Jerry Silaa kutolewa ardhi, tutarajie tena migogoro ya ardhi kuanza kuibuka upya na matapeli wa ardhi kuanza kutembea vifua mbele

Jerry Silaa kutolewa ardhi, tutarajie tena migogoro ya ardhi kuanza kuibuka upya na matapeli wa ardhi kuanza kutembea vifua mbele

No one is indispensable, hivyo sii kweli kuwa hakuna mtu anajua mambo ya ardhi zaidi ya Jerry, watu ila hawajatafutwa, uwaziri hauombwi na hauna usaili!.

Kitu ambacho nakubaliana na wewe, Jerry did the best, amethubutu, ni kweli watu wenye uthubutu wa kiwango hicho ni wa kutafuta kwa tochi!.

Pia naunga mkono hoja yako its wrong kumteua mtu na kumtoa baada ya too short time, and he was the best performer, kama Konda Boy was the best kwenye uenezi na akatolewa baada ya muda mfupi.

Ukiwa unataka kwenda safari lakini hujui unataka kwenda wapi, huwezi kujua utumie njia gani, ili ufike kwasababu hujui unakwenda wapi, matokeo yake ni kutanga tanga na hufiki!.

Mimi kama naziona dalili za mtu kutanga tanga kwa mbali, as if baadhi ya teuzi zinafanywa kwa gues work and trial and error, unamteua mtu kumjaribisha hapa kama atafiti, asipofiti, unamuondoa, kitu cha ajabu ni kama hata best performers kama Jerry Ardhi, nae anaondolewa I seriously doubt, kama anajua anataka nini.

Mwanzo nisema tusimlaumu kwa makosa ya kukoseshwa na wasaidizi wake, nikashauri tumpe muda, Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda but as times goes by, nimeanza kujiridhisha kuwa ..

P
Alitakiwa kumdhibiti kwa kumuongezea NGUVU kama alivyo Fanya kwa Waziri Mkuu kumuongezea Bashungwa kuwa Naibu wake
 
Hao uliokuwa unaona wanatii sheria walifanya kitu gani cha maana zaidi ya kile alichofanya Silaa. Silaa alikuta kuna watu walitapeliwa viwanja vyao tangu enzi za Nyerere. Mawaziri wote tangu enzi za Nyerere, Mwinyi mpaka Magufuli walipita bila kuwasaidia si kwa sheria wala kash kash kama ya Silaa.

Lakini Silaa alipoingia alianza kuzirudisha ardhi hizo kwa wamiliki halali na kuwafanya waliokuwa wanapanga kuendelea na utapeli kuogopa kuendelea na utapeli wao. Alaf leo unakuja kuleta habari za sheria. Hivi kuna kiongozi wa serikali au chama chochote nchi hii anaefata sheria zote kwa 100%?
Wapi na wapi nimemtaja aliye sahihi kwenye CCM ya nchi hii! We elewa kwamba nchi inaendeshwa kwa sheria!

Hakuna utashi mzuri dhidi ya sheria kwenye kuendesha nchi, suluhu za majukwaani zinapumbaza! Msiwe wavivu wa kusoma na kujifunza!
 
Niaje waungwana

Japo hakuna mtu mwenye dhamana ya kumpangia raisi kile anachoamua, lakini katika hili la kumtoa Silaa ardhi na kwenda kumtupa huko kwenye habari kwa kweli Rais wetu amefanya kosa la kiufundi sana.

Jerry alikuwa ashaanza kuwashughulikia vibaka na matapeli wa ardhi wote, yaani mmoja baada ya mwingine hadi kupelekea wengine kutupwa ndani. Sasa leo anapotolewa na kupelekwa wizara nyingine ni kuwapa nafasi wale wote waliokuwa washaanza kurudisha ardhi walizotapeli kabla kiama hakijawashukia waendelee nazo na pengine kuendelea kutapeli na zingine kwani aliekuwa anawapa tumbo joto kaondolewa na kupelekwa kungine.

Najiuliza, kwanini hiyo wizara ya habari asingepewa hata Mwana FA, ili Silaa aendelee kuwanyoosha wezi na vibaka wa ardhi za watu!

Anyway acha tuone mwisho wa game utakuaje. Lakini mama kama unatusikia na kufanikiwa kusoma uzi huu tafadhali TUNAOMBA (kwa herufi kubwa) UMRUDISHE JERRY SILAA W/ ARDHI 🙏🙏
Acheni tukuza watu kwani wizara ya aridhi imeanza leo ,wamepita wangapi? Heshima ni kipimo cha utu
 
Nchi unatakiwa ujumuike nao kwenye upigaji, ukienda tofauti wanakuwekea mizengwe
 
Raisi kakosea kumtoa huyu kwenye hii wizara ni ngumu kupata mtu anajua zaidi yake matatizo ya Ardhi
Kwa sasa hawezi kumpata na sifikirii kama atampata mtu mwenye utashi, msimamo na moyo wa uthubutu wa kupambana na matapeli wa ardhi kama Jerry Silaa. Kwa vile raisi huwa hashtakiwi kwa makosa anayofanya akiwa madarakani.

Basi tungeshauri itungwe sheria ya kuwawajibisha wale wanaomshauri raisi pumba ili wawe wanahukumiwa kutokana na makosa yatokanayo na ushauri wao mbovu. Ni wazi kuna watu wamepambana kuhakikisha mh Jerry anang'olewa katika ile wizara.
 
Jerry Silaa hana lolote kazi alizokuwa akizifanya pale Ardhi ni kazi Mahakama na mabaraza ya ardhi.
Ukifuatilia hizi kesi utagundua kwamba kuna kesi nyingi tu zimefika mahakamani nyingine toka enzi za Nyerere, Mwinyi, Mkapa na mpaka Magufuli lakin hakuna la maana lililofanyika kuamua kesi hizo.

Sasa huyu jamaa yeye kaja kuondoa ujinga unaofanywa na mahakama na hayo mabaraza ya ardhi yaliojaa ukiritimba. Halaf hizi mahakama si ndio huwa zinalaumiwa kila siku hata na wapinzani kuwa nyingi zimejaa rushwa na uzandiki wa hali ya juu.

Nakumbuka kuna mkutano mmoja wa Iringa (kama sijasahau) katibu mwenezi mwenyewe wa wakati huo ndugu Paul Makonda alizungumzia swala la mahakama kukosa usimamiaji mzuri wa sheria. Sasa inawezekanaje leo zionekane kuwa ndio zinaweza kuamua kila kesi ya ardhi bila waziri husika kuchukua maamuzi.
Jerry kama Waziri alikuwa hajui anafanya nini zaifi ya kutafuta jukwaa la kukuza jina lake na hili kafanikiwa haswa kuwapata wajinga wajinga kama wewe.
Humu lazima kuna matapeli ya ardhi na chawa wao wametumwa kuja kupinga kila jema litakaloongelewa kuhusu Silaa ili kuhakikisha wanamuharibia sifa alizokuwa nazo huko wizarani.
 
Matapeli wa Viwanja mnavyopenda Mahakama na Mabaraza ya Aridhi kisa tu muhalalishiwe dhuluma zenu mnazofanya kwa watu! Mmeshindwa kumuhonga Jerry mmebaki kumchukia!!
Kumbe ningejua kama ushamjibu, basi nisingejisumbua kumjibu kwa mara ya pili katika comment yang namba 189 😂😂😂
 
Hii imenikumbusha
Magufuli alipotolewa Wizara ya Ujenzi na kupelekwa Kuhesabu samaki(Mifugo)

Magufuli hakuwa Eng lakini alikuwa anajuwa caravat linatengenezwaje na ubora wake
Alikuwa anajuwa Wizi wote katika tenda za Barabara
Umenikumbusha mbali mjombaa 😂😂😂
 
Sababu itoke wapi mkuu. Wao wameona wamtoe eidha kwa kutofatilia kile alichokuwa anafanya, au kuna kundi laI washauri wa raisi ambalo limeona kuwa masilahi yao yanakwenda kuguswa na Silaa kupitia wizara ya ardhi.

So wakaona bora wamshauri raisi amchomoe fasta fasta bila kosa wala maelezo.
Nakubaliana na wewe
 
No one is indispensable, hivyo sii kweli kuwa hakuna mtu anajua mambo ya ardhi zaidi ya Jerry, watu ila hawajatafutwa, uwaziri hauombwi na hauna usaili!.

Kitu ambacho nakubaliana na wewe, Jerry did the best, amethubutu, ni kweli watu wenye uthubutu wa kiwango hicho ni wa kutafuta kwa tochi!.

Pia naunga mkono hoja yako its wrong kumteua mtu na kumtoa baada ya too short time, and he was the best performer, kama Konda Boy was the best kwenye uenezi na akatolewa baada ya muda mfupi.

Ukiwa unataka kwenda safari lakini hujui unataka kwenda wapi, huwezi kujua utumie njia gani, ili ufike kwasababu hujui unakwenda wapi, matokeo yake ni kutanga tanga na hufiki!.

Mimi kama naziona dalili za mtu kutanga tanga kwa mbali, as if baadhi ya teuzi zinafanywa kwa gues work and trial and error, unamteua mtu kumjaribisha hapa kama atafiti, asipofiti, unamuondoa, kitu cha ajabu ni kama hata best performers kama Jerry Ardhi, nae anaondolewa I seriously doubt, kama anajua anataka nini.

Mwanzo nisema tusimlaumu kwa makosa ya kukoseshwa na wasaidizi wake, nikashauri tumpe muda, Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda but as times goes by, nimeanza kujiridhisha kuwa ..

P
Asante mkuu P kwa mchango wako wenye kuelewesha na kuelimisha. Wewe ni mtu mkubwa mwenye heshima zako humu. Hivyo nina imani hiki ulichoandika hapa kitakuwa pia kimesomwa na wengi, hivyo pengine kuna watu watamfikishia mama aone jinsi watu tunavyolalamika kuhusu maamuzi yake ambayo mengine hayana faida yoyote kwa taifa.

Makonda alianza vizuri kamtoa kamuweka mtu asieweza kufit nafasi ile. Silaa kaanza vizuri kamtoa kamuweka mtu asiefit nafasi yake. Lakini cha kushangaza wale ambao wanahitaji kubadilishwa au kutolewa katika nafasi zao kwa sababu ya uzembe, ufisadi au ukosefu wa uzalendo ndo wanaendelea kuachwa ili waendelee kuharibu zaidi.

Kuna wizara ambazo mpaka leo wengine mawaziri wake hatuwajui kutokana na mawaziri hao kushindwa kujishughulisha na shughuli za wizara zao kama alivyokuwa akijishughulisha Silaa, lakini hao mpaka leo hawajaguswa na kila mkeka ukitoka wao wapo tu.
 
slaa sio kwamba alikuwa anajua, ni rahisi sana, unaita kamishna wa ardhi, chagua case moja mbili tatu, anapewa lecture na picha halisi, anaenda eneo la tukio anajua kila kitu, akihojiana na raia unafikiri anajua matatizo yote kumbe kalala jana amekariri kama form one anayekariri achimedes principle. hayo mambo sio magumu kama mnavyofikiri kwasababu chini yake ana watendaji wazoefu kuliko yeye wanaomsaidia kufanya kazi.
Mbona kesi nyingi zinaonekana ni za kipindi kirefu mno. Kuna kesi za toka enzi za utawala wa Nyerere, zingine enzj za Mwinyi, Mkapa nk. Sasa unaweza kujiuliza wewe mwenyewe kuwa toka enzi za Nyerere na Mwinyi mpaka leo washapita mawaziri wa ngapi wa ardhi. Hao makamishna hiyo miaka yote toka enzi ya Nyerere mpaka sasa Samia walikuwa wapi kuwasaidia mawaziri waliopita kabla ya Silaa. Mbona waliotapeliwa wengi wameonekana kuanza kupata ufumbuzi wa matatizo yao kipindi hiki cha Silaa na sio cha mawaziri wengine waliopita.

Wahindi wanasema "Baniani baya lakini kiatu yake nzuli bana".

Na sisi waswahili tunasema "Mnyonge myongeni lakini haki yake mpeni".

Silaa alikuwa anakwenda vizuri kuliko mawaziri wengine wote waliopita katika wizara hiyo.
 
Wanaweza wakawepo wengine wa kuiendesha wizara ya ardhi lakini kwa nini tupoteze muda wa kumtafuta mwingine wakati tayari alishapatikana anayeiwezea hiyo,it doesnt make any sense.
Sasa itakuwa ni mchezo wa trial and error hadi miaka 10 inaisha kitafanyika kitu gani cha maana cha kuibadilisha nchi?
Kumbuka kwenye baraza la mawaziri tukisema tuanze kuwatathmini mawaziri kiuhalali kabisa utapata mawaziri wanne tu ambao wanafanya kazi yao kwa ufanisi na uweledi sasa hao hao wanne tena unawainterfere badala ya kutafuta vipaji vipya kwa ajili ya wizara zingine zilizobaki ili idadi ya wachapakazi iongezeke sasa huoni hapo tunakuwa kama tunacheza tu.
Umeandika vizuri sana.
 
Mama naye Sasa pumzi imekata
Imekuwa palinga chibite

Hii Sasa Imani inetutoka
Anataka iweje

Joto la matumaini ya haki ameififisha
Kweli kabisa. Sasa ashaanza kutunyong'onyesha wengi ambao hatukuwa na tatizo nae.
 
Kuwa waziri mzuri hakuhitaji kutumia nguvu sana na a lot of publicity… Huenda ata waliomtangulia walikuwa na impact kubwa kuliko ata yeye lakini walikuwa hawapendi attention za media kama yeye . However migogoro ya Ardhi haimaliziki kwa kutumia sana nguvu bali burasa na utulivu wa kuelewa kiini cha migogoro . Alifanya kadri awezavyo lakini sio Sawa kusema ni makosa. Mh Raisi anamacho Mengi na anajua zaidi why kamtoa hapo . Sijajua kwa nini nguvu kubwa inatumika katika hili….

Wapo mawaziri wengi mfano Simbachawene na wana utulivu wa hali ya juu na impact kubwa , sasa mpaka waonekane wakifokea wananchi Ndo wawe bora ???
Anyway mimi naona alikopelekwa panamfaa zaidi !
Raisi na wasaidizi wake wote ni binadam wanaoweza kukosea kama mimi na wewe tunavyokosea. Mara ngapi unakuta wanamtoa mtu au wanamuhamisha, halaf baada ya muda wanaona kuwa wamekosea na kumrudisha katika nafasi yake ya mwanzo, au waliemtoa kumteua katika nafasi nyingine.

Ukitaka kujua kama raisi kweli ana macho mengi lakini anaweza kukosa fatilia ule uteuzi waliomteua mtu ambae tayari alikuwa na siku tatu ameshafariki kwa ajali ya gari.
 
Katia hasara watu wanadai fidia kwa mihemko yake faler yule akwendeleee huko akafye mbele
 
Amekula nyingi kwa muda mfupi, alikuwa anatembea viunga vya matajiri kama Mikocheni, Mbezi, Mbweni, mikoa mitamu mitamu kama Arusha, Mwanza, Dodoma ambako anaweza kupata chochote, alitelekeza kabisa kamati ya kitaifa ya utatuzi wa migogoro ya ardhi ambayo ililenga vijijini.
Ushahidi wa kuthibitisha ulichoandika uko wapi?
Sasa vijijini wangempa nini na yeye anatafuta chochote kwa ajili ya kampeni
Kampeni gani tena na wakati inaaminika kuwa CCM siku zote huwa inaiba kura. Yani mpinzani hata akishindanishwa na kuku, kama huyo kuku atagombea kwa ticket ya CCM basi anauhakika wa kushinda kwa njia yoyote ile.

Sasa hizo hela aibe kwa kampeni ya nini tena na wakati uhakika upo?
 
Wengine tuliona ni makosa kuondolewa kwa Lukuvi.
Lukuvi alikuwa mzuri na pia mfuatiliaji lakini kuna baadhi ya watu (matapeli) alikuwa anahofia kuwa face na kuwanyang'anya viwanja walivyotapeli.

Lakini Silaa yeye mfuatiliaji na haogopi tapeli yoyote. Ukijifanya wewe ni tapeli sugu wa viwanja, unaeogopeka huku ukiwa hauna hati ya kueleweka ya viwanja hivyo, basi anakunyang'anya mchana kweupe na unaenda kunyea debe na ubabe wako.
 
Alitakiwa kumdhibiti kwa kumuongezea NGUVU kama alivyo Fanya kwa Waziri Mkuu kumuongezea Bashungwa kuwa Naibu wake
Mwaka gani tena Bashungwa alikuwa naibu wa waziri mkuu?
 
Back
Top Bottom