugenzi Wa TACADS kupaki kuwa asubiri vita ikitokea watamtumia !!! Akakubali kwa shingo upande .Loo Mzee anapenda vita huyo sihapata kuona
 
ubarikiwe kwa historia nzuri uliyoitoa
 
Ni kipi kutoka kwa marehemu kilikua kinafanya mpaka mwinyi asipumue
 

Katika list hiyo umemsahau retired General Mwakalindile!!
 

JF imejaa kina sisi wala isikusumbue...ni General Kiwelu ndio aliyopanga na kuendesha yale mapigano ya kumtoa Idd Amin ndani ya Tanzania. Chini ya usimamizi wake, makomandoo wa Tanzania walivuka mto, wakaweka ulinzi ili daraja la muda lijengwe na vifaa kuweza kupita. Kuna General Mmoja anaitwa Kabunda, pengine sasa amestaafu, ndio aliongoza makomandoo hao katika kuwezesha daraja kujengwa.
Hili Jeshi la Wananchi ni jeshi kweli kweli. Toka waasi mwaka 1964 wale waliokuwa KAR, limejengwa kama moja ya majeshi madhubutu, yenye nidhamu na uthubutu mkubwa.
Inapendeza kuona mpaka leo JWTZ bado ni jeshi lililo vile vile
 
RIP Kamanda.
Kwa MKurugenzi wa Habari an Mahusiano wa JWTZ asante sana kwa taarifa na uandishi uliosimama:
Sahihisho: Ukiamua kutujulisha familia ya marehemu huwezi kuandika nusu kuwa ameacha Mke na Watoto. Utaulizwa Watoto wangapi; Majina ya Mke na hao Watoto n.k
 
Marehemu Lupogo is not in good books of the then good Generals.
Ukifuatilia historia ya vita vya Kagera Lupogo alishindwa kuongoza vikosi kukabiri adui maeneo ya Sembabule na kupoteza wapiganaji wengi kwenye uwanja wa mapambano.
Aliondolewa kwenye uwanja wa mapambano na nafasi yake akapewa Brigadier Muhidin Kimario akiwa mkuu wa mkoa Mwanza wakati huo.
Brigadier aliwapanga wapiganaji wake na kuwajegea morali wakasonga mbele na kuwasambaratisha majeshi ya adui.

Someni kinaitwa ;War in Uganda and legacy of IDD Amin msitake kupotosha ukweli.
 
..unadhani tatizo lilikuwa kamanda wa vita, au askari aliokuwa nao hawakuwa tayari kwa mashambulizi waliyokutana nayo uwanja wa vita? huoni kwamba ana mchango wa kuleta ushindi toka Kagera mpaka Sembabule?
 
Siyo kweli mkuu napafahamu vizuri sn na siyo kwamba eti kumejaa makaburi hizo ni hear say
 
..Kuna jambo wengi tumelisahau kuhusu Gen.Tumainieli Kiwelu.

..alipotoka jeshini aliteuliwa kuwa Balozi wetu Ufaransa.

..baadae uteuzi huo ukabadilishwa na akateuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga.
Inawezekana host country ili mkata au yeye mwenyewe aliona hivyo.
Enzi zile wakati mwingine wakita kukutenganisha na strong area zako wanakupeleka Ubalozini ili uwe mpweke na mnywaji pombe tu au wanawake
 
Naona kuna jadi ya kusifia marehemu inaendelezwa kupita kiasi.

Ninakubali ndiyo kuwa huyu Marehemu Kiwelu(Gen rtd) alikuwa ndiyo kamanda muasisi wa vita vya Kagera (ops chakaza).

Lakini je nisababu gani iliyomfanya mwalimu Nyerere kumuondoa haraka sana chini ya moto wa adui mwanzo wa vita mwaka 78?

Yeye pamoja na marehemu Yusufu Himid (brig gen rtd) waliondolewa mwanzo kabisa wa vita, tena kwa sababu maalumu zinazofahamika na kila askari aliyekuwepo vitani wakati ule.

Embu uliza afisa ama askari yeyote aliyeshiriki dhahiri mwanzo wa vita hiyo pia askari waliokuwepo jeshini miaka ya 70-90 wanaomfahamu vizuri marehemu, ukipata wasifu wake wa kweli hautakuja kurudia kumpamba na kumpa sifa za kisiasa.
 
Siyo kweli mkuu napafahamu vizuri sn na siyo kwamba eti kumejaa makaburi hizo ni hear say
Siajasema Mamba Kokirie pamejaa makaburi, ila nimesema eneo la Kiwelu hapo Mamba Kokirie hapatoshi kuubeba mzigo huo, na nilisema toka awali atazikwa shambani kwake Mbezi Luis kwani hilp eneo ni lake kanunua kwa wazaramo na ni kubwa kuliko huko Kokirie km angeenda
Generali Kiwelu amemzika mke wake mkubwa, hapo na upande mwingine alimzika Mkwe (mke wa mtoto wake huyu binti alikuwa Mwanajeshi kabila mmasai hapohapo Mbezi Luis) Kwa hiyo ni mahali patakapodumu kwa familia na ukoo wake
 
Sawa mkuu nimekuelewa
 
Yusuph Himid si ndio alikuwepo wakati Kagera inatwaliwa? Siwezi kumuongelea sana huyu bwana. General Kiwelu alikuwa mkorofi sana. Inasemekana aligoma kabisa kuelezea mipango ya kivita kwa Marehemu Sokoine. Alikuwa na communication problem ambayo sio kitu kizuri kwa operations kubwa kama zile. It could insurbodination of some kind in other places.
Pamoja na hayo, yeye ndio alianza kazi ya kumtoa nduli. Hilo hata kama watu hawakumpenda, lilikuwa la kwake. Yeye ndio alisimamia ujenzi wa daraja la muda baada ya kuvuka mto. Ingawa alirudi makao makuu ya jeshi baada tu ya zoezi lile
 
Inawezekana host country ili mkata au yeye mwenyewe aliona hivyo.
Enzi zile wakati mwingine wakita kukutenganisha na strong area zako wanakupeleka Ubalozini ili uwe mpweke na mnywaji pombe tu au wanawake

Huyu mtu alikuwa na mahusiano mazuri na watu wengine?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…