Vifungu vya 7 na 15 vya Sheria ya Tawala za Mikoa ya mwaka 1997 imempa mamlaka Mkuu wa mkoa kuweka Mtu mahabusu Kwa masaa 48 (kif.7). Mkuu wa wilaya sheria imemruhusu kumweka Mtu ndani Kwa masaa 24 (kif.15) pale inapothibitika Mtu Huyo anàhatarisha Amani ya mbele yake.
Nimejaribu kuisoma sheria hiyo yote lakini sijaona kifungu kinachompa Waziri yeyote mamlaka ya kumweka Mtu mahabusu. Lakini ni kawaida nchini na jana tu Waziri wa Ardhi Jerry Slaa akiwa Kihonda Morogoro aliamuru mwananchi akamatwe na OCD na kuwekwa ndani Kwa kutoa maelezo Kwa kirefu wakati Waziri alimtaka atoe Kwa kifupi.
Kabla ya kutoa amri hiyo alimkatisha Msemaji na kumwambia hataki hotuba anataka majibu kitu ambacho mzungumzaji alishindwa na kuendelea kutoa maelezo na hivyo kumuudhi MHESHIMIWA WAZIRI na kuamuru akamatwe na OCD mara moja.
Swali langu Nataka kujua kama kuna sheria nyingine tofauti na nikiyoitaja inayompa Waziri mamlaka ya kuweka watu mahabusu kadri wanavyojisikia.
Sasa kama hata nyie wenzangu na Mimi mnajua Hana mamlaka hayo, hiyo Tume ya maadili ya viongozi wa Umma inafanya kazi gani? Je, haya si matumizi mabaya ya madaaka?
Kuhusu Mkuu wa Wilaya nimeweka kifungu. Nijulishe kuhusu Waziri kama kuna kifungu. Madaraka ya Waziri ni Makubwa lakini hayampi hadhi ya Ulinzi na usalama.
Jerry Silaa amelewa sifa. Uongozi wa vitisho hauna nafasi kwenye kizazi hiki. Sijaona kosa la wananchi wote hao wawili.
Nahisi Waziri Silaa amekuja na majibu yake (preconceived ideas), kumbe kunako ground mambo ni vice versa. Hawezi kuukabili ukweli na ndiyo maana anaamua kuwatoa wenye ukweli kwenye mkutano. This is bullshit