Gwappo Mwakatobe
JF-Expert Member
- Nov 22, 2019
- 1,730
- 2,230
Tulikuwa pamoja na Jenerali Ulimwengu jioni ya leo kwenye mahojiano yaliyoongozwa na Mkamiti Kibayasi wa VOAJenerali ulimwengu ambaye ni mwanahabari nguri amepinga vikali hatua ya kumpa bi Samia Suruhu siku 100 za kumjadili.
Amesema kwanza hatupaswi kutumia njia hiyo sababu ni njia ambayo wamarekani ndiyo wanaitumia kwa viongozi wao iweje na sisi tuige wakati hatuya simamii malengo yetu.
Pia ameendelea kusema, hategemei jipya sababu bi Samia alikuwa msaidizi wa rais aliyepita na chama ni kile kile cha muda mrefu, hivyo matamko yoyote hayawezi kuleta jipya.
Jenerali amesema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na kituo cha redio cha sauti ya Marekani VOA.
View attachment 1838069
PICHANI: Jenerali Ulimwengu, picha haina uhusiano na mada.
Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app