Jenereta: Fahamu Aina, Matumizi Sahihi, Matengenezo na Namna ya Utunzaji wake

Jenereta: Fahamu Aina, Matumizi Sahihi, Matengenezo na Namna ya Utunzaji wake

Kuhusu wachimbaji na gharama (baada ya ku servey) ni pm tuwasiliane.
 
Kwa Jenereta waone Plustronic nafikiri wana website, ebu wa google. Wana Generators za uhakika.
 
LAT hiyo elevated concrete storage inaingizaje maji bila kutumia pump? Shule plse.
 
Nashukuru kwa msaada wenu na bado nahitaji msaada wenu wa mawazo, Nimeangalia kampuni ya plustronic lakini sijaona generator ndogo za KV 6 naona zimeanzia zaidi ya KV 10 na kuendelea je kuna kampuni nyingine? Na vipi generator za kampuni ya boss?
 
Habari za kazi wakuu,

Samahanini naomba msaada wenu kufahamu ni aina nzuri za majenereta yenye ubora unaokidhi kuzalisha umeme wa kawaida tu na bei zake, ulaji wake wa mafuta n.k

NB: Nahitaji yale #madogo tu yenye nguvu ITAKAYOFAA KUZALISHA UMEME KWA AJILI YA ROOM MOJA TU KWA MATUMIZI YA KAWAIDA KAMA MWANGA USIKU, Radio, KUCHAJIA SIMU na LAPTOP nitakapokua kijijini nafanya kazi kwa kipindi hichi.

Natanguliza shukrani zangu kwenu.

Ahsanteni.
 
Kama matumizi yako kidogo hivyo kwanini usitafute solar?

Nlkua na wazo hiloo mkuu ila nmekua naskia kwamba umeme wa solar sio mzuri kwani unaharibu sana Mabetri ya Laptop, Simu n.k mkuu.

Nami hivyo ndio vitendea kazi vyangu sasa sijui hilo lipo vipi naomba kuelweshwaa zaidi.
 
Nlkua na wazo hiloo mkuu ila nmekua naskia kwamba umeme wa solar sio mzuri kwani unaharibu sana Mabetri ya Laptop, Simu n.k mkuu
Nami hivyo ndio vitendea kazi vyangu sasa sijui hilo lipo vipi naomba kuelweshwaa zaidi...
Bora umeme wa Solar upo Stable, wa Generato ni majanga.

Nunue Solar halafu nunua stabilizer au Ups kwa Laptop au computer ya kawaida. Generator ni ghali sana kulimagane kwa matumizi unayotaka wewe.

Muda mfupi tu unaweza kukuta umetumia mafuta ya kujenga nyumba kama unayoishi.Nilikuwa nayo kipindi umeme Zanzibar ulipokuwa hakuna nakumbuka balaa lake.hasa tupu.Halafu Hatari nje nje kwa Petrol.

Pia hakuna Generator dogo lenye uhakika wa ubora, nyingi zinaanzia zile kubwa za kuanzia laki saba au milioni moja na nusu hadi mbili. Hivi vi Tigers vya Mchina vitakuripukia siku yoyote.

Kama unataka ktupa pesa na kuukaribisha umaskini basi nunua Generator uone.
 
Inakuwaje wakuu,

Naombeni Mawazo kwenye hili nataka kununua Jenereta kale kadogo kabisa mana umeme umekuwa kizungumkuti sana..Vitu ninavyotaka Kurun nin Laptop Tv na Redio ya Kawaida sasa sijui hizi generator zikoje kuna mtu nilimuliza akananiambia kuna generator ya laki na Hamsin kadogo kabisa ila nataka kujua kama ipo kweli pia vip kuhusu comfigarition inahitaji vitu kama stabilizer?

Pia connection yake ni lazima ipitie kwenye main switch tu maana niko nyumba ya kupanga sasa nikiunga kwenye main switch matumizi yatakuwa makubwa sana mim ntashindwa kupata kile nataka kwa mda sahihi.

Nawasilisha
 
Anza kutafuta madalali mapemaaaa! Nani akuvumilie na kelele zako hapa uwani!
Kama vipi ununuwe la kututosha wote.

Hahahaha kama Unanunua Futa Haina Shida Mkuu wew tu na pesa yako tunatumia kabisa
 
Mkuu Calculate total power ya vifaa vyako baada ya hapo utajua size ya generate litakalokidhi needs zako Generator iko rated ktk apparent power kVA lakini pia unaweza kulifunga automatic kama ni electric start utaunga supply inayoingia kwako tu itakubidi ufunge kwa contactor kwa ajili ya kuruhusu supply ya tanesco kujirudi auto yani mfano umeme umekata ukiwasha generator ,umeme wa tanesco hata urudi hautafikia load yako mpaka ukizima generator apo apo unafikia load zako.
 
Nunua ups au sijui niite power bank, ndo habari ya mjini siku izi. Achana na hayo makelele.
 
Habari Wadau,

Nilikuwa nina ofisi yangu sasa kutoka na kero ya umeme nataka kununua jenereta sasa sina uzoefu na majenereta kiujumla nilikuwa naomba msaada kwa wazoefu wa majenereta je ni aina gani nzuri ya jenereta naweza kununua kwaajil ya mahitaji ya ofisi yangu?

NB: Ofisi yangu ina laptop 2, printer moja pamoja na water dispenser.
 
Hata mi nmewaza kununua walau la kuwasha tu feni moja ya chumbani, tanesco ni kero mnooo.Umeme ukikatika Nyumba inak a tanuru.
 
Tafuta jenerata ya Japan, eg Honda; jitahidi kukwepa Mchina hata kama anavutia kiasi gani kwa sura.
 
Back
Top Bottom