Jerry Silaa kutolewa ardhi, tutarajie tena migogoro ya ardhi kuanza kuibuka upya na matapeli wa ardhi kuanza kutembea vifua mbele

Alitakiwa kumdhibiti kwa kumuongezea NGUVU kama alivyo Fanya kwa Waziri Mkuu kumuongezea Bashungwa kuwa Naibu wake
 
Wapi na wapi nimemtaja aliye sahihi kwenye CCM ya nchi hii! We elewa kwamba nchi inaendeshwa kwa sheria!

Hakuna utashi mzuri dhidi ya sheria kwenye kuendesha nchi, suluhu za majukwaani zinapumbaza! Msiwe wavivu wa kusoma na kujifunza!
 
Acheni tukuza watu kwani wizara ya aridhi imeanza leo ,wamepita wangapi? Heshima ni kipimo cha utu
 
Nchi unatakiwa ujumuike nao kwenye upigaji, ukienda tofauti wanakuwekea mizengwe
 
Raisi kakosea kumtoa huyu kwenye hii wizara ni ngumu kupata mtu anajua zaidi yake matatizo ya Ardhi
Kwa sasa hawezi kumpata na sifikirii kama atampata mtu mwenye utashi, msimamo na moyo wa uthubutu wa kupambana na matapeli wa ardhi kama Jerry Silaa. Kwa vile raisi huwa hashtakiwi kwa makosa anayofanya akiwa madarakani.

Basi tungeshauri itungwe sheria ya kuwawajibisha wale wanaomshauri raisi pumba ili wawe wanahukumiwa kutokana na makosa yatokanayo na ushauri wao mbovu. Ni wazi kuna watu wamepambana kuhakikisha mh Jerry anang'olewa katika ile wizara.
 
Jerry Silaa hana lolote kazi alizokuwa akizifanya pale Ardhi ni kazi Mahakama na mabaraza ya ardhi.
Ukifuatilia hizi kesi utagundua kwamba kuna kesi nyingi tu zimefika mahakamani nyingine toka enzi za Nyerere, Mwinyi, Mkapa na mpaka Magufuli lakin hakuna la maana lililofanyika kuamua kesi hizo.

Sasa huyu jamaa yeye kaja kuondoa ujinga unaofanywa na mahakama na hayo mabaraza ya ardhi yaliojaa ukiritimba. Halaf hizi mahakama si ndio huwa zinalaumiwa kila siku hata na wapinzani kuwa nyingi zimejaa rushwa na uzandiki wa hali ya juu.

Nakumbuka kuna mkutano mmoja wa Iringa (kama sijasahau) katibu mwenezi mwenyewe wa wakati huo ndugu Paul Makonda alizungumzia swala la mahakama kukosa usimamiaji mzuri wa sheria. Sasa inawezekanaje leo zionekane kuwa ndio zinaweza kuamua kila kesi ya ardhi bila waziri husika kuchukua maamuzi.
Jerry kama Waziri alikuwa hajui anafanya nini zaifi ya kutafuta jukwaa la kukuza jina lake na hili kafanikiwa haswa kuwapata wajinga wajinga kama wewe.
Humu lazima kuna matapeli ya ardhi na chawa wao wametumwa kuja kupinga kila jema litakaloongelewa kuhusu Silaa ili kuhakikisha wanamuharibia sifa alizokuwa nazo huko wizarani.
 
Matapeli wa Viwanja mnavyopenda Mahakama na Mabaraza ya Aridhi kisa tu muhalalishiwe dhuluma zenu mnazofanya kwa watu! Mmeshindwa kumuhonga Jerry mmebaki kumchukia!!
Kumbe ningejua kama ushamjibu, basi nisingejisumbua kumjibu kwa mara ya pili katika comment yang namba 189 😂😂😂
 
Hii imenikumbusha
Magufuli alipotolewa Wizara ya Ujenzi na kupelekwa Kuhesabu samaki(Mifugo)

Magufuli hakuwa Eng lakini alikuwa anajuwa caravat linatengenezwaje na ubora wake
Alikuwa anajuwa Wizi wote katika tenda za Barabara
Umenikumbusha mbali mjombaa 😂😂😂
 
Nakubaliana na wewe
 
Asante mkuu P kwa mchango wako wenye kuelewesha na kuelimisha. Wewe ni mtu mkubwa mwenye heshima zako humu. Hivyo nina imani hiki ulichoandika hapa kitakuwa pia kimesomwa na wengi, hivyo pengine kuna watu watamfikishia mama aone jinsi watu tunavyolalamika kuhusu maamuzi yake ambayo mengine hayana faida yoyote kwa taifa.

Makonda alianza vizuri kamtoa kamuweka mtu asieweza kufit nafasi ile. Silaa kaanza vizuri kamtoa kamuweka mtu asiefit nafasi yake. Lakini cha kushangaza wale ambao wanahitaji kubadilishwa au kutolewa katika nafasi zao kwa sababu ya uzembe, ufisadi au ukosefu wa uzalendo ndo wanaendelea kuachwa ili waendelee kuharibu zaidi.

Kuna wizara ambazo mpaka leo wengine mawaziri wake hatuwajui kutokana na mawaziri hao kushindwa kujishughulisha na shughuli za wizara zao kama alivyokuwa akijishughulisha Silaa, lakini hao mpaka leo hawajaguswa na kila mkeka ukitoka wao wapo tu.
 
Mbona kesi nyingi zinaonekana ni za kipindi kirefu mno. Kuna kesi za toka enzi za utawala wa Nyerere, zingine enzj za Mwinyi, Mkapa nk. Sasa unaweza kujiuliza wewe mwenyewe kuwa toka enzi za Nyerere na Mwinyi mpaka leo washapita mawaziri wa ngapi wa ardhi. Hao makamishna hiyo miaka yote toka enzi ya Nyerere mpaka sasa Samia walikuwa wapi kuwasaidia mawaziri waliopita kabla ya Silaa. Mbona waliotapeliwa wengi wameonekana kuanza kupata ufumbuzi wa matatizo yao kipindi hiki cha Silaa na sio cha mawaziri wengine waliopita.

Wahindi wanasema "Baniani baya lakini kiatu yake nzuli bana".

Na sisi waswahili tunasema "Mnyonge myongeni lakini haki yake mpeni".

Silaa alikuwa anakwenda vizuri kuliko mawaziri wengine wote waliopita katika wizara hiyo.
 
Umeandika vizuri sana.
 
Mama naye Sasa pumzi imekata
Imekuwa palinga chibite

Hii Sasa Imani inetutoka
Anataka iweje

Joto la matumaini ya haki ameififisha
Kweli kabisa. Sasa ashaanza kutunyong'onyesha wengi ambao hatukuwa na tatizo nae.
 
Raisi na wasaidizi wake wote ni binadam wanaoweza kukosea kama mimi na wewe tunavyokosea. Mara ngapi unakuta wanamtoa mtu au wanamuhamisha, halaf baada ya muda wanaona kuwa wamekosea na kumrudisha katika nafasi yake ya mwanzo, au waliemtoa kumteua katika nafasi nyingine.

Ukitaka kujua kama raisi kweli ana macho mengi lakini anaweza kukosa fatilia ule uteuzi waliomteua mtu ambae tayari alikuwa na siku tatu ameshafariki kwa ajali ya gari.
 
Katia hasara watu wanadai fidia kwa mihemko yake faler yule akwendeleee huko akafye mbele
 
Ushahidi wa kuthibitisha ulichoandika uko wapi?
Sasa vijijini wangempa nini na yeye anatafuta chochote kwa ajili ya kampeni
Kampeni gani tena na wakati inaaminika kuwa CCM siku zote huwa inaiba kura. Yani mpinzani hata akishindanishwa na kuku, kama huyo kuku atagombea kwa ticket ya CCM basi anauhakika wa kushinda kwa njia yoyote ile.

Sasa hizo hela aibe kwa kampeni ya nini tena na wakati uhakika upo?
 
Wengine tuliona ni makosa kuondolewa kwa Lukuvi.
Lukuvi alikuwa mzuri na pia mfuatiliaji lakini kuna baadhi ya watu (matapeli) alikuwa anahofia kuwa face na kuwanyang'anya viwanja walivyotapeli.

Lakini Silaa yeye mfuatiliaji na haogopi tapeli yoyote. Ukijifanya wewe ni tapeli sugu wa viwanja, unaeogopeka huku ukiwa hauna hati ya kueleweka ya viwanja hivyo, basi anakunyang'anya mchana kweupe na unaenda kunyea debe na ubabe wako.
 
Alitakiwa kumdhibiti kwa kumuongezea NGUVU kama alivyo Fanya kwa Waziri Mkuu kumuongezea Bashungwa kuwa Naibu wake
Mwaka gani tena Bashungwa alikuwa naibu wa waziri mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…