Jenerali Ulimwengu apinga kutumia siku 100 kumtathimini Rais

Jenerali Ulimwengu apinga kutumia siku 100 kumtathimini Rais

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
14,747
Reaction score
24,250
Jenerali ulimwengu ambaye ni mwanahabari nguri amepinga vikali hatua ya kumpa Rais Samia Suluhu siku 100 za kumjadili.

Amesema kwanza hatupaswi kutumia njia hiyo sababu ni njia ambayo wamarekani ndiyo wanaitumia kwa viongozi wao iweje na sisi tuige wakati hatuya simamii malengo yetu.

Pia ameendelea kusema, hategemei jipya sababu bi Samia alikuwa msaidizi wa rais aliyepita na chama ni kile kile cha muda mrefu, hivyo matamko yoyote hayawezi kuleta jipya.

Jenerali amesema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na kituo cha redio cha sauti ya Marekani VOA.

Screenshot_20210702_200827.jpg

PICHANI: Jenerali Ulimwengu, picha haina uhusiano na mada.
 
Namuunga mkono jenerali 100%

Hii issue ya kusema nampa Rais siku 100 za kumtathmini imekaa kimaigizo zaidi, unampa siku 100 za nini wakati utendaji wa mtu unaanza kuonekana kuanzia siku yake ya kwanza akiwa ofisini?

Huu ni ustaarabu wa kimagharibi tulio copy ambao hauna maana kwetu, siasa ipo kila siku, na matukio yake yapo kila siku, uamuzi wa Rais wa siku moja unaweza kusababisha mvuragano wa aina yoyote.

Hapa lazima tuwe tayari kukemea au kusifia kulingana na utendaji wa Rais, habari za kumpa siku 100 waachiwe waandishi wa makala kwenye magazeti waje kuandika kulingana na mitazamo yao, lakini kwa wanasiasa, hakuna haja ya kusubiri siku 100 ni kujipotezea muda tu.

After all, baada ya hizo siku 100, bado kuna uwezekano mkubwa wa kurudi kulekule kuanza kupiga kelele pale Rais anapokosea, au kumsifia anapopatia, so siku 100 kwangu naona ni maigizo tuliyo copy yasiyo na maana.
 
Nakubaliana naye 💯%.


Unapinga nini na unafanya nini???

Unapinga siku 100 za mama samia lakini unaipenda 💯%, kwanini isingekuwa 2% au 40% nk, kwanini dunia ichague kwamba kitu kamili kiwe 💯% na sio 200%??
 
Mzee wangu Mungu ampe maisha marefu ,hakuwi niangusha, watu Kama awa bila kujali misimamo yao ilitakiwa rais madarakani kuwaomba kuwa washauri wake, sio kuchukua watu ili mradi wanakupongeza tu kumbe ni wanafiki
 
Mimi napinga hiyo 💯% yako kama jinsi wewe unavyopinga siku 💯 za Rais samia Suluhu.
 
Nami nimemsikia ila Gwandumi Mwakatobe kaongea vizuri zaidi,ikiwezekana tubandikie na ya Gwandumi
Tatizo la Gwandumi lilikuwa ni kumsifia jenerali akashindwa kufunguka na kila akitaka kufunguka anapiga break akishtuka kuwa mama Samia ni amiri jeshi so awezi kumwaga madini as jenerali.
 
Unapinga nini na unafanya nini???

Unapinga siku 100 za mama samia lakini unaipenda [emoji817]%, kwanini isingekuwa 2% au 40% nk, kwanini dunia ichague kwamba kitu kamili kiwe [emoji817]% na sio 200%??
Hii dunia ina watu sijui mnawaza kwa kutumia nini? Unajua utofauti wa asimia 100 na siku 100 ivyo ni vitu viwili tofauti sana kimaana na kimahesabu mkuu. Mbona kwenye teknolojia tunasema gb 1= mb 1024 kwanini tusiseme 1000 mb ? Usifananishe vitu bila kutumia reasoning na kujenga hoja
 
Back
Top Bottom