Jenereta: Fahamu Aina, Matumizi Sahihi, Matengenezo na Namna ya Utunzaji wake

Mbwambo

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2008
Posts
625
Reaction score
95
​

Wapendwa, nimechoka na kero za kukatika umeme kila mara. Nimeamua kutafuta generator japo napo ninatafuta makelele ya mngurumo wake.

Je, nitapata wapi generator nzuri kwa kijihela changu cha laki 4? Yaani 400,000/=.

Vitu vyangu ni vya kawaida: fridge 2, taa kama 13 hivi, microwave, tv set, pasi 2, etc.

Je, kwa hela kama hiyo nitapata generator? Aina gani ndio nzuri?

Nisaidieni waungwana.


MAHITAJI YA WADAU KUHUSU JENERETA​


MICHANGO YA WADAU ​

MATENGENEZO YA JENERETA ZA DIZELI​

ZAIDI, SOMA:

AINA ZA JENERETA, SIFA, MATUMIZI NA MUONGOZO WA MATENGENEZO​

Jenereta hufanya nini?
Jenereta kimsingi ni mwokozi katika maisha. Ni vyanzo vya nishati ambavyo vinabadilisha gesi ya propane, dizeli au petroli, kuwa nishati ya umeme. Ni vyanzo vya msingi vya usambazaji wa umeme wakati wa umeme kukatika.

Aina za jenereta
Kuna aina tatu kuu ya jenereta: portable, inverter na standby. Licha ya tofauti zao, jenereta hizi zote zinapaswa kupitia matengenezo sawa ili kuhakikisha matumizi ya muda mrefu.

Jenereta Potable

Jenereta portable inaendeshwa na gesi au mafuta ya dizeli na inaweza kutoa nguvu za umeme kwa muda mchache.

Hapa kuna sifa kadhaa za kuzingatia kuhusu aina hizi za jenereta:
  • Inatumia injini-mwako kutengeneza nishati.
  • Unaweza kutumia vifaa vya umeme kupitia soketi zake.
  • Inaweza kutumika katika maeneo ya mbali, yaani ya ndanindani
  • Ina uwezo wa kutosha kuendesha televisheni, friza na jokofu.
  • Injini inapaswa kuwa katika kasi ya 3600 rpm kutoa kiwango cha 60hz cha mkondo.
  • Inatumia gavana kudhibiti kasi ya injini.
  • Zinaweza kuendesha zana na taa za majumbani
Jenereta ya Inverter

Jenereta ya inverter hutumia injini iliyounganishwa na mbadala kutengeneza nguvu ya AC. Pia hutumia kiambatisho tofauti na jenereta zingine kubadilisha nguvu ya AC kuwa nguvu ya DC.

Hapa kuna sifa kadhaa za kuzingatia kuhusu aina hizi za jenereta:
  • Hutegemea kwenye sumaku za teknolojia ya hali ya juu.
  • Inatumia mzunguko wa umeme wa hali ya juu.
  • Kupitia hatua tatu za kutengeneza umeme.
  • Inadumisha mtiririko wa mkondo wa umeme kwa vifaa.
  • Ina nguvu zaidi, kwani kasi ya injini inajirekebisha kulingana na nguvu kiasi gani inahitajika.
  • AC yake inaweza kusetiwa kwa voltage yoyote na frequency kama ikitumiwa na vifaa sahihi.
  • Huwa ni ndogo na nyepesi.
  • Inaweza kutosha katika gari au boti ndogo.

Jenereta ya standby

Jenereta hii ni mfumo wa umeme ambao moja kwa moja unaiamuru kupeleka nishati katika vifaa vya umeme pindi tu umeme unapokatika. Hizi ni zile jenereta ambazo zinajiwasha mara tu baada ya umeme kukatika, yaani huhitaji kuiwasha manually.

Hapa kuna sifa kadhaa za kuzingatia kuhusu aina hizi za jenereta:
  • Inafanya kazi kiautomati, yaani ni automatic
  • Hutoa nishati ya umeme ya kuaminika
  • Inaweza kufanya kazi kwa propane au gesi asilia.
  • Inatumia combustion engine ya ndani.
  • Ina uwezo wa kuhisi kukatika kwa umeme ndani ya sekunde chache na huongeza umeme haraka sana ili mtumiaji asipate adha ya kutokuwa na umeme hata kwa muda mfupi tu.
  • Hujifanyia majaribio ya kila wiki moja ili kuona kuwa ina-respond vizuri dhidi ya upoteaji wa nishati na kwamba lipo katika utimamu wake.
  • Inatumika katika mifumo ya usalama kwenye lifti, taa za standdby, vifaa vya msaada wa matibabu, uokoaji wa maisha pamoja na mifumo ya kinga ya moto.

Jenereta kwa matumizi sahihi
Aina ya JeneretaMatumizi
PortableMajokofu (friji), mashine za kugongea misumari n.k
InverterBetri za gari, laptops nk
StandbyMahitaji ya dharura, lifti, vifaa na mashine za hospitali

Matengenezo ya jenereta
Utunzaji wa jenereta ni mchakato sawa na unaotumika miongoni mwa aina kuu tatu za injini. Kwanza, ni muhimu kufuata ratiba ya matengenezo iliyopendekezwa na mtengenezaji, yaani manufacturer, kwa kuzingatia aina ya jenereta husika.

Utaratibu wa matengenezo ya kawaida ni ule wa ukaguzi wa jumla. Uchunguzi unajumuisha kuangalia uvujaji, kukagua viwango vya mafuta na mafuta, kutazama mikanda na mirija na kuangalia vituo vya betri na nyaya. Ni muhimu kukagua mafuta pia, kwani lazima ibadilishwe mara kwa mara. Muda wa mafuta hutegemea mtengenezaji na aina ya jenereta. Ni mara ngapi jenereta inatumiwa na mazingira yako ya kazi. Kwa kawaida, inashauriwa kubadilisha mafuta baada ya masaa 100 ya kufanya kazi, haswa ikiwa jenereta hutumia dizeli.

Matengenezo ya jenereta yanahitaji:
Kusafisha na kuchuja mafuta kila mwaka. Kama mafuta ya dizeli huharibika haraka. Baada ya wiki chache za kufanya kazi, mafuta ya dizeli huharibika kupitia uchafuzi wa maji na vijidudu, hivyo kusababisha mistari na vichujio vya mafuta kuziba.

Kusafisha mafuta kunajumuisha kutumia biocides kila mwaka kwenye jenereta zote isipokuwa jenereta ya standby, ambayo yenyewe itaweka unyevu.

Mfumo wa upoozeshaji ni wa kutunzwa vyema, kwa kuangalia kiwango cha vimiminika vya kupoozesha. Hii lazima ifanyike wakati wa kuzima.

Kuangalia nguvu ya betri; hii ni kweli hasa kwa jenereta za standby, kwani masuala ya betri ndio sababu kuu ya aina hizi za jenereta kufeli. Hakikisha betri ni imara na zimechajiwa vya kutosha ili kudumu kwa muda mrefu na kutosababisha hitilafu wakati wa kuwasha jenereta.

Pima mara kwa mara ili kujua hali ya betri kwa wakati husika. Upimaji ni pamoja na kuangalia viwango vya electrolyte na nguvu maalum ya betri. Betri zenyewe pia lazima ziwe safi.

Utunzaji zaidi wa jenereta
Mbali na mambo hayo hapo juu, ni muhimu pia kuliwasha jenereta kila wiki kwa dakika 30 katika kipindi ambacho halitumiki mara kwa mara. Hii itasaidia kuchaji betri, kuondoa unyevu kupita kiasi, kutia mafuta injini na kuchuja mafuta na foil. Sehemu zozozte za Jenereta ambazo hazijakazwa vizuri ni lazima zirudishiwe mahala pake.

Unapaswa pia kuweka kumbukumbu za ukaguzi kwa ajili ya baadaye. Rekodi hizi zitakuruhusu kujua vizuri hali ya jenereta yako.
 
Wadau wa majenereta tunawasubiri mtumwagie mautaalam.
 
mvumilivu Wangu,

Nenda Kariakoo, mtaa wa uhuru, karibu na ile petrol station ya total, ilo dukaliko opp na na icho kituo cha mafuta.

Kwa laki 4, unapata generator nzuri kabisa.
 
nenda kariakoo, mtaa wa uhuru, karibu na ile petrol station ya total,ilo dukaliko opp na na icho kituo cha mafuta.

Kwa laki 4, unapata generator nzuri kabisa.

Asante kaka yangu, nitakwenda hapo kariakoo karibu na petrol station ya total. Asante na ubarikiwe.
 
Naomba mnaotumia generators mtufunze ni capacity gani inahitajika kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya nyumbani, yani kuwasha freezer, taa za vyumbani, tv na computer.
 
Achana na zi-jenerator ndogondogo zitachoma na kuunguza vifaa vyako. Jenereta nzuri kwa maana hiyo hazipatikani Tanzania. wachuuzi wetu wanaleta bidhaa duni kutokana na uwezo wetu wa kutonunua vifaa ghali na vyenye ubora.

Ungelikuwa na kama $2000 ningelikushauri utumie solar na inverter ya 5000watts ingelitosha kwa usalama wa vifaa vyako na kubana matumizi. Panel za solar zinadumu zaidi ya miaka ishirini na tano na betri hudumu si chini ya miaka mitano. hesabu za LUKU na MAFUTA YA GENERATOR sidhani kama zitakuwa na uwiano na za solar.

Matumizi ya generator ni makubwa mno kwani ikiwa inabana matumizi ya mafuta kama wanavyosema utatumia kwa uchache lita tano kwa masaa kumi na nane. Aidha, unaweza kujibana na kutumia lita 2-3 kwa siku kutokana na uchache wa vifaa utakavyotumia. lakini ukiongeza vifaa ndipo balaa la mafuta linapokuja!

Ila jitahidi upate jenereta za Honda au YANMAR 3500 zinaweza kukufaa. (kuwa makini katika kusoma majina -uchakachaji ni mwingi unaweza kukuta inasomwa KHONDA au YMYMAR)
 

Ni kweli umeme wa solar (Solar Energy Businesses in Tanzania). (Rex Investment Limited - Tanzania's leading solar energy contractor - Rex donates solar system to Kerege orphanage) ni bora kuliko jenereta ya laki 4.

Tatizo ni ku raise io hela (2.5m-3m). Kwa wengine sio rahisi, pale wanapoamua na kuwa na uhakika wa kupata hizo hela.

Jenereta ni nzuri na itakusaidia kwa wakati wa emmergency, hasa kama ukiiwasha kwa 3 au 4 tu. kwa siku.
 
Je, vipi substitute ya inverter? Nimeambiwa kuna za mpaka laki 2 kisha nikaongezea laki 1.2 ya betri, ni kweli?
Zinadumu na chaji kwa muda siku ngapi? Durability yake ikoje? wapi nitapata nzuri? Tusaidiane tu jaman kukabiliana na huu mgao wa Giza-nesco!!
 

Inventer nazo sio mbaya, hata zile za kutengeneza, ila kama ujuavyo, zinaweza kudumu na zinaweza kubuma.

Jirani hapa bunju b anatumia io, anachofanya ni kuichaji betri ya inventer mara 2 au 1 kwa wiki.

Umeme wake sio mkali ila kuondoa giza kwa kuwasha taa tu utaweza, na itategemea inakupa watts ngapi ili uweze hata kuwasha ka feni au tv.

Wapi utapata hapo kasheshe, maana mafundi wako kibao, na siku kuna kautapeli tapeli kwenye swala hilo, ndio, kama mafundi seremala, utazungushwa na kupigwa tarehe, mpaka uipate ujue na urafiki na hata hamu ya io inventer itakuisha!

Uliza uliza kwa ndugu na marafiki, za dukani sina uhakika kwa hela yako.

Durability, hakuna guarantee mkuu, swala ni kwenda na reputation ya huyo fundi.
 

Ahsante sana mkuu, ukweli umejitahidi kuelezea na nimekupata vizuri,Ila ukweli pia umezidi kunichanganya sana. Maana hata naogopa tena kwenda kununua.Kwa maelezo yako zinahitaji imani zaidi kuliko uhalisia wake.Yaani ukimbiwa ni ya watt 500 inabidi uamin tu.
 
Kaulizieni Tanesco maana wanawakatia umeme ili wakubwa wauze majenereta. Kwahiyo watakuwa na data za kutosha sababu wana wataalam pia.
 
Naomba mnaotumia generators mtufunze ni capacity gani inahitajika kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya nyumbani, yani kuwasha freezer, taa za vyumbani, tv na computer.

Hapo umenena mkuu, ni muhimu wataalamu watufahamishe capacity gani inatosha kwa mfano wa vitu nilivyosema?
 
Habari zenu wana jamii,

Nina kashamba kangu maeneo ya rufiji lakini kuna shida sana ya maji hivyo kulima bustani na ufugaji imekuwa ngumu, nilifanya utafiti wa ili nichimbe kisima ikaonekana maji yanaweza kupatikana mita 100 kwenda chini, lakwanza ningeomba mtu yoyote anayefahamu makampuni yanayochimba visima kwa gharama nafuu lakini kazi ya uhakika.

Swala la pili ningeomba mwenye kufahamu sehemu nitakapoweza kupata generator za kv 6 mpaka 10 mpya na zilizotumika kwa bei nafuu.

Tatu ningeomba kufahamishwa kati ya simtank, polytank na kiboko lipi bora zaidi, na wapi nitawaza kupata rank la lit 3000 na 5000 kwa bei poa?

Naombeni msaada wenu.
 
Tatu ningeomba kufahamishwa kati ya simtank, polytank na kiboko lipi bora zaidi, na wapi nitawaza kupata rank la lit 3000 na 5000 kwa bei poa?..

Naombeni msaada wenu.

Kwa uimara ni Simtank, likifuatiwa na Kiboko.
 
Mkuu, nakushauri ujenge elevated concrete water tank (storage/reservoir tank). Hii itakusaidia kujaza maji bila kutumia pump na maji yatatiririka kwenye bomba bila kutumia pump. Pia, hili ni durable kuliko Polytank kama Simtank, na pia haliwezi kuibiwa.
 
Asante kwa ushauri wako. Je, unaweza kuwafahamu watu ambao wataweza kunijengea hilo tank?
 
U can visit me physically for a free consultation. We are available at Nkrumah Street, next to Total Petroleum HQ. Company name SNTECH.
 
u can visit me physically for a free consultation. We are available at Nkrumah street, next to Total Petroleum HQ. Company name SNTECH

Popobaawa! Dah

Back to the main topic, Simtank imetulia zaidi lkn bei yake pia iko juu ukilinganisha na nyingine.
 
Okay nitakutafuta wiki hii, mida ya mchana, but sidhani kama nikifika hapo nikiuliza jina la popobawa utapatikana. Je, unaweza kunipa mawasiliano yako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…