Jerry Silaa na matumizi mabaya ya Madaraka: Waziri kapata wapi mamlaka kuwaweka mahabusu watanzania?

Jerry Silaa na matumizi mabaya ya Madaraka: Waziri kapata wapi mamlaka kuwaweka mahabusu watanzania?

Katika hili tukio ambapo waziri wa ardhi Jerry Silaa anaamuru OCD kumkamata mzungumzaji kosa la anayezungumza ni nini?View attachment 3042185
Slaa anaumia kuona kama anaporwa nafasi ya kuhutubia....maana ni yeye tu anapaswa kuhutubia vinginevyo ataamrisha polisi wakufunge masaa 24.....Ndio zile za: " Hivi unanijua mimi ni nani"?.... Zimerudi kwa Kasi! 🤔
 
Hawa viongozi wetu bwana yaani kisa waziri basi hataki hata kujibiwa lolote la raia yeyote.

hapo kaenda kutafuta suluhu au kutisha watu.

Awamu hii imejaa viongozi wa aina hii ambao wapo kwa ajili ya kutishia raia na sio kuwatumikia.
 
Hakuna kosa lolote alilo fanya ni upumbavu tuu wa watawala kutaka kunyenyekewa na kupewa sifa kila sehemu, haka kajamaa kalivyo pewa nafasi kuna watu tulisema haka na kenyewe ndio wale wale tukaonekana tunamuonea wivu haya kameanza kuonesha rangi zake
 
Jamaa hajui kuongea na authority.
Umevamia eneo, unaulizwa swali unaanza kupiga chenga na kuleta madharau.
Mimi naona Jerry Slaa yupo sawa. Imevamia eneo la serikali, utakamatwa na kufunguliwa mashtaka. Cha ajabu ni nini hapo?
Una uthibitisho gani wa yeye kuvamia eneo? Kwa nini akuhojiwa tangua mwanzo na polisi kwa kufuata taratibu za kumuhoji mshatikiwa ?
 
Dharau gani emeleta?
Usipende kutumia neno
Ngoja kwanza
Kwani hukusikia?
Huelewi?
Sikiliza basi ...
Sasa si ndiyo nakwambia?
Kwani we unaonaje?
Hebu tuliza kwanza .... Etc ni maneno yanayoonyesha dharau kwa authority.
 
hiyo authority, wala sio authority, mwenye authority hapo ni mwananchi, jerry hata hilo shati kavaa kwa kodi za hao wananchi, na aliyemteua ameweka madarakani na hao wananchi. kwanini hampi nafasi ya kusikilizwa ili atatue tatizo?
Mwananchi Hana authority mbele ya kiongozi. Labda kwa ujumla wao.
Tusijidanganye, Kuna ideal situations na real situations.
Try your best to live in the second.
 
Una uthibitisho gani wa yeye kuvamia eneo? Kwa nini akuhojiwa tangua mwanzo na polisi kwa kufuata taratibu za kumuhoji mshatikiwa ?
Kuvamia ardhi ni kazi rahisi sana kutambua. Labda hufuatilii Mambo tu unaangalia juujuu. Una hatimiliki .... Sina. Umenunua eneo toka kwa nani? .... Mwenyekiti.
Unajua hili eneo ni msitu wa Serikali (Reserved land) ...... Mimi natoa michango kama vile matofali etc ... Blah blah.

Badala ya kusema sijui, unaanza maneno maneno.
Unajua???
Jibu swali.
Ni kutaka kuamini uongo kilazima, ubishi na dharau kwa sababu ushazoea kununua haki kwa viongozi wadogo.
 
Uongozi unataka hekima sana
Mbona mwanzo alikuwa mtulivu sana what happened to him now?
Amekuwa na hasira za haraka
Mimi sijaona shida ya hao wawili, ila kwa kuwa ana uwezo wa kuamuru mtu afungwe sawa, ila sio haki

Hapo anaenda kufungwa kwa kosa gani
Kama mimi ni OCD ningehoji ila kwa kuwa wote tunaogopana basi
 
Back
Top Bottom