TANZIA Jenerali Tumainiel Kiwelu afariki Dunia, kuzikwa Mbezi Loius Dar

Thanks.

Hata Mimi sikujua
 
..angekuwa hana nidhani asingerudishwa makao makuu ya jeshi wakati wa vita na kuendelea kuwa CoS nafasi ambayo ni kubwa kuliko aliyokuwa nayo akiwa uwanja wa mapambano. vilevile mwaka 1988 asingeteuliwa kuwa CoS kwa mara ya pili wakati faili na rekodi zake zilichafuka mwaka 1978/79 wakati wa vita.

NB:

..siamini kama Brig.Yussuf Himid anastahili lawama kwa kilichotokea mpaka ardhi ya Tanzania ikachukuliwa na majeshi ya Uganda. taarifa mbalimbali zinaeleza kwamba majeshi yetu yalizidiwa kiidadi, na vilevile yalizidiwa kwa silaha walizokuwa wakitumia majeshi ya Uganda.
 
Kwa maana ipi
Ili uwe balozi lazima level ya communication skills iwe juu sana. Watu hawaendi kwa amri kama jeshini. Wengine ni maaskari wazuri ila diplomasia ni sifuri. Wanafaa zaidi jeshini. Yeye alikuwa mtu wa aina gani?
 
Makamanda wa vita ya Kagera wanaisha mmoja mmoja nafikiri kabakia Jenerali Mwita Marwa

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
Hivi kumbe? yaani wengine tupo mbali sikusikia taarifa za David Musuguri ambaye naye kama tumainiel Kiwelu ameshika eneo kubwa sana maeneo ya Kimara tena pana kituo kabla ya Kibanda cha mkaa.
Pia Mayunga alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro sikumsikia muda mwingi. Ila Gen Sarakikya ingawa vita hakupigana ila naona bado tupo naye Mungu awalinde
 
Ili uwe balozi lazima level ya communication skills iwe juu sana. Watu hawaendi kwa amri kama jeshini. Wengine ni maaskari wazuri ila diplomasia ni sifuri. Wanafaa zaidi jeshini. Yeye alikuwa mtu wa aina gani?
..sina uhakika kama ni kweli au la.

..lakini kuna jamaa mmoja alisema hapa JF kuwa kiwelu hakukubaliwa na Wafaransa kwasababu ya cheo chake cha kijeshi-- Jenerali.

..baada ya hapo ndio akapelekwa kuwa rc shinyanga.

cc BAK
 
Makamanda wa vita ya Kagera wanaisha mmoja mmoja nafikiri kabakia Jenerali Mwita Marwa

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app

..mbona mwita marwa alifariki miaka mingi iliyopita?

..nadhani aliyebaki ni Gen.Musuguri, wengine wameshatangulia mbele ya haki.


cc Ukwaju
 
Nilikusoma juzi kwenye uzi wa teuzi za balozi watu mbali mbali kutaka kujua kwanini hawakupangiwa vituo vya kazi. Nadhani nilikuuliza kama imeshawahi kutoka balozi mteule kutoka Tanzania kukataliwa na nchi nyingine. Ulijibu iliwahi kutokea lakini hukumtaja mhusika. Nakushukuru sana kwa kuweka jina lake hadharani. Nadhani hiyo ya yeye kuwa mjeshi ni sababu tosha kabisa ya kumuwekea kauzibe.
..sina uhakika kama ni kweli au la.

..lakini kuna jamaa mmoja alisema hapa JF kuwa kiwelu hakukubaliwa na Wafaransa kwasababu ya cheo chake cha kijeshi-- Jenerali.

..baada ya hapo ndio akapelekwa kuwa rc shinyanga.

cc BAK
 
..lakini kiwelu alishatangazwa kuwa ameteuliwa kuwa Jenerali na kuwa balozi wetu ufaransa. baadae tukasikia ameteuliwa mkuu wa mkoa wa shinyanga. sasa ktk kuulizauliza kwa wakongwe wa JF wa wakati huo jamaa mmoja akasema kiwelu ameponzwa na cheo chake cha Ujenerali. Ati wafaransa hawapendi mabalozi wenye mavyeo makubwa ya kijeshi.
 
Mkuu hii ni ya kushangaza kuwa kimya kimya
pia tumetafuta picha zake mahali popote hazijaonekana licha ya ile iliyowekwa kwenye jeneza hakuna
ni kweli mnavyosema Wafaransa walimkataa na alipofika Shinyanga ndio kabisa akaharibu kwenye mashimo ya dhahabu kuwafukia wachimbaji.
Kitendo cha kurudishwa Makao Makuu bado sikiafiki ila naona alipigana na baadae kurudi Makao makuu kuongoza zaidi. sehemu naitafuta wanasema alitumwa Nchi za nje hasa zile zilizotupa msaada wa kivita na hata maaadui zetu alienda (hii naitafuta nitaileta kuna mpiganaji alinukuliwa)
Mwisho ni hichi cha kuwa Jenerali (4Star) bila ya kuwa CDF yote naona km mawaa ktk Historia yake
 

JokaKuu
Kiwelu amepata mafunzo ya officer cadet Sandhurst. sasa niambie Kiaro na Musuguri wamepata mafunzo yao wapi kama siyo kwa promotions za Africanization!!
..Kiwelu alikuwa chief of staff wa Twalipo. Ina maana alikuwa senior kwa Musuguri na Kiaro.
..Kiwelu aliongoza mapambano ya kumuondoa Amini ktk ardhi ya Tanzania. Baada ya hapo akarudi ngome kwenye planning na logistics. Hiyo inaonyesha jinsi gani wataalamu wa aina yake wako flexible na well rounded.
..Kabla na baada ya vita vya Kagera, Kiwelu alikuwa senior kwa Musuguri, lakini akapitwa kwenye promotion ya kuwa CDF.
..Kiwelu tena kama Major General alikuwa senior kwa Kiaro, lakini Kiaro akawa promoted to General na Kiwelu to Lt.Gen, and Kiwelu was made to serve under Kiaro kama Chief of Staff.
..Maj-Gen.Herman Lupogo ni graduate wa Makerere. Pia aliwahi kuwa CO wa Monduli. Wasomi hao ndiyo wameweka standards pale mpaka tunaheshimika kimataifa. Makamanda wote wa Monduli walikuwa wasomi na waliopata mafunzo ktk vyuo vinavyoeleweka vya kijeshi.​



Mkuu JokaKuu hii sasa ndio ingekaa huku km Hisrtoria na kumbukumbu ya Gen Kiwelu kwa vizazi vya sasa vinavyojiunga JF
 

..kuna uzi mwingine ulihusu mahojiano aliyofanya na gazeti la raia mwema nadhani huo ni mzuri zaidi.

..tafuta pia uzi wa Ahmed Kitete, Muhidin Kimario, Silas Mayunga, na makamanda wengine wa vita vya Kagera.
 
Kwani ukiwa generali lazma uwe CDF? Kumbuka CDF anachaguliwa mmoja tu na kwenye jeshi huwa kunakuwa na majenerali wengi yeye alikuwa chief of staff (CoS) cheo ambacho ni kikubwa chini ya CDF!
 
Hata Sarakikya na Nyirenda na Jamal pia walisoma Sandhurst hii kurukwa vyeo ni suala la utashi wa mteuzi ambae ni Rais ila kuwa CoS sio cheo kidogo rankwise!

Msuguri hakuenda Sandhurst kwavile commission yake ilikuwa kipindi cha ukoloni na kipindi hicho nafasi ya shule kwa waafrika ilikuwa nadra ila alipanda cheo mpaka u-sergeant na platoon commander hazikuwa rank rahisi kipindi cha ukoloni!

At the time Msuguri na Twalipo were highest ranked African soldiers under KAR. Not a small feat!
 
Kwani ukiwa generali lazma uwe CDF? Kumbuka CDF anachaguliwa mmoja tu na kwenye jeshi huwa kunakuwa na majenerali wengi yeye alikuwa chief of staff ambacho ni cheo kikubwa chini ya CDF!

..imezoeleka kwamba askari anayepewa cheo kikubwa kupita vyote jeshini, ktk wakati husika, huteuliwa kuwa Mkuu wa majeshi.

..kwa hapa Tz, sasa hivi cheo hicho ni General [ 4 Star general ] kwamba Raisi akishakupa cheo hicho basi mazoea au matarajio ni kuwa mhusika atateuliwa kuwa Cdf.

..kilichotokea ni Raisi Mkapa kumpandisha Luteni Jenerali Kiwelu wakati huo CoS kuwa Jenerali lakini badala ya kumteua kuwa Cdf akamteua kuwa Balozi wa Tz Ufaransa.

..Nadhani tukio hilo ndilo linalowapa maswali mengi wadadisi na wapenda ujeshi-jeshi hapa JF.

..Swali linaloulizwa ni Tumainieli Kiwelu ni nani? Kwanini alipewa Ujenerali wakati hakuwa mkuu wa majeshi?

..Kwa maoni yangu Amiri Jeshi Mkuu Rais Mkapa alikuwa anatambua mchango wa Kiwelu jeshini. Yeye ndiye Mtanzania pekee aliyetumikia kaa CoS mara mbili. Aliaminiwa ktk nafasi hiyo na Maraisi wawili.

..Jambo lingine, Kiwelu ndiye CoS aliyetumikia wakati nchi iko VITANI. Na anakumbukwa kama kamanda aliyeongoza operation Chakaza iliyokomboa ardhi ya Tz toka mikononi mwa majeshi ya Idi Amin.

..Kwa maoni yangu, utumishi wa muda mrefu jeshini na uliotukuka ndio uliopelekea Raisi Mkapa kumpa Tumainieli Kiwelu Ujenerali na baadae kumteua Balozi.

Cc Nguruvi3
 
sasa ni hivi si lazma ukiwa generali kuwa CDF kwa vile ni mmoja tu kwenye jeshi huwa na cheo hicho fuatilia majeshi mengi yanayofuata ranking system za Kiingereza hata za Kichina! CoS or CoDS or CoAS mara nyingi huwa ni cheo cha General au Leutenant General! Inategemea kuna magenerali wangapi! Na mara nyingi baada ya vita magenerali huwa wengi maana yeyote wa cheo cha major general au Leutenant general is likely to be promoted!
 

..kwa hapa Tz, kutokana na muundo, na ukubwa wa jeshi letu, cheo au rank ya juu kabisa ni Jenerali [ 4 star general ].

..Vivyo hivyo cheo cha pili kwa ukubwa ktk jeshi letu ni Luteni Jenerali [ 3 star general].

..Raisi akimpandisha askari cheo kuwa Jenerali maana yake amelenga kumteua kuwa Cdf.

..Vilevile Raisi akimpandisha askari cheo kuwa Luteni Jenerali maana yake amelenga kumteua kuwa CoS.

..Hivyo basi Cdf lazima awe the most senior General / 4 star general in active duty.

..Vivyo hivyo CoS lazima awe the most senior Lieutenant General serving in the army.

..Haijawahi kutokea ktk historia ya JWTZ kuwa na Cdf mwenye rank inayolingana na askari mwingine in active duty.

..Sarakikya alikuwa Cdf na Major General pekee jeshini. Twalipo alipoteuliwa Major General, Sarakikya aliondolewa jeshini na kuteuliwa Waziri.
 
Huyu Afande alikuwa si mtu wa maneno mengi na ni kweli hakupendelea mambo ya kitoto. Licha ya CV nzuri ya utumishi wake ambayo JWTZ imeweka, ni bora kutambua pia kuwa akiwa Chuo cha Mafunzo ya Uofisa pale Sandhurst, England, alinunukiwa kuwa mwanafunzi wa kwanza kwa ubora katika mafunzo yote kati ya wanafunzi wa Commonwealth na nchi nyingine wa mwaka wake ukiacha Wanafunzi wa Uingereza ambao huwa wanashindanishwa wenyewe kwa wenyewe. Kuweza kufuzu hiyo nafasi ya kuwa wa kwanza siyo mchezo ingawa kuna Watanzania wengine wamewahi pia kupata sifa hiyo nakumbuka mwaka 1989 pia nchi yetu ilitoa mpiganaji mwingine katika ubora huo. Hii ina maana huyu Afande Kiwelu alikuwa jeshi "material" tangu akiwa na umri mdogo! Hakubahatisha. RIP Commander!

Sent from my ONEPLUS A5000 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…