Jengo Maarufu Zanzibar kwa utalii, Beit Al Ajaib laporomoka

Samahani,naomba unielezee kidogo jinsi utumwa ulivyoanza wakati dunia inaanza
system ya kuwa
na watu wakawafanyia shughul imekuapo miaka na miaka.ni mfumo tu umekua unabadilika badilika.enzi na enzi kutumiana kuzalisha mali au kazi za nyumban imekuapo.kadiri maendeleo yalivozidi ikaonekana kuna haja ya kupanua wigo wa mahitaji mfano baada ya mahitaji ya rasilimal kuwa makubwa kwa nchi za ulaya makolon yakatafitiwa kwa safar nyingi tu za mabaharia kina vasco da gama na wengineo.

kwa mfano mfrance alipokuwa na mahitaj makubwa ya muwa akahitaji man power ya kutosha ndipo biashara ikachanganya ya kuuza watu, ilumtumikisha mtu eidha unamlipa au humlipi hujaanza leo.ni toka zamaan za kale kwel kweli.aliyefanya kafanya asiyefanya basi
 
Nilipita hapo mwaka jana pakiwa pamefungwa, nimeshaangaa hadi leo linabomoka walikuwa hawachukua hatua zozote za kuliendeleza na mkuu wao wa mkoa bwana hussein mwinyi yupo tu
 
Njama hizo hawataki majumba na miskiti ya kuonyesha waarabu wameamua kuacha ianguke lakini kanisa halitaachwa lianguke
 
Labda africa mashariki Omanis vs British..... Kumbuka wa mwanzo kuanza utumwa ni Mzungu wa kiportuguese. Oman ilitawaliwa na portuguese empire na wakafanikiwa kuwaondoa, ndipo wazanzibari wao wenyewe wakawaita wa Oman kuja kusaidia kuwaondoa wareno hao. Na kwa ridhaa yao wakakubali kutawaliwa na mwarabu wa Oman.

Mfalme wa Oman, amehamisha makao makuu yake na yeye mwenyewe kuhamia Zanzibar rasmi, na kama ulikuwa hujui basi tambua kuwa Zanzibar ndio ilikuwa mji mkuu wa nchi ilioitwa Oman. Mimi sijaona Mzungu/Mwingereza akisema kuwa Nairobi ni capital city of UK au mjerumani akisema Dodoma ni capital city of German. Ukitumia akili utaona kuwa mmoja alikuja kuongoza wananchi na mwengine alikuja kutumikisha wananchi wa eneo husika na kufaidisha kwao.

Katika link ulioileta, huyo mwandishi asema kuwa watu wanazungumzia kuhusu trans atlantic trade lakini kumbe waarabu walifanya kuliko ivo. Hivi nikuulize wewe mwenyewe, Waarabu walitawala nchi ngapi hapa Afrika hata aseme kuwa eti wao ndio wamekithiri kwenye hio biashara?
 
Kwanini umeuliza swali hilo?

Mbona zinafunguka na kutazamika
Labda kwako... Lakini kwa upande wangu mara nyingi zimekuwa zikinipeleka kwenye (tuseme) home page ya jf, tofauti na mwanzo ilikuwa ikinilink na videoder
 
Labda kwako... Lakini kwa upande wangu mara nyingi zimekuwa zikinipeleka kwenye (tuseme) home page ya jf, tofauti na mwanzo ilikuwa ikinilink na videoder
Sasa nimekuelewa Kiongozi.

Ahsante kwa ufafanuzi
 
Hilo jengo siyo John Walker - Whiskey: Getting stronger as days pass on.
 
Kuna habari kuwa kumetokea tetemeko la ardhi kule Zanzibar na kusababisha mtikisiko mkubwa na sintofahamu ya wakazi wa eneo, tetemeko hilo.

Inasemekana limeidungua jumba kubwa la kihistoria katika viwanja vya Forozani.

Sina uhakika na habari hizi nimeona picha zilizozagaa mitandaoni haijulikani kama kulikuwa na wafanya kazi ndani ya jumba hilo.

Labda wenye ubavu wa kupata habari za huko wanaweza kututonya ili tujue hawa ndugu zetu wa Muungano wako na hali gani baada ya mtikisiko huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…