Kuhusu COVID bado Magufuli ni shujaa,,
Niambie Leo kuna inchi gani bado wanaweka watu wao lock down?
Au caranteen.
Au bado wanavaa barakoa?
Magufuli alisema huu ugonjwa ni wa kupuuza,
Na sasa dunia imeupuuza ugonjwa wa COVID.
Nikikusoma naona madhara ya Magufuli kama alivyosema Jenerali ''imbecilization''
Ni kwamba dunia inafunguka kwasababu wataalam wanaujua ugonjwa na chanjo imesaidia sana kupunguza hospitalization na death. Kuna watu ni asymptomatic wanagundua katika routine check up
Magufuli, kwanza, hakukubali uwepo wa virus akipima mafenesi kwa vipimo vya virus
Huwezi kupata matokeo ya sampuli tofauti katika vipimo vyenye specifications
Pili, magufuli kazuia watu wasiseme kuna virus hata pale watu walipokufa.
Kwamba hakuna tatizo, watu wanazika . Kusema COVID ikawa ni jinai !
Tatu, Magufuli akahamsisha maombi. Saudia Arabia wakafunga kwenda Hijja, Vatican wakafunga makanisa. Papa akavaa barakoa , Masheikh wakavaa barakoa.
Magufuli anaamini Tanzania ina Mungu tofauti na sehemu nyingine.
Anakusanya watu wanaambukizana wanakufa huko huko katika mikusanyiko
Magufuli kaaminisha umma vaccine ni mradi wa wazungu.
Kawanyima Raia fursa kwa utashi wake akiwalaghai wachemshe majani.
Waziri kaenda kuchukua mchachai Madagascar.Huko alikokwenda kuchuku watu walikufa mpaka WHO ikaingilia kati. Akajenga mtambo wa kufukiza muhimbili! dah!
Kuna ushujaa wa aina gani.
Kuhusu kusemwa vibaya Magufuli,Hivi Magufuli hakuwa na mazuri?
Sijaona yeyote msafii akamsema vibaya Magufuli.
Wengi wanaomsema vibaya ni wale watu waliopokonywa maslahi yao kwa njia moja au nyingine.
Kama kweli ni wazalendo wa kweli waongee mabaya ya waliohai.
Sio kuendelea kupambana na marehemu...
Magufuli aliishi kwa kodi za Watanzania kama alivyoishi Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete
Wote hao tunawasema kwa mazuri na mabaya yao hakuna 'excuse' yoyote
Kinachotofautisha ni rekodi . Kila mtu atavuna alichopanda na hapo ndipo utaona tofauti
Kumsema Magufuli vibaya tu bila sababu si jambo jema, kueleza rekodi yake bila kupepesa ni kumtendea haki. Rekodi inahusisha yaliyoambatana na utawala iwe Magufuli au Nyerere