Jengo la Kituo cha Polisi Oysterbay lawa gumzo Nigeria

Rais wa kwanza wa Botswana alikuwa rangi gani? Soma Geografia na historia yako ya darasa la tano vizuri unless ni kizazi kipya kilichopotea.

Sijaelewa bado unataka kusema nini!
 
Kituo cha polisi hata kiwe kizuri namna gani, usiombee kwenda ukiwa kama mhalifu. Bora hata ingekuwa shule.
Au na huyo msanii angepewa chumba chake hapo hata wiki 1!
Kituo kikiwa kizuri ndio watu hawateswi humo? Sifa za kijinga tu hizo
 
Tufafanulie pls na sisi wa huku Mbwinde,hicho kituo cha Polisi Oysterbay kiko mkoa gani...
 
Hawajui hawa siku wakipata kuona vya pembeni huko wata jua hii ndoo tz
 
Yaani kusifia kwenyewe ni kwamba kizuri kama vya KWAO?!!!! Wapuuzi nini, mi nilijua wanasifia kuwa hawajaona mfano wake. Na kwa maelezo haya inaonyesha kuwa wametudharau sana!
Umesoma vizuri hizo comments na kuzielewa?
 
Tunasifia kujengewa mpaka Kituo cha polisi na fisadi la kimataifa.
Kilijengwa bure?ilizungumzwa hapa kwamba kuna mwekezaji kachukua eneo lote la Obay polisi anavunja na kujenga Mall na vitu vingine.
Pia atawajengea Polisi kituo,ndo hicho?
 
Yaani kusifia kwenyewe ni kwamba kizuri kama vya KWAO?!!!! Wapuuzi nini, mi nilijua wanasifia kuwa hawajaona mfano wake. Na kwa maelezo haya inaonyesha kuwa wametudharau sana!
Unaongea nini?
Kwa hao mapopo kituo gani ukute kama hicho?
 
Enzi hizo nilipokuwa chuo nlivutiwa na kuleta suluhisho la mlundikano wa mahabusu katika kituo cha polisi mwananyamala, hivo project yangu ikawa kudesign hicho kituo cha polisi.

Ili kupata data zake ilinibidi kuzunguka tokea kituo cha mwananyamala,osterbay,wizara ya mambo ya ndani na hatimae ufundi.

Nilijifunza vitu vingi chini ya kamanda Mwaseba, na nikafahamishwa Aina mbali mbali za vituo (classes) lakini pia nikajionea walivyo jipanga katika mambo ya ujenzi wa vituo.

Kule Kuna consultation firm inayohusika na uchoraji(usanifu majengo nikiwalenga ma architect) pamoja na wahandisi wa kada zote.

Hitimisho. Licha ya mfadhili kutoa pesa credit pia apewe mchoraji wa jengo pamoja na wasimamizi.

Afande Mwaseba Ahsante sana kwa elimu ile kwani project ilikuwa poa sana nikatusua.
 
Tunasifia kujengewa mpaka Kituo cha polisi na fisadi la kimataifa.
Kilijengwa bure?ilizungumzwa hapa kwamba kuna mwekezaji kachukua eneo lote la Obay polisi anavunja na kujenga Mall na vitu vingine.
Pia atawajengea Polisi kituo,ndo hicho?
Amefisadi nini? Acha wivu tafuta pesa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…