Jenga na tofali za kisasa za mwamba! Zisizo na gharama ya plasta kwa nje

Habari za leo ndugu zangu?

Nauza tofali za Mwamba tofali ngumu mara 5 ya tofali za block!
ukijenga nazo usitegemee nyumba itapata crack au msuko suko wowote!

Tofali hizi ni ngumu kiasi ambacho wakati wa kupakiwa zinarushwa tu kwenye gari na wakati wa kushusha unabinua tu tipa. Uwezekano wa kukufikia popote ulipo upo, kwa mikoani tunatumia semi trela zinazoleta mahindi mpaka wa Kenya Holili.

Semi inaweza kubeba tofali 1200 kwa tofali hizi ndefu na 1360 kwa tofali fupi, ambazo idadi hiyo ya tofali inaweza kujenga vyumba hadi vitano kulingana n ramani ya nyumba yako.

Tofali hizi zimechongwa vizuri zina mwonekano mzuri hazina mashimo mashimo zimechongwa kwa mashine hivyo kama utapenda kwa nje ya nyumba unaweza usipige plasta na ukaishi vizuri tu ukaenda na fashion!

Bei yake sasa,
Tofali zote inch 5&6 ni 1050 zenye urefu wa inch 18 na 1000 zenye urefu wa inch 16.

Kwa wanaojenga Moshi hadi zifike site ni 1300, kwa wilaya za Same, Korogwe, Tanga Mjini, na Dar tofali zinakuja kwa bei rafiki kwakuwa kuna masemi mengi yanayokuja kupakia simenti maeneo ya Tanga.

Faida za ziada
  • No crack.
  • Tofali zetu ni imara sana.
  • Haziliwi na magadi.
  • Unaweza usipige plasta na ukaenjoy kuishi hapo.
  • Ukizijenga hazitumii sementi nyingi.
  • Unanzia msingi hadi kwenye lenta hakuna gharama za mawe ya msingi.
 
kwa Arusha ni bei ngapi
 
kuna Jamaa aliuziwa Miti ya Mpingo akaambiwa ni Imara sana sana hasa kadri inavyokauka ndo inazidi kuwa Imara

alisahau kuwa Mlango utahitaji upigwe Msumali, uchongwe urekebishwe n.k ili iweze kufit …

ubora wa mbao upo pia kwny udhaifu wake kwa kuwa kuna siku utahitaji kuuvunja, kuutoboa n.k
 
untoboa tu bila shida.
 
Tabora zinafika kwa bei gani?
 
Unaposema ni imara sana una maanishA nini? Ulishawahi kuzipima kwenye maabara yeyote ya ujenzi ukajua uimara wake? Kama ushawahi pima unaweza weka ripoti ya maabara ili tuuone huo "uimara sana"?
 
Unaposema ni imara sana una maanishA nini? Ulishawahi kuzipima kwenye maabara yeyote ya ujenzi ukajua uimara wake? Kama ushawahi pima unaweza weka ripoti ya maabara ili tuuone huo "uimara sana"?
ndio zina richerscale ya 12 yaaani mgandamizo wa 12 na ukitaka ujue hizi tofali ni imara zikija tipa linabinua kama unavyobinua mawe na hazikatik wala kuvunjika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…