Wewe umefuatilia majengo mangapi ya mahakama za wilaya mpya?
Au kwa sababu umeletewa moja la Chato basi unadhani umeona yote?
Kusanya picha ya majengo yote mapya yaliyojengwa na serikali wilaya mpya na za zamani, majengo yawe ya idara zote sio mahakama pekee kisha njoo uone hiki kitu nimeungumzia.
Mfano umeona Machinjio, Bus Stands mpya, Masoko na Hospital mpya zote nchi nzima?
Chato ni Wilaya mpya na changa sana hivyo majengo ya serikali ya hadhi ya kiwilaya mapya karibu yote. Tegemea kuona majengo ya kisasa.
Haiwezekani tuendelee kujenga majengo ya kizamani ili yafanane nchi nzima. Hata madaraja mapya nchi nzima mengi yana muundo na muonekano mzuri wa kisasa. Vifaa vya ujenzi tu vimebadilika kulingana na wakati na teknolojia.
Mfano sasa bati za Asbestos hazifai hazipo sokoni sababu ya sumu, Ceiling boards za kizamani hazitumiki kuna Gypsum boards, sakafu sasa hivi kuna tiles na mawe ya Tanga au tarazo bado ipo sokoni.
Mabomba ya maji ya chuma hayatumiki kusambazia maji majumbani kama zamani,... the list goes on.
Let's use common sense though "Common sense is not so common".