Mkuu,
Acha kutu tukania dada na mama zetu, usaliti katika masuala ya ndoa unatokea kwa pande zote mbili waume na wake na usichukue isolated cases na kuwahukumu watu wote. Umetoa mfano wa rafiki yako alie msomesha mkewe mpaka chuo kikuu na baada akamsaliti mumewe iweje case hiyo moja au kama kuna nyingine 100 ndio iwe hukumu kwa akina mama zaidi ya milioni 20 Tanzania? Je na mimi nikitoa mfano wa "rafiki" yangu alianza ground zero na mkewe na baada ya kupata ulaji akamtupa na kuchukua totoz itatosha kuwa ni hukumu kwa wanaume wote?
Ni muhimu tuwe makini katika masuala ya ndoa za watu hili jamvi ni kubwa na linasomwa na wengi, sikutarajia mtu calibre ya Philemon Michael kutoa maoni ya ki ze utamu utamu. Tokea awali ulianza kupotosha na kumtaja mumewe Ghasia kwa jina silo umesahihishwa sasa unakuja na blah blah za "rafiki" yako.