MgonjwaUkimwi,
Mkuu nimekusikia sana na hakika ulosema ni kweli tupu hasa ktk transaction za biashara..Nadhani hapa tunazungumzia ununuzi wa nyumba au sio!. Hayo ya EPA na biashara hayahusiani na maelezo yangu hata kidogo.
Sasa nipe mfano ktk hilo ambao wewe unafikiria Tanzania wamefanya ktk ununuzi wa hiyo nyumba! maanake hata kama serikali yetu ina account Marekani nina hakika kabisa benki (hasa Marekani) haziwezi kukubali kuwa kati ya mjadala wa ununuzi wa nyumba bila wao kuingiza kitu kidogo...yaani sionmi ndani kabisa unaposema wao wajanja wakati kuvta interest ndio mfumo wa biashara zote za Bank isipokuwa huko Arabuni.
Mkuu,
Fedha halali haikataliki hata siku moja. Hakuna nchi inayokataa fedha halali. Hakuna benki inayokataa fedha halali. Hakuna financial institution duniani inayokataa fedha halali. Hakuna muuzaji anayekataa fedha halali.
Tatizo la uchumi wa nchi zilizoendelea kama Canada na Marekani ni kwamba information nyingi ambazo zinaweza kuwafikia wanunuzi au watu wakawaida ambazo zinaweza kuchangia kuzorota kwa shughuli za uchumi zinafichwa kwa makusudi na wajanja wachache wenye information hizi wanazitumia kwa faida yao. Nafafanua.
Benki ni bihashara inayotengeneza faida kwa KUKOPESHA (miongoni mwa shughuli nyingine). Kwa mantiki hii wakopaji wakiwa wengi benki zinafurahia. Kwa mantiki hii mteja mwenye fedha tasilimu kwenye account yake na hasiyehitaji kukopa HALETI FAIDA KWA BENKI inayotunza fedha zake. Wakati huo huo wachumi wa serikali ya nchi husika wanafurahia kuona watu wanachukuwa mikopo kutoka katika benki kwa sababu kufanya hivyo kunachochea shughuli za uchumi. Kwa mantiki hii, kadri watu wanavyochukuwa mikopo ndipo benki na serikali inavyofurahia. Kwa hiyo kumekuwa na jitihada za makusudi za mabenki ku discourage watu wachache wenye fedha tasilimu za kununua nyumba (kwa mfano) zikiwashawishi wakope (mortgage) kwa kisingizio kwamba watu watapata faida kwa kuwekeza fedha zao mahala pengine badala ya kuzitumia kununua nyumba (opportunity cost). Ushawishi huu SIO SHERIA bali ni ujanja wa benki kujiongezea assets (mikopo). Na kwa kukosa information watu kadhaa wenye fedha halali za kununua nyumba wanauingia mkenge kila siku ya muumba.
Mimi sio mmoja wa walioshiriki katika kukamilisha ununuzi wa jengo DC lakini nitakupa mfano wa jinsi Tz inavyoweza kununua na foreign assets abroad kwa kutumia fedha zake tasilimu. Mfano huu pia una apply kwa mtu wakawaida aliye na fedha zake halali kwenye account yake.
Muuzaji wa jengo anaweza kuwa ni mtu mwenye account yake katika bank of America; muuzaji huyu yaweza kuwa nimfanya bihashara tu wakawaida. Ubalozi unapotaka kununua jengo utapatana na muuzaji huyu juu ya bei na kuridhiana. Muuzaji atataka ahakikishiwe jinsi atakavyozipata ngawila zake, na ubalozi utamuhakikishia kwamba atazipata fedha tasilimu. Pande zote zitawashirikisha wanasheria na wengineo for administrative tasks. Bihashara INAISHIA HAPO. Kitakachoendelea hapo ni bank to bank transcation; yani fedha tasilimu na halali zitatoka BoT katika kitengo cha EPA na zitaingizwa kwenye bank of America kwenye account ya muuza jengo.
Mkandara, cha muhimu hapa ni kwamba MUUZAJI WA JENGO HAJALI PESA ZINATOKA WAPI. Benki yake itahakikisha kwamba imepokea fedha halali kutoka katika benki ya mnunuzi (ubalozi). Sasa kwakuwa imekuwa kawaida kwa wanunuzi wa nyumba katika nchi zilizoendelea kukopa fedha kutoka kwenye benk (mortgage), benki zinaleta ujanja wa kushawishi watu wenye fedha zao tasilimu wachukuwe mortgage, na kwakuwa mortgage inakuza uchumi, serikali nayo imekaa pembeni ikishangilia kifaranga kinavyonyofolewa na mwewe.
Huyo ndugu unayemfahamu ambaye alikataliwa kununua nyumba kwa kutumia fedha halali tasilimu, nachelea kusema kwamba kuna jambo juu ya hizo fedha na si vinginevyo. Wapo watu wanaoshinda bahati nasibu na wanatumia fedha tasilimu kununua nyumba, magari, nk ili mradi tu manunuzi yanafanyika kwa kuhamisha fedha kutoka account moja hadi nyingine.
Fedha halali imetengenezwa ili INUNUE KILA KITU KINACHOUZIKA. Kisheria. Na unahaki ya kuishitaki serikali kama ela yako halali inashindwa kutumika katika manunuzi ya kitu chochote kinachouzika.