Jengo jipya la ubalozi DC - Dola milioni 10?

Jengo jipya la ubalozi DC - Dola milioni 10?

You are missing the boat completely again. Is this your specialty?

Sikusema chochote kuhusu unapoishi, wala kwamba huijui hiyo embassy, for all I know you could be the ambassador himself.

Ninachosema ni kwamba, umei approach issue in a very narrow minded way, na mazungumzo yetu hapa yalikuwa mapana sana.Hukuifanyia justice thread, umeonekana kama mtu aliyekurupuka tu bila kusoma wala kufanya research yoyote, ukapost tu "ununuzi wa jengo kitu muhimu, wanaobisha wanaboronga"

Is this the best you can do?

Hebu mwenyewe tazama hiyo sentensi halafu angalia mtiririko wa arguments, watu wana discuss mambo mengi zaidi ya ununuzi wa jengo. Tanzania ni sovereign nation ambayo haishindwi kununua jengo la dola milioni kumi, lakini kuna mambo mengine lukuki tumejadili.

Naomba kabla ya kuchangia jaribu kujielimisha kuhusu topic kidogo ili usije uka ji expose na post shallow kama "Ununuzi wa jengo muhimu, wanaopinga wanaboronga"

Nani anaboronga sasa?

Mkuu una-complicate maisha bure. Kabla ya kuchangia nimesoma posti zote. Na mpaka Jasusi kutoa points zake, ujue kuna kitu cha kuweka sawa.

Mpaka sasa posti nyingi zinachangia kuhusu idadi ya ghorofa wakati idadi ya ghorofa sio determinant ya maana katika ununuzi wa property.

Kuna nyumba sio za ghorofa lakini zina bei mbaya kuliko nyumba za ghorofa kumi.

Watu wanaleta mentality ya bongo kuwa nyumba nzuri ni lazima iwe ya ghorofa na idadi ya ghorofa inaongeza thamani ya nyumba. Hivyo mjadala mzima umekaa kwenye 10 millioni zilizotumika kununua nyumba ya ghorofa 6 na kuna wanaofikiri kuwa nyumba ya ghorofa 3 itakuwa na discount ya milioni 5.

Na kama una sababu nyingine ya maana ya kupinga na nikasema unaboronga naomba samahani, chonde mkuu.
 
Mkuu wangu hatuhitaji kubishana nchi hii ni ya mtandao nipe agent, broker anayeweza kufanya hivyo kisheria.
Trust me, huwezi kwenda benki na bag la fedha millioni ati nimeuza nyumba..acha millioni elfu 20 tu cash utaitiwa Polisi palepale.

Mkandara hiyo kwa mtu binafsi au muuza unga. Lakini kwa serikali unakamatisha mshiko wote.
 
hivi huyo balozi ana akili timamu kweli?...huwezi kuomba fedha ya kununulia jengo bovu wakati mahitaji huna!...hu ni ufisadi wa balozi mwenyewe thats it!
 
hivi huyo balozi ana akili timamu kweli?...huwezi kuomba fedha ya kununulia jengo bovu wakati mahitaji huna!...hu ni ufisadi wa balozi mwenyewe thats it!

Afu nyie mnaosema kuwa balozi hana akili, mnaendesha HUMMERS wakati pesa ya gasoline taabu kupata.
 
jengo la bilion 10 kwa nchi kama tz ambayo majority ya wapiga kura wanaishi chini ya dola moja kwa siku.ama kweli priorities

Huenda ndo litaleta maisha bora kwa kila mtanzani kama si kuzalisha mafisadi zaidi ya hawa tulio nao.
Lakini kwa upande wa pili kama kutakuwa na mkakati mzuri wa kukusanya kodi na kuwafikia wa Tanzania kama fedha za kigeni litakuwa na umuhimu zaidi kuliko pengine hata migodo yetu ya dhahabu na maliasili tulizo nazo maana fedha za kigeni zinazo patikana huko sidhani kama mpiga kura kule kijiji kwangu huwa azionja hata harufu yake.
 
Kwa maana nyingine kama ubalozi ulitaka ofisi yenye vyoo 4 sio busara ikanunua ofisi yenye vyoo 5. Kwa maana nyingine ubalozi ulitakiwa kumweleza muuzaji kwamba iuziwe gorofa 3 tu kati ya sita na hivyo muuzaji atafute mnunuzi wa gorofa zilizobaki?



Haya ni mawazo ya kibongo-bongo, bora hata ubalozi wetu DC hawakuwa na mawazo haya. Ofisi katika nchi zilizoendelea sio kama soko au sehemu ambapo kila mtu anatandika gunia na kuuza nyanya zake. Na Usalama katika ofisi katika nchi za wenzetu unadumishwa kwa kuwa na controlled access za ofisi. Hivyo basi si kwamba kila atakayeingia kwenye jengo hilo atakuwa na access ya ofisi nyingine za kibihashara na wala haina maana kwamba maofisa wa kibalozi wataonana kila siku na watu wa ofisi nyingine.



Haya pia ni mawazo mgando. Yani jengo moja tayari tunapiga kelele za wasiwasi wa property management, kana kwamba ili ni jengo la kwanza kwa Tz kulinunua. Balozi zetu kadhaa zina residents, nani ana manage? Nani anazifanyia ukarabati? Ngapi zimeharibika kwa kukosa property managers?

Tupo mbaaaaaaaaaali sana kimawazo kuliko wenzetu walioendelea.
kama unaakili utaelewa point yangu kwamba ikiwa mahitaji yako ni 3 floors then unaingia ubia na nchi nyingine kama EU walivyo fanya Tanzania, lakini kama akili zako ni hizo utasema kama ulivyo sema.
kuhusu property management , ulizia wizara ya nje , nyumba zetu za uingereza zikoje? kama hutaambiwa ukurafati unaotakiwa ni sawa na kununua nyumba zingine. au kama una rafiki au ndugu uingereza muulizie hizo nyumba zikoje, lakini kama una akili za ushasbiki tu utaendelea na hoja yako.
Ukija kuhusu investment katika property na suala la upangishaji ujue pia unatakiwa uwe na utaalamu huo, sio mambo ya Bongo unampimia mtu kwanza au mpaka dalali apige mahesabu yake.
Sasa unataka kusema hapo DC tutapeleka mtu wa namna hiyo au huyo afisa tawala ana uwezo huo?
Halafu bei tumepewa kiujumla jula tu kwamba bei zina range $400-900 bila kuambia je hilo jengo liko katika hali gani? pia bei za sasa baada ya economic down turn ndio iliyo competitive au?
Pia kuna issue ya maintenance, kama ufagizi, marekebisho madogo madogo etc, je tuna mtu anaye faaa kumanage hatua hizo au ndio tutampeleka kisa tuna jengo kubwaaaa hapo Washington ambalo wenyewe tunaona ni investment kubwa kwa nchi yetu kujisifia na ku-justify kumpeleka mtu huko mwwenye uelewa wa property management. maana mahesabu ya majengo sio sawa na haya mengine ya afisa utawala kuyajua. kuna mambo ya kugwa vyumba etc, square feets etc etc.
Lakini kwa akili zako sijui za wapi unaona ni kila mtu anaweza kufanya hiyo kazi, basi tufute vyuo vyetu vikuu na specialization.
Ndio maana nasema serikali yetu including u, kama ni mwerevu au una akili tanzania housing agency wangeanza na kuinvest kwenye hizo nyumba chakavu O'bay kwa kujenga nyumba mpya na kupangisha iwe kwa waziri au watu wa nje kwani hiyo government agency inao hao wataalamu , na ingekuwa cost effective kumanage hizo nyumba badala ya kuzungumzia jengo moja, kisa lipo Washington DC.
 
Wakuu zangu,
naona bado mnajadili swalai la ununuzi wa jumba hilo la Ubalozi..
Kwanza kabisa navyofahamu mimi Marekani na nchi zote zilizobobea Uibepari, huwezi kununua nyumba kwa cash money yaani ulipe zote billioni 10 kwa sababu uuzaji wa nyumba hutegema interest inayokusanywa kwa kila mwezi na mara zote transaction ni lazima zipitie financial institution kisheria kutokana na michezo ya money laundry, hakuna exceptional wala untouchables ktk sheria za wenzetu..kumbukeni tu wenzetu wana system nzima inayo monitor mabadilishano ya fedha kati ya muuzaji na mnunuzi. .

Mkuu wangu wa miaka nenda rudi hapa, naomba nikusahihishe na kutofautiana na wewe.

Muuzaji wa nyumba anaweza kuwa private buyer; huyu hana hofu ya money laundary ili mradi tu fedha zinakuwa transfered from one bank to another. Bank ndio inayo control money laundary na sio vinginevyo; muuzaji ataogopa tu kupokea fedha endapo mnunuzi ana CASH MKONONI badala ya kuwa na fedha kwenye benki yake. Fedha halali ni ile inayokuwa transfered from one bank to another.

Serikali ya Tz ina account yake ya nje ambayo ina fedha halali zinazoweza kuwa transfered kwenye bank ya muuzaji jengo. Bank ya muuzaji wa jengo nitahakikisha inapokea fedha halali na kuzihamishia kwenye account ya muuzaji.

Mkuu sio kweli, na narudia kwamba sio kweli kwamba ukiwa na cash kwenye account yako ambayo umezipata kwa halali huwezi kununua nyumba. Hapa mkuu wangu umeteleza, na kubali yaishe. Vinginevyo kusingekuwa na international transaction, na wala kesi za EPA zisingekuwapo.

Nihitimishe kwa mfano; yupo rafiki yangu ambaye alikuwa na ela yote ya kununua nyumba, ela hii alipewa urithi na mzazi wake. Alipotaka kununua nyumba "wajanja" wa benk wakamwambia kwamba akope ela benki na ela zake za urith awekeze sehemu nyingine; rafiki yangu akawakomalia akisema hapendi kukopa na hapa tunaposema kanunua nyumba kwa ela yake na si yakukopa.

Benki za nchi zilizoendelea ni wajanja, hawataki mtu mwenye fedha badala yake wanataka mtu hasiyenazo ili wamkamue. Watakuambia kwamba tunza ela zako na tumia za kwetu, ukifanya hivyo ni kosa. Lakini ukiwa mjanja unawaambia kwamba hutaki kutumia ela ya benk wakati unazakwako.

All in all, mtu mwenye fedha halali katika account yake (sio mkononi) anaweza kununua nyumba, na uhalali wa fedha hizo ndio utakaofanya ziwe transfered from one bank to another na hivyo kuhitimisha ununuzi wa nyumba. Ila wajinga ndio waliwao; benk ikiwashauri wakope badala ya kutumia ela zao wanazani ni SHERIA.
 
Waungwana,

Haya mambo ya Serikali kutaka kujihusisha na mambo ya kibiashara ya kukodisha baadhi ya sehemu ya jengo la ubalozi mimi siafikiani nayo hata kidogo. Kama mnavyojua mara nyingi balozi zetu zinachelewa sana kupata mishahara yao kutokana na sababu mbali mbali ambazo nyingi ziko ndani ya uwezo wa Serikali. Pia hakutakuwa na uangalizi wa kutosha wa pesa zitakazopatikana kutokana na mapato ya ukodishaji wa sehemu ya jengo la ubalozi huo. Asilimia kubwa zitaishia kwenye ufujaji wa kifisadi na hazina yetu si ajabu haitaona hata senti moja kutokana na mapato hayo ya pango.

Wengi tunaofuatilia ripoti za CAG kuhusiana na matumizi ya kienyeji katika balozi zetu tunalijua hilo la ufujaji wa pesa ambazo balozi hazikuwa na authorization toka hazina katika matumizi ya pesa hizo mfano ni kesi inayoendelea sasa hivi ya aliyekuwa balozi Italy. Pia fees za kuomba visa kwa wale wanaotakiwa kuingia Tanzania zimeshatafunwa katika baadhi ya balozi zetu na hata senti moja haikufikishwa hazina.

Hili pia alilolileta mwenzetu Bluray la usalama wa ubalozi wetu nalo ni la kuliangalia kwa kina. Je, kutakuwa na maofisa katika balozi ili kuhakikisha tathmini ya kutosha inafanywa dhidi ya hao wapangaji ili kuhakikisha ni watu salama na siyo magaidi ndiyo wanapangishwa? Je, kutakuwa na tathmini ya kuhakikisha hao wapangaji wana financial ability to pay their monthly/annual rent? Na kama wanafanya biashara je zitakuwa ni biashara halali? Tusije kukuta tunakodisha jengo kumbe hiyo sehemu inafanywa kama danguro au jamaa ni wazungu wa unga au ni magaidi. Likitokea hili la kuwapangisha watu ambao hawakustahili kupangishwa ni aibu kubwa siyo tu kwa ubalozi bali kwa Serikali yote.

Serikali ilishasema haitajihusisha na mambo ya kibiashara, hili la tamaa ya fisi ya kutaka kutajirika kwa kujenga/kununua ofisi kubwa ya ubalozi na kukodisha sehemu ambayo haitahitajika ni lazima tu litakuwa na utata na pia ufisadi hautakosekana. Hizo bilioni 10 zinaweza kuelekezwa kwingine ambako zitakuwa na manufaa zaidi badala ya kutaka kujiingiza kwenye biashara bila ya kuwa na utaalamu wa mambo ya biashara.

Leo tunataka kununua jengo la ubalozi DC kwa sababu tumesikia kwamba kupangisha nyumba DC kunalipa, kesho balozi wetu pale London (UK) naye atasema kwamba biashara ya taxi pale London inalipa hivyo basi Serikali iwekeze katika biashara ya taxi pale London, where do we draw the line when it comes to this issue of our govt "doing business" in foreign countries!?
 
Last edited:
mambo ya ghorofa sita na tatu.
ukweli ni kwamba ubalozi umenunua mara mbili ya office space zaidi ya mahitaji yao.
kwa nini wasinunue office space ya mahitaji yao.
 
mambo ya ghorofa sita na tatu.
ukweli ni kwamba ubalozi umenunua mara mbili ya office space zaidi ya mahitaji yao.
kwa nini wasinunue office space ya mahitaji yao.

I like that argument mkuu. Big up!
 
MgonjwaUkimwi,
Mkuu nimekusikia sana na hakika ulosema ni kweli tupu hasa ktk transaction za biashara..Nadhani hapa tunazungumzia ununuzi wa nyumba au sio!. Hayo ya EPA na biashara hayahusiani na maelezo yangu hata kidogo.

Sasa nipe mfano ktk hilo ambao wewe unafikiria Tanzania wamefanya ktk ununuzi wa hiyo nyumba! maanake hata kama serikali yetu ina account Marekani nina hakika kabisa benki (hasa Marekani) haziwezi kukubali kuwa kati ya mjadala wa ununuzi wa nyumba bila wao kuingiza kitu kidogo...yaani sionmi ndani kabisa unaposema wao wajanja wakati kuvta interest ndio mfumo wa biashara zote za Bank isipokuwa huko Arabuni.

Mkuu wangu huyo rafiki yako ambaye unamjua wewe sielewi kaweza vipi kuwakomalia Bank yake akaweza kufanikisha. Mimi sii mara moja wala mbili, kuna watu wangu wa karibu wamenunua nyumba zao New York kwa kupitia bank hizo hizo wamekataliwa. Tumefanya kila mbinu iwezekanayo na nafuu tuliyoipata ni mortgage ya miaka 5 pamoja na kwamba cash ilikuwepo kulipa thamani yote. Tumewaona toka meneja wa branch hadi makao makuu wenyewe wanapaita shimoni imeshindikana kwa sababu bank zinaishi kwa service charge na interest ambazo tayari zina vifungu vyake kiasilimia kulingana na muda. Walishindwa kutusaidia tukatukana matusi yote lakini ndio Utaratibu ambao hauwezi kuvunjwa na mtu yeyote.
Hiyo ndio experience yangu hivyo pengine yawezekana Tz tumenunua jengo hilo cash sijui kwa misingi ipi kwani kuna kodi za umilikaji ardhi na jengo ambazo zina taratibu zake, makaratasi kibao ya kuweka sahihi...kama kweli utaweza kununua nyumba ya millioni 10 cashed basi utalipa zaidi theruthi nzima ya thamani ya nyumba hiyo kwa wakati mmoja..Jambo ambalo sii akili!
 
Jasusi,

Of all people you should know better kwamba, economics aside, sababu za kiusalama tu haziruhusu kufanya jengo la ubalozi wetu liwe na ofisi za kibiashara juu yake.


In order to justify their lopsided deal,these thieves start talking about renting the extra office space that they will not use. Can someone tell me where in the world respectable embassies share their buildings with other tenants for commercial purposes? Msitufanye wajinga; mmezoea kula bila kunawa!!
 
MgonjwaUkimwi,
Mkuu nimekusikia sana na hakika ulosema ni kweli tupu hasa ktk transaction za biashara..Nadhani hapa tunazungumzia ununuzi wa nyumba au sio!. Hayo ya EPA na biashara hayahusiani na maelezo yangu hata kidogo.

Sasa nipe mfano ktk hilo ambao wewe unafikiria Tanzania wamefanya ktk ununuzi wa hiyo nyumba! maanake hata kama serikali yetu ina account Marekani nina hakika kabisa benki (hasa Marekani) haziwezi kukubali kuwa kati ya mjadala wa ununuzi wa nyumba bila wao kuingiza kitu kidogo...yaani sionmi ndani kabisa unaposema wao wajanja wakati kuvta interest ndio mfumo wa biashara zote za Bank isipokuwa huko Arabuni.

Mkuu,
Fedha halali haikataliki hata siku moja. Hakuna nchi inayokataa fedha halali. Hakuna benki inayokataa fedha halali. Hakuna financial institution duniani inayokataa fedha halali. Hakuna muuzaji anayekataa fedha halali.

Tatizo la uchumi wa nchi zilizoendelea kama Canada na Marekani ni kwamba information nyingi ambazo zinaweza kuwafikia wanunuzi au watu wakawaida ambazo zinaweza kuchangia kuzorota kwa shughuli za uchumi zinafichwa kwa makusudi na wajanja wachache wenye information hizi wanazitumia kwa faida yao. Nafafanua.

Benki ni bihashara inayotengeneza faida kwa KUKOPESHA (miongoni mwa shughuli nyingine). Kwa mantiki hii wakopaji wakiwa wengi benki zinafurahia. Kwa mantiki hii mteja mwenye fedha tasilimu kwenye account yake na hasiyehitaji kukopa HALETI FAIDA KWA BENKI inayotunza fedha zake. Wakati huo huo wachumi wa serikali ya nchi husika wanafurahia kuona watu wanachukuwa mikopo kutoka katika benki kwa sababu kufanya hivyo kunachochea shughuli za uchumi. Kwa mantiki hii, kadri watu wanavyochukuwa mikopo ndipo benki na serikali inavyofurahia. Kwa hiyo kumekuwa na jitihada za makusudi za mabenki ku discourage watu wachache wenye fedha tasilimu za kununua nyumba (kwa mfano) zikiwashawishi wakope (mortgage) kwa kisingizio kwamba watu watapata faida kwa kuwekeza fedha zao mahala pengine badala ya kuzitumia kununua nyumba (opportunity cost). Ushawishi huu SIO SHERIA bali ni ujanja wa benki kujiongezea assets (mikopo). Na kwa kukosa information watu kadhaa wenye fedha halali za kununua nyumba wanauingia mkenge kila siku ya muumba.

Mimi sio mmoja wa walioshiriki katika kukamilisha ununuzi wa jengo DC lakini nitakupa mfano wa jinsi Tz inavyoweza kununua na foreign assets abroad kwa kutumia fedha zake tasilimu. Mfano huu pia una apply kwa mtu wakawaida aliye na fedha zake halali kwenye account yake.

Muuzaji wa jengo anaweza kuwa ni mtu mwenye account yake katika bank of America; muuzaji huyu yaweza kuwa nimfanya bihashara tu wakawaida. Ubalozi unapotaka kununua jengo utapatana na muuzaji huyu juu ya bei na kuridhiana. Muuzaji atataka ahakikishiwe jinsi atakavyozipata ngawila zake, na ubalozi utamuhakikishia kwamba atazipata fedha tasilimu. Pande zote zitawashirikisha wanasheria na wengineo for administrative tasks. Bihashara INAISHIA HAPO. Kitakachoendelea hapo ni bank to bank transcation; yani fedha tasilimu na halali zitatoka BoT katika kitengo cha EPA na zitaingizwa kwenye bank of America kwenye account ya muuza jengo.

Mkandara, cha muhimu hapa ni kwamba MUUZAJI WA JENGO HAJALI PESA ZINATOKA WAPI. Benki yake itahakikisha kwamba imepokea fedha halali kutoka katika benki ya mnunuzi (ubalozi). Sasa kwakuwa imekuwa kawaida kwa wanunuzi wa nyumba katika nchi zilizoendelea kukopa fedha kutoka kwenye benk (mortgage), benki zinaleta ujanja wa kushawishi watu wenye fedha zao tasilimu wachukuwe mortgage, na kwakuwa mortgage inakuza uchumi, serikali nayo imekaa pembeni ikishangilia kifaranga kinavyonyofolewa na mwewe.

Huyo ndugu unayemfahamu ambaye alikataliwa kununua nyumba kwa kutumia fedha halali tasilimu, nachelea kusema kwamba kuna jambo juu ya hizo fedha na si vinginevyo. Wapo watu wanaoshinda bahati nasibu na wanatumia fedha tasilimu kununua nyumba, magari, nk ili mradi tu manunuzi yanafanyika kwa kuhamisha fedha kutoka account moja hadi nyingine.

Fedha halali imetengenezwa ili INUNUE KILA KITU KINACHOUZIKA. Kisheria. Na unahaki ya kuishitaki serikali kama ela yako halali inashindwa kutumika katika manunuzi ya kitu chochote kinachouzika.
 
mkandara
mtu unaweza kununua nyumba cash, bank itakukatalia kama ikiwa na wasiwasi na pesa zako

wauzaji wengi wa nyumba wanapenda cash buyer hasa kwa kipindi hichi cha recession ambapo bank wanaweza kukukatalia mkopo.
ukiwa na cash agents wanakukimbilia na unakuwa na power ya kunegotiate
 
Chakujiuliza ni Je gharama yake kweli ni $ mil 10 tusutake kujifanya tumesahau yaliyotoke Italy.
 
Acha tuwe na jengo letu la ubalozi, mbona kila jitihada ya JK inapingwa hata kama ina manufa?
 
Its true, investment in construction pays alot and if the collected money land to faithful Tanzania who handle it, we will benefit . i just argue the concern personnels to keep in mind that what they are taking care of is not theirs but belongs to Tanzanians.
 
Acha tuwe na jengo letu la ubalozi, mbona kila jitihada ya JK inapingwa hata kama ina manufa?
Bw Magezi kwanza naomba usichukulie kwamba anacho fanya kikwete ndicho kinachopingwa, kwani hata cha nkapa kuuza nyumba za serikali kinapingwa kununua ubalozi italy kwa kuongeza cha juu kinapingwa na hata ofisi ya ubalozi uingereza kunaweza kuwa na madudu ingwa hayajaibuka nk nk.
Sasa tukirudi kwenye hili jambo, wewe ukiwa ni mtu mwenye akili ni lazima una mahitaji ya nyumba, sasa suala linakuja unataka nyumba ya choo kila chumba au yenye ya kawaida yenye choo kimoja, au ya kati yenye choo extra kwa master bedroom tu. Sasa uamuzi wako wa busara utatokana na uwezo wako wa kifedha na mambo mengine ya kimsingi kama eneo, usalama na shughuli unazotaka kufanya.
Sasa baada ya utangulizi huo tuje kwenye hili jambo, kwanza tunasikia tulikuwa na jengo la zamani, sasa sijui kwanini waliliuza na kununua hilo, aidha lilikuwa halitoshi , na pili jee tulio liuza tulipata fair price au huku tunaliwa na kule tunaliwa.
halafu linakuja hiyo busara ya kulinunua hili la sasa je ni wa busara, na je bei ni halali , na hiyo paper iliyo kwenda kwa waziri mpaka baraza la mawaziri mpaka kwenye budget inasemaje? maana najua utayarishaji wa budget mpaka inapopita na mpaka utekelezaji muda utakuwa umepita, sasa na hii economic recession bei kweli haijapungua, je mahitaji yetu ni ya hilo ghorofa nk nk.
 
Back
Top Bottom