..imezoeleka kwamba askari anayepewa cheo kikubwa kupita vyote jeshini, ktk wakati husika, huteuliwa kuwa Mkuu wa majeshi.
..kwa hapa Tz, sasa hivi cheo hicho ni General [ 4 Star general ] kwamba Raisi akishakupa cheo hicho basi mazoea au matarajio ni kuwa mhusika atateuliwa kuwa Cdf.
..kilichotokea ni Raisi Mkapa kumpandisha Luteni Jenerali Kiwelu wakati huo CoS kuwa Jenerali lakini badala ya kumteua kuwa Cdf akamteua kuwa Balozi wa Tz Ufaransa.
..Nadhani tukio hilo ndilo linalowapa maswali mengi wadadisi na wapenda ujeshi-jeshi hapa JF.
..Swali linaloulizwa ni Tumainieli Kiwelu ni nani? Kwanini alipewa Ujenerali wakati hakuwa mkuu wa majeshi?
..Kwa maoni yangu Amiri Jeshi Mkuu Rais Mkapa alikuwa anatambua mchango wa Kiwelu jeshini. Yeye ndiye Mtanzania pekee aliyetumikia kaa CoS mara mbili. Aliaminiwa ktk nafasi hiyo na Maraisi wawili.
..Jambo lingine, Kiwelu ndiye CoS aliyetumikia wakati nchi iko VITANI. Na anakumbukwa kama kamanda aliyeongoza operation Chakaza iliyokomboa ardhi ya Tz toka mikononi mwa majeshi ya Idi Amin.
..Kwa maoni yangu, utumishi wa muda mrefu jeshini na uliotukuka ndio uliopelekea Raisi Mkapa kumpa Tumainieli Kiwelu Ujenerali na baadae kumteua Balozi.
Cc
Nguruvi3