Namuunga mkono jenerali 100%
Hii issue ya kusema nampa Rais siku 100 za kumtathmini imekaa kimaigizo zaidi, unampa siku 100 za nini wakati utendaji wa mtu unaanza kuonekana kuanzia siku yake ya kwanza akiwa ofisini?
Huu ni ustaarabu wa kimagharibi tulio copy ambao hauna maana kwetu, siasa ipo kila siku, na matukio yake yapo kila siku, uamuzi wa Rais wa siku moja unaweza kusababisha mvuragano wa aina yoyote.
Hapa lazima tuwe tayari kukemea au kusifia kulingana na utendaji wa Rais, habari za kumpa siku 100 waachiwe waandishi wa makala kwenye magazeti waje kuandika kulingana na mitazamo yao, lakini kwa wanasiasa, hakuna haja ya kusubiri siku 100 ni kujipotezea muda tu.
After all, baada ya hizo siku 100, bado kuna uwezekano mkubwa wa kurudi kulekule kuanza kupiga kelele pale Rais anapokosea, au kumsifia anapopatia, so siku 100 kwangu naona ni maigizo tuliyo copy yasiyo na maana.