BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Wakuu, nimepita mara kadhaa pale kwenye jengo la TANESCO Ubungo Maji nikaishia kushangaa tu kwanini Mwendazake alikomaa sana lile jengo libomolewe na kile kilichoitwa kupisha ujenzi wa 'Flyover' iliyopewa jina la swahiba wake hayati 'Kijazio'.
Kimsingi ukipita pale utaona ni kiasi gani motive za siasa zilitumika katika kulivunja jengo la mbele la ofisi hizo. Kwa sababu licha jengo hilo kuwa karibu na barabara lakini halikuwa na madhara yoyote na hata lingeachwa lisingezuia ujenzi huo kwasababu bado kuna nafasi kubwa ya kutosha kupitisha barabara ya one-way pale na jengo likiwepo.
Kwa mtazamo wangu, Serikali iliingizwa kwenye gharama zisizo na msingi wowote kwenye ubomoaji wa lile jengo kwa maagizo ya mzee chato.