Jenerali Ulimwengu apinga kutumia siku 100 kumtathimini Rais

Jenerali Ulimwengu apinga kutumia siku 100 kumtathimini Rais

Tulikuwa pamoja na Jenerali Ulimwengu jioni ya leo kwenye mahojiano yaliyoongozwa na Mkamiti Kibayasi wa VOA
😂
Kama ulikuwepo mbona ulikuwa unalukaluka kuongea reality from real management power?.
 
Hata kutokutathminini ni kutathmini. Ukisema alikuwa msaidizi wa aliyepita kwa hiyo hawezi kwa tofauti nako ni kutathmini. Hi ya America ni akili kuyumba kwa sababu zisizo wazi, we ignore that.
Mkuu tumjadili Jenerali alichosema not me!.
 
Wewe unajua kusoma na kutafakari unachosoma au umezoea ku crame???--- hiyo ndiyo shida ya elimu zetu. Hebu soma hiki nilichoandika;
Acha kutoka nje ya hoja yangu hoja zangu ni mbili tu.

1. Kwanini ufananishe siju 100 na asilimia 100 vitu ambavyo
Havifanani hata kidogo kimaana na kimahesabu?

2. Kwanini useme tunataka kitu hadi kianzishwe na wazungu ndo tukikubali bila kujua evaluation ya siku 100 imeanzishwa na wazungu na tume copy marekani?

Hakuna maali nimekukubalia au kukukatalia kutumika kwa siku 100. Sijapenda tu kuona kuwa kwenye comment zako hamna reasoning bali emotions.
 
Bingwa wakukaza sipana kitambo sana ,alikataaga teuzi enzi ya nyerere huyu
 
[emoji23]
Kama ulikuwepo mbona ulikuwa unalukaluka kuongea reality from real management power?.
Ielezee hapa hiyo real management power iliyokosekana kwangu. Hili nalo ni jukwaa la kutoa maoni kama ilivyo redio. Ila weka r na andika rukaruka, siyo "lukaluka"

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
hata mimi namuunga mkono , tanzania kama nchi hatuna misingi ya kitaifa hivyo hatuwezi kumpima rais kwa siku 100 kwa sababu kila rais anapokuja anaanza upya
 
Jenerali ulimwengu ambaye ni mwanahabari nguri amepinga vikali hatua ya kumpa Rais Samia Suluhu siku 100 za kumjadili.

Amesema kwanza hatupaswi kutumia njia hiyo sababu ni njia ambayo wamarekani ndiyo wanaitumia kwa viongozi wao iweje na sisi tuige wakati hatuya simamii malengo yetu.

Pia ameendelea kusema, hategemei jipya sababu bi Samia alikuwa msaidizi wa rais aliyepita na chama ni kile kile cha muda mrefu, hivyo matamko yoyote hayawezi kuleta jipya.

Jenerali amesema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na kituo cha redio cha sauti ya Marekani VOA.

View attachment 1838069
PICHANI: Jenerali Ulimwengu, picha haina uhusiano na mada.

Kuna hoja mbili hapo:

Hoja ya kwanza ni kwamba, "hatupaswi kutumia njia hiyo (ya siku 100 kupima utendaji wa Rais kwa) sababu"

  • (1) "ni njia ambayo wamarekani ndiyo wanaitumia kwa viongozi wao" na
  • (2) "sisi ...hatuyasimamii malengo yetu" kama wanavyofanya wamarekani.
Na hoja ya pili ni kwamba, Ulimwengu "hategemei jipya (kwa) sababu"
  • (1) "Samia alikuwa msaidizi wa rais aliyepita (Magufuli),"
  • (2) "chama ni kile kile cha muda mrefu (cha CCM)," na
  • (3) "matamko yoyote hayawezi kuleta jipya" bila mabadiliko ya kimfumo yanayoanzia nje.

Hoja ya kwanza inaweza kupingwa kwa sababu kama vile:
  • Kwamba, kuna ushahidi kwamba tumeiga mambo mengi kutoka nje;
  • Kwamba, miezi mitatu ni muda mzuri wa matazamio kwa mwajiriwa mpya popote; na
  • Kwamba, bila tathmini hiyo ya siku 100 hatuwezi kujua kama Rais amesimamia malengo ya Taifa au hapana.
Kwa hiyo, inayumba.

Hoja ya pili inaweza kupingwa kwa sababu kama vile:

  • Kwamba, kuna uwezekano wa mabadiliko kuanzia ndani ya mfumo kwa sababu ya minyukano ya ndani, na ushahidi ndani ya siku 100 za Samia umeanza kupatikana;
  • Kwamba, kuna uwezekano wa mabadiliko kuanzia ndani ya mfumo kwa sababu ya mabadiliko ya uongozi, na ushahidi ndani ya siku 100 za Samia umeanza kupatikana;
Kwa hiyo, inayumba.

Kwa hiyo, hoja zote mbili zinahitaji ushahidi wa nyongeza ili tuweze kuelewa msemaji alikuwa na msingi gani wa kutamka aliyoyasema; na hatimaye kushawishika kuwa upande wake.

Lakini, mpaka sasa ushahidi wake hautoshi.
 
Unapenda kufikiria kwa mantiki uliyoikuta au unapenda kufikiria kwa usahihi?Anza na hilo.

Chochote chenye mantiki kina usahihi. Siku 100 za Samia zina mantiki na jinsi 💯% ilivyokuwa na usahihi na mantiki.
 
Acha kutoka nje ya hoja yangu hoja zangu ni mbili tu.

1. Kwanini ufananishe siju 100 na asilimia 100 vitu ambavyo
Havifanani hata kidogo kimaana na kimahesabu?

2. Kwanini useme tunataka kitu hadi kianzishwe na wazungu ndo tukikubali bila kujua evaluation ya siku 100 imeanzishwa na wazungu na tume copy marekani?

Hakuna maali nimekukubalia au kukukatalia kutumika kwa siku 100. Sijapenda tu kuona kuwa kwenye comment zako hamna reasoning bali emotions.

Haya sasa twende kimahesabu; kwanini iwe ni 💯% (100 per cent) na isiwe 1000 per milli ??!!,
 
Haya sasa twende kimahesabu; kwanini iwe ni [emoji817]% (100 per cent) na isiwe 1000 per milli ??!!,
Acha kuniuliza maswali jibu hoja. Kubali tu ulikua hujui kuwa waanzilishi wa siku 100 za raisi sio sisi na tume copy . Acha undezi
 
Namuunga mkono jenerali 100%

Hii issue ya kusema nampa Rais siku 100 za kumtathmini imekaa kimaigizo zaidi, unampa siku 100 za nini wakati utendaji wa mtu unaanza kuonekana kuanzia siku yake ya kwanza akiwa ofisini?

Huu ni ustaarabu wa kimagharibi tulio copy ambao hauna maana kwetu, siasa ipo kila siku, na matukio yake yapo kila siku, uamuzi wa Rais wa siku moja unaweza kusababisha mvuragano wa aina yoyote.

Hapa lazima tuwe tayari kukemea au kusifia kulingana na utendaji wa Rais, habari za kumpa siku 100 waachiwe waandishi wa makala kwenye magazeti waje kuandika kulingana na mitazamo yao, lakini kwa wanasiasa, hakuna haja ya kusubiri siku 100 ni kujipotezea muda tu.

After all, baada ya hizo siku 100, bado kuna uwezekano mkubwa wa kurudi kulekule kuanza kupiga kelele pale Rais anapokosea, au kumsifia anapopatia, so siku 100 kwangu naona ni maigizo tuliyo copy yasiyo na maana.
Well said
 
Hii dunia ina watu sijui mnawaza kwa kutumia nini? Unajua utofauti wa asimia 100 na siku 100 ivyo ni vitu viwili tofauti sana kimaana na kimahesabu mkuu. Mbona kwenye teknolojia tunasema gb 1= mb 1024 kwanini tusiseme 1000 mb ? Usifananishe vitu bila kutumia reasoning na kujenga hoja
Umepiga za uso kweli kweli
 
Acha kuniuliza maswali jibu hoja. Kubali tu ulikua hujui kuwa waanzilishi wa siku 100 za raisi sio sisi na tume copy . Acha undezi

Wewe Mao Tsetung hakuwa mburula kama wewe Mao Zedong feki, nakwambia soma hapa uone kama sikujua kama nchi zingine hatumia siku 100 kutathimini utendaji wa viongizi wao. Kwenye percentage umeshindwa na kimsingi kama hujui nini maana ya percentage basi hukuwa na moral authority ya kuhoji hoja yangu niliyohusisha na siku 100 za Mama Samia. Angalia nilichosema kuhusiana na Siku 100:-

Maana yangu ni hii; kupanga ni kuchagua, kama tumepanga na kuamua kutathimini Uongozi wa mama katika kipindi cha siku 100 kitu ambacho nchi zingine nazo hufanya hapo hakuna kosa
 
Jenerali ulimwengu ambaye ni mwanahabari nguri amepinga vikali hatua ya kumpa Rais Samia Suluhu siku 100 za kumjadili.

Amesema kwanza hatupaswi kutumia njia hiyo sababu ni njia ambayo wamarekani ndiyo wanaitumia kwa viongozi wao iweje na sisi tuige wakati hatuya simamii malengo yetu.

Pia ameendelea kusema, hategemei jipya sababu bi Samia alikuwa msaidizi wa rais aliyepita na chama ni kile kile cha muda mrefu, hivyo matamko yoyote hayawezi kuleta jipya.

Jenerali amesema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na kituo cha redio cha sauti ya Marekani VOA.

View attachment 1838069
PICHANI: Jenerali Ulimwengu, picha haina uhusiano na mada.
Kwani mi ni nani nibishane nae.
 
Wewe Mao Tsetung hakuwa mburula kama wewe Mao Zedong feki, nakwambia soma hapa uone kama sikujua kama nchi zingine hatumia siku 100 kutathimini utendaji wa viongizi wao. Kwenye percentage umeshindwa na kimsingi kama hujui nini maana ya percentage basi hukuwa na moral authority ya kuhoji hoja yangu niliyohusisha na siku 100 za Mama Samia. Angalia nilichosema kuhusiana na Siku 100:-
Ok mkuu ngoja nikikubalie ila jua tu " mtu anapokua ni kichaa hajui kama ye ni kichaa bali wanaoa athirika na ukichaa wake ndo wanaumia" unahitaji akili kubwa kuelewa nilicho andika. [emoji23][emoji23][emoji23]

Mtu akikosa hoja bana umeangalia hadi jina naitwa nani then ukaanza kufanya personal attack kwenye jina hii mbinu huwa inatumiwa sana na watu ambao ni vichaa
 
Back
Top Bottom