Jerry Silaa kutolewa ardhi, tutarajie tena migogoro ya ardhi kuanza kuibuka upya na matapeli wa ardhi kuanza kutembea vifua mbele

Mi nalinda taifa na siyo kujenga
Sasa unalindaje kitu kisichojengwa mkuu. Hata nyumba inabidi kwanza uijenge alaf ndo uilinde.

Mwl Nyerere alijenga kwanza misingi ya nchi na utaifa. Halaf ndo akailinda misingi hiyo isije kuanguka au kuharibiwa.
 
Hata mimi najiuliza hivyo, by the way kuna wajuzi wa mambo zaidi yetu tunaoona kwa macho ya nyama.
 
Duu inawezekana matapeli wa ardhi wako hadi .......................
Inawezekana wapo au hawapo, lakini wakatumia rupia kuwafanya washauri wa mama wamshawishi mama amtoe Silaa kule awekwe mtu wao.
 
Tanzania hii.. Mtu anayepinga ufisadi , ndio huzushiwa ajali kila aina ya kisiasa , hata ya kimwili... Ilikuwa hamna sababu yenye mashiko kumuondoa Jerry .... Yaani sijui wanatakiwa viongozi wa aina gani?
 
Unajua kwa nini alikuwa anatumia muda mwingi mikocheni, mbweni, kariakoo, Mwanza,Morogoro, Dodoma,Arusha? Huko alikuwa analazimisha Makamishna wa Ardhi wampe viwanja vya bure, na akienda maeneo potential kama Mikocheni na kwingine, apewe cha juu kwa kumtisha tajiri

Sehemu kama Kintinku, Gairo, au Manyoni na Mpanda humuoni
 
Je, yeye ndio mwenye uwezo wa kushughulika kiuwajibika na hakuna mtu mwingine?

Au wangempa Ask Gwajima?
Huyo Ndejembi hatumfahamu lakini nafikiri anatokea Dodoma huyu mwenye nasaba na Malecela
 
Sababu iko wazi, ameenda tofauti na falsafa ya chama chake, washazoea dhulma halafu jerry hataki dhulma
Kashindwa kutanzua dhuluma iliyotokea kwa wananchi wa Mbopo kudhulumiwa ardhi na DDC na KMC watu waliwekeza wakanyang'nywa mbele ya mtutu wa bunduki yeye kimya.

Kipunguni ambayo imo ndani ya jimbo lake wanadai serikali kulipwa fidia kwa kuchukuliwa maeneo yao kwa ajili ya kupanua uwanja wa ndege halafu mnamsifu ni mtendaji. Nilimdharau kuwatishia polisi wananchi wa Morogoro
 
ila bibi anazingua, yaani kumtoa kijana namimi imeniuma sana. Kijana alikuwa na nia ya kuwasaidia wananchi kwa moyo wake wote nikimtazama. Sasa anakuja kutuwekea watoto wa viongozi ambao wamepewa nafasi hizo kwa heshima za wazazi wao na si kwa kuwa na sifa.....yaani nikisikia ukoo tu mfano; makamba, pinda, nnauye, mavunde, ndejembi, kikwete, nani sijui...yaani hawa wote ni vilaza hamna kitu.....ni majina ya baba zao ndio yapo ...upendeleo wa watawala na kulipana fadhila. Lakini ukisikia ukoo unaitwa makonda, slaa, chalamila, mtaka, mpina, majaliwa, mwamri, unajua wazi kuwa ni watu wa kazi kazi
 
Tanzania hii.. Mtu anayepinga ufisadi , ndio huzushiwa ajali kila aina ya kisiasa , hata ya kimwili... Ilikuwa hamna sababu yenye mashiko kumuondoa Jerry .... Yaani sijui wanatakiwa viongozi wa aina gani?
Labda wanatakiwa viongozi wanaoshinda wanalala ofisini, alafu mwisho mwezi analipwa mamilioni yanayotokana na kodi zetu.
 
Bado umerudi kule kule kwenye porojo zako ambazo hazina ushahidi.
 
Ni kweli mkuu.
 
Je, yeye ndio mwenye uwezo wa kushughulika kiuwajibika na hakuna mtu mwingine?

Au wangempa Ask Gwajima?
Huyo Ndejembi hatumfahamu lakini nafikiri anatokea Dodoma huyu mwenye nasaba na Malecela
Wanaweza wakawepo wengine wa kuiendesha wizara ya ardhi lakini kwa nini tupoteze muda wa kumtafuta mwingine wakati tayari alishapatikana anayeiwezea hiyo,it doesnt make any sense.
Sasa itakuwa ni mchezo wa trial and error hadi miaka 10 inaisha kitafanyika kitu gani cha maana cha kuibadilisha nchi?
Kumbuka kwenye baraza la mawaziri tukisema tuanze kuwatathmini mawaziri kiuhalali kabisa utapata mawaziri wanne tu ambao wanafanya kazi yao kwa ufanisi na uweledi sasa hao hao wanne tena unawainterfere badala ya kutafuta vipaji vipya kwa ajili ya wizara zingine zilizobaki ili idadi ya wachapakazi iongezeke sasa huoni hapo tunakuwa kama tunacheza tu.
 
Mama naye Sasa pumzi imekata
Imekuwa palinga chibite

Hii Sasa Imani inetutoka
Anataka iweje

Joto la matumaini ya haki ameififisha
 
Inawezekana wapo au hawapo, lakini wakatumia rupia kuwafanya washauri wa mama wamshawishi mama amtoe Silaa kule awekwe mtu wao.
Mkuu inawezekana hii Dunia hakuna kitu watu wanashindwa isipokuwa kufufua aliyekufa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…