Jenerali Ulimwengu: Kuna Mtanzania alitufanya Mazuzu

Jenerali Ulimwengu: Kuna Mtanzania alitufanya Mazuzu

Kwenye hili gazeti lako,kitu cha maana ni kuwaaminisha Watzn kwamba Katiba ndio muarobaini.

Pili hili la scholarships na exposure ni muhimu sana kuepusha viongozi mazuzu kama bwana yule..

Japo umeponda sana ila scholarships huwa zipo Sana tuu sema Watzn ni wazito Sana kuchangamkia fursa za nje.
Scholarship maalum kwa watanzania si nyingi, zilizopo ni za ujumla. Sijui haujaelewa nilichokieleza. Nchi nyingi wana scholarship maalum kwa nchi zao, achana na hizi za jumla jumla.
Pia Uvivu wa watanzania na hasa kusoma, hudhani kila kitu ni gazeti. Na mtu amtukanae mwingine akili yake umtuma yeye yuko sahihi kumbe waweza kuta yeye ndo zuzu. Siku zote kichaa au mweu uwaona watu wengine ndo vichaa. Nyani haoni kundule.
 
Kuliko kukaa kimya na kujifanya hayakutokea, bora kusema ili watu wajifunze na kuhakikisha huo ujinga haujirudii tena. Ndio maana ya historia.
Ndo mnajidanganya, kwa wale waliompenda ni ngumu kugeuza imani yao kwake. Kelele za chura hazimzuiii ng'ombe kunywa maji.
 
Umeandika gazeti reeefu!! Uzuzu mtupu! Wewe ni yale mazuzu ya Magu yaliyojificha
Kuna sheria inayoweka viwango vya kuandika. Uzuzu upo nao wewe ambaye unadhani wengine ni mazuzu. Nawasiwasi na malezi uliyapata kwa wazazi wako. Mwana mwema hatokwi na maneno ya ovyo kinywani mwake, bali alie mpumbavu na mwenye malezi yasiyo na maadili.
Alie wadanganya kuwa ukitukana umeshinda, kawaona ninyi ni mazuzu msietumia akili zenu.
 
Kuna sheria inayoweka viwango vya kuandika. Uzuzu upo nao wewe ambaye unadhani wengine ni mazuzu. Nawasiwasi na malezi uliyapata kwa wazazi wako. Mwana mwema hatokwi na maneno ya ovyo kinywani mwake, bali alie mpumbavu na mwenye malezi yasiyo na maadili.
Alie wadanganya kuwa ukitukana umeshinda, kawaona ninyi ni mazuzu msietumia akili zenu.
Nenda Chato huko ukalinde legacy 🚮
 
miaka takribani 6 na ushee nchi ilizimika kifkra kabisa akabakia mtu mmoja tu, yeye ndiyo aongee sisi tumsikilize - hatari kubwa.
 
Sasa tungefanyaje? Nani aliyekuwa tayari kupotezwa na kuuawa?
 
nashukuru Mungu mimi sikuwa zuzu, mazuzu wapo hata humu
Hasa kule lum
1649680034006.png
 
Kuhusu COVID bado Magufuli ni shujaa,,
Niambie Leo kuna inchi gani bado wanaweka watu wao lock down?
Au caranteen.
Au bado wanavaa barakoa?
Magufuli alisema huu ugonjwa ni wa kupuuza,
Na sasa dunia imeupuuza ugonjwa wa COVID.
Nikikusoma naona madhara ya Magufuli kama alivyosema Jenerali ''imbecilization''

Ni kwamba dunia inafunguka kwasababu wataalam wanaujua ugonjwa na chanjo imesaidia sana kupunguza hospitalization na death. Kuna watu ni asymptomatic wanagundua katika routine check up

Magufuli, kwanza, hakukubali uwepo wa virus akipima mafenesi kwa vipimo vya virus

Huwezi kupata matokeo ya sampuli tofauti katika vipimo vyenye specifications

Pili, magufuli kazuia watu wasiseme kuna virus hata pale watu walipokufa.
Kwamba hakuna tatizo, watu wanazika . Kusema COVID ikawa ni jinai !

Tatu, Magufuli akahamsisha maombi. Saudia Arabia wakafunga kwenda Hijja, Vatican wakafunga makanisa. Papa akavaa barakoa , Masheikh wakavaa barakoa.

Magufuli anaamini Tanzania ina Mungu tofauti na sehemu nyingine.
Anakusanya watu wanaambukizana wanakufa huko huko katika mikusanyiko

Magufuli kaaminisha umma vaccine ni mradi wa wazungu.
Kawanyima Raia fursa kwa utashi wake akiwalaghai wachemshe majani.

Waziri kaenda kuchukua mchachai Madagascar.Huko alikokwenda kuchuku watu walikufa mpaka WHO ikaingilia kati. Akajenga mtambo wa kufukiza muhimbili! dah!

Kuna ushujaa wa aina gani.
Kuhusu kusemwa vibaya Magufuli,Hivi Magufuli hakuwa na mazuri?
Sijaona yeyote msafii akamsema vibaya Magufuli.

Wengi wanaomsema vibaya ni wale watu waliopokonywa maslahi yao kwa njia moja au nyingine.

Kama kweli ni wazalendo wa kweli waongee mabaya ya waliohai.
Sio kuendelea kupambana na marehemu...
Magufuli aliishi kwa kodi za Watanzania kama alivyoishi Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete
Wote hao tunawasema kwa mazuri na mabaya yao hakuna 'excuse' yoyote

Kinachotofautisha ni rekodi . Kila mtu atavuna alichopanda na hapo ndipo utaona tofauti

Kumsema Magufuli vibaya tu bila sababu si jambo jema, kueleza rekodi yake bila kupepesa ni kumtendea haki. Rekodi inahusisha yaliyoambatana na utawala iwe Magufuli au Nyerere
 
Hivi siku ya hukumu Mungu anakwambia utoe ushahidi wa hiyo tuhuma kwamba sisi watanzania tulimuabudu Mwendazake je, utaweza kutoa ushahidi mbele za Mungu?
Mungu ninayemuabudu hafanyi kazi kizembe hivyo!!
 
Basi hatendi haki huyo Mungu unayemuabudu, maana sie wengine tunaamini Mungu ndio mtenda haki.
Ni mtenda haki ndiyo maana amerahisha mtu mwovu anashughulikiwa kwa uovu wake bila delay kabla hajaondoka duniani!
 
Ni mtenda haki ndiyo maana amerahisha mtu mwovu anashughulikiwa kwa uovu wake bila delay kabla hajaondoka duniani!
Sio kweli mbona kuna watu wengi tu hadi wanakufa hawajalipa uovu wao.
 
Back
Top Bottom