Jerry Silaa hajahudhuria shauri lake, Kamati yaomba kumkamata

Jerry Silaa hajahudhuria shauri lake, Kamati yaomba kumkamata

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Dodoma. Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki Maadili na Madaraka ya Bunge, Emmanuel Mwakasaka amesema ameomba kibali kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai cha kukamatwa kwa mbunge wa Ukonga (CCM), Jerry Silaa baada ya kutofika katika shauri lake.

Silaa alihojiwa mara ya kwanza na kamati hiyo Agosti 24, 2021 ambapo mwenyekiti wa kamati hiyo Mwakasaka alimtaka kurudi tena leo Alhamisi kuendelea na mahojiano.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Agosti 26, 2021 mwenyekiti huyo alisema ameomba kibali cha kukamatwa kwa mbunge huyo baada ya kutofika katika shauli lake.

Mwakasaka amesema Silaa hakutoa taarifa za kutofika kwake na kwamba kamati hiyo ilimsubuiri hadi saa 8.00 mchana, hivyo wamemwomba Spika kutoa kibali cha kukamatwa kwake na kufikishwa katika kikao cha kamati hiyo kesho saa 4.00 asubuhi.

Chanzo: Mwananchi
 
Hata hili la Gwajima kukataa kukaa wakati wa kuhojiwa litamgharimu sana.
 
 
Back
Top Bottom