Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mahakama nyingi mpya zimejengwa...Kwani awamu hii wilaya mpya ni moja tu
Kutoka rohoni nikiwa rais kitu cha kwanza ni kuyabomoa yote ambayo yamefanyika kwa upendeleo!
Kata ninayoishi kuna kituo kidogo cha polisi, ni kizuri sana hadi mahabusu kuna tiles, mahabusu wa vituo vingine huwa wanaombwa wapelekwe kule bahati mbaya sana mahabusu ni ndogo haiwezi kuaccommodate watu wengiKali balaa ila mahakama hata iwe nzuri kiasi gani haivutii ni kama jeneza tu hata liwe zuri namna gan huwez kulitamani
Ww huwezi kuwa hata mjumbe wa mtaaKutoka rohoni nikiwa rais kitu cha kwanza ni kuyabomoa yote ambayo yamefanyika kwa upendeleo!
Nitapata "ngekewa" kama ya Jiwe!Ww huwezi kuwa hata mjumbe wa mtaa
Basi utafanya hayo hayo anayofanya Jiwe hv sasaNitapata "ngekewa" kama ya Jiwe!
Mhe.Rais mimi najua wewe sio mbunge wa Chato bali ni Rais wa nchi. Maana yangu ni kwamba linapofika suala la maendeleo simamia bila kupendelea.
Ukiangalia jengo hili jipya la Mahakama ya Wilaya ya Chato hivi ni wilaya gani nyingine yenye jengo la mahakama ya kisasa kama hili? Kama ni kwa nia njema ningetamani kuona majengo ya namna hii ya kisasa kwenye mahakama zote za wilaya nchi nzima lakini jengo hili nimeliona Chato tu anakotoka Rais.
Mdude Nyagali
#Sumu_ya_nyigu
#freedom_fighter
View attachment 1294907View attachment 1294907View attachment 1294907
Hizi nguvu mnazotumia kwenye mambo madogo kama haya munge elekeza kwenye mambo muhimu makubwa.
Hilo jengo la kawaida sana tatizo ni hizo ngazi au au urembo wa nguzo za kwenye baraza?
Wilaya nyingine ni za zamani sana, mahakama zake zilijengwa zamani hivyo huwezi kufananisha na wilaya mpya inayojengwa majengo au miundombinu ya kisasa.
Akili ya kawaida tu inatosha kutambua hii sababu ya utofauti wa miundombinu mipya.
Mnataka mwaka 2015/2019 lijengwe jengo kama la mwaka 1961/1986?
Hata huku mitaani maeneo ya miji au makazi mapya huwa na majengo mazuri ya ramani na urembo wa kisasa.
Hii ndio shida ya kuwa na watu wako wa propaganda na kampeni wenye elimu ndogo kama akina mdude.
Sijawahi kuona ukosoaji wa kitoto namna hii enzi za ujana wa akina Mnyika, Halima Mdee, Zitto Kabwe n.k.
Na hao wote utaona elimu yao ni tofauti na akina Mdude. Kibaya zaidi hata wenye elimu ya juu wanaingia mkenge kuuunga juhudi za ukosoaji wa mambo madogo sana na kuacha makubwa ya msingi.
Nyerere?????
Kwanini alifeli kuijenga Butiama
Mahakama ipo katika mpango wa kuboresha mahakama zake za wilaya.....
kaangalie mahakama ya Wilaya Kibaha nenda Mahakama mpya ya Ilala.....
na sehemu kadhaa tu....
Wewe si kawaida yako matusi.