Hizi nguvu mnazotumia kwenye mambo madogo kama haya munge elekeza kwenye mambo muhimu makubwa.
Hilo jengo la kawaida sana tatizo ni hizo ngazi au au urembo wa nguzo za kwenye baraza?
Wilaya nyingine ni za zamani sana, mahakama zake zilijengwa zamani hivyo huwezi kufananisha na wilaya mpya inayojengwa majengo au miundombinu ya kisasa.
Akili ya kawaida tu inatosha kutuambua hii sababu ya utofauti wa miundombinu mipya.
Mnataka mwaka 2015/2019 lijengwe jengo kama la mwaka 1961/1986?
Hata huku mitaani maeneo ya miji au makazi mapya huwa na majengo mazuri ya ramani na urembo wa kisasa.
Hii ndio shida ya kuwa na watu wako wa propaganda na kampeni wenye elimu ndogo kama akina mdude.
Sijawahi kuona ukosoaji wa kitoto namna hii enzi za ujana wa akina Mnyika, Halima Mdee, Zitto Kabwe n.k.
Na hao wote utaona elimu yao ni tofauti na akina Mdude. Kibaya zaidi hata wenye elimu ya juu wanaingia mkenge kuuunga juhudi za ukosoaji wa mambo madogo sana na kuacha makubwa ya msingi.