Jerry Silaa: Alex Msama ni tapeli namba 3 wa Viwanja, ajisalimishe

Jerry Silaa: Alex Msama ni tapeli namba 3 wa Viwanja, ajisalimishe

Msama mzushi tu miaka nenda rudi.....
Kuna wakati fulani alifungua mgahawa wake pale jirani na bestbite,mbeleni huko si akataka kumfanyia figisu yule mama mwenye eneo,kumbe yule mama mme wake mtu mzito,msama aliondolewa pale kama mwizi
Jambo lolote ukifanya na msama lazima uzushi uzushi utakuwepo

Ova
Leo unamkana kada mwenzako siyo? 😂
 
Mkimalizana nae katika hili Mamlaka nyingine imkamate kwa Kosa la Kudhulumu Mishahara na Stahiki za Wafanyakazi ( Waandishi wa Habari ) wa iliyokuwa Media ( hasa Gazeti ) akiongozwa na Marehemu Dada Yamola.
Mbowe pia ni mshiriki wa kosa kama hili hili.
Amewadhurumu stahiki zao waandishi wa iliyokuwa "Tanzania Daima" gazeti la habari lililokuwa likichapishwa na free media ikimilikiwa na Freeman Aikael Mbowe na kusimamiwa na mwanae Dudley Freeman Mbowe.
 
Basi jamaa ana pepo la dhuluma. Angetulia pale ule mgahawa ulikuwa unafanya vizuri sana kibiashara. Hizo tamaa zimemponza.
Msama tapeli tapeli dhuluma namjuwa miaka mingi sana
Na pale kwenye mghahawa ule alishapaweka sawa na akawa anapata sana,ttz lake huo uzushi
Wake na longolongo
Pale aliondolewa kama mwz vile

Ova
 
Eti promota wa nyimbo za injili ,tamasha la pasaka?
Mkiambiwa dini ya ukristo ni kiota cha kile ndege mchafu muwe mnakubali.
Wezi kwa utapeli, waganga na wachawi , wapiga deal na watawala wamejificha kwenye dini.
Tatizo sio dini, kabla ya alex msama kuna tapeli mwingine tena ni muslim, ila anakula kodi ya kitapeli eneo lisilo lake. Ndio kusema uislam ni utapeli no?

Matapeli, wezi, dhulumati wapo haijalishi dini ipi au dini gani.
 
Jamaa ni tapeli mkubwa sana wa viwanja na amewashika watu wa ardhi wote hata huyo kamishna unaweza kukuta ni mtu wake so waziri akitaka kumkomesha msama adeal nae mwenyewe. Msama anaweza hadi kuiba viwanja vya serikali haogopi wanashirikiana na watu wa wizarani.

Ile wizara wangeifumua yite kuna majizi pale hatari sana.
Huko wizaran wamejaza watu wao
So ni Hadith tu,utamu kolea,uongoo njoo
 
Hivi huyu ndiye aliye lalamikiwa na mwimbaji wa nyimbo za injili Rose Mhando ??

Looo!! Kumbe huyu jamaa ni mafia kiasi hiki!
Yes
Na nimeona mahali akihojiwa amesema ss imefika Muda aongee ukweli amechoka kukaa kimya na kusemewa uongo
 
Alafu hili jambo la pesa limejengeka hadi kwa makarani wa Mahakama, wanakwambia kabisa, flani ana pesa lazima ashinde kesi! Sasa mimi najiuliza kesi ni pesa au ni ushahidi usiyo acha shaka !?
Tanzania kesi ni pesa, ikiwa ushahidi upo wazi hakimu anakula pesa halafu kesi inapigwa kalenda hata miaka 10 ili mwenye haki achoke kufatilia
 
Promota wa Tamasha la Pasaka, Mtangazaji wa vipindi vya kwaya na Mgombea wa nafasi mbalimbali za uongozi huko CCM, Bwana Alex Msama ametajwa kuwemo kwenye 3 bora ya Matapeli Papa wa Viwanja DSM.

Taarifa kamili hii hapa

====



Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amemtaka Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama kujisalimisha kwa Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Dar es salaam akiwa na baadhi ya watu waliouziwa eneo la viwanja namba 1 kitalu 22 lililopo Kibada Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es salaam ili kurejesha kwa wananchi eneo hilo lijengwa shule ya sekondari.

Silaa ametoa maagizo hayo alipofanya ziara katika eneo hilo Manispaa ya Kigamboni baada ya mgogoro huo kuwa wa muda mrefu kati ya wananchi wa eneo hilo na baadhi ya watu walionunua eneo la shule akiwemo Allex Msama.

Aidha, Waziri Silaa amemtaja Alex Msama kuwa ni tapeli namba 3 wa viwanja jijini Dar es salaam na tayari ameishaagiza baadhi ya maeneo anayoyamiliki kinyemela kunyang’anywa ikiwemo eneo la wazi na eneo la fukwe lililopo Mbweni Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam.

Mwanahalisi Digital
PAMOJA NA UKADA WA CCM KUMBE NI TAPELI
 
Hii ishu ilimalizikaje!!??
CCM kwa CCM, ulitegemea nini?
Ni marufuku kada kumwajibisha kada.
Ufumbuzi hutafutwa pole pole na kimya kimya
Huwezi kuamini tuna awamu ya sita badala ya tano.
Chama kile kile, watu wale wale na kazi inaendelea.
 
Back
Top Bottom