Jerry Silaa na matumizi mabaya ya Madaraka: Waziri kapata wapi mamlaka kuwaweka mahabusu watanzania?

Jerry Silaa na matumizi mabaya ya Madaraka: Waziri kapata wapi mamlaka kuwaweka mahabusu watanzania?

Usipende kutumia neno
Ngoja kwanza
Kwani hukusikia?
Huelewi?
Sikiliza basi ...
Sasa si ndiyo nakwambia?
Kwani we unaonaje?
Hebu tuliza kwanza .... Etc ni maneno yanayoonyesha dharau kwa authority.
Kulingana na katiba ya Tanzania ambayo kiongozi msomi wa sheria Jerry Slaa anatumia, kuambiwa "ngoja kwanza" ni kosa??

Ngoja kwanza ni kosa gani limefanyika. Kwahiyo huyo Slaa yuko sahihi kumkamata mwananchi aliyesema hivyo?
 
Kuvamia ardhi ni kazi rahisi sana kutambua. Labda hufuatilii Mambo tu unaangalia juujuu. Una hatimiliki .... Sina. Umenunua eneo toka kwa nani? .... Mwenyekiti.
Unajua hili eneo ni msitu wa Serikali (Reserved land) ...... Mimi natoa michango kama vile matofali etc ... Blah blah.

Badala ya kusema sijui, unaanza maneno maneno.
Unajua???
Jibu swali.
Ni kutaka kuamini uongo kilazima, ubishi na dharau kwa sababu ushazoea kununua haki kwa viongozi wadogo.
Kama Waziri tayari alikuwa anajua huyo mtu ni mhalifu mvamizi wa ardhi kwa nini alikuwa anafanya majadiliano naye kwa nini police wasingekuwa wamemfungulia hiyo kesi mapema badala yake wanasuburi kuja kupewa amri na Waziri?
Hata hivyo haionekani kwamba Waziri aliamuamrisha OCD amkamate kwa kosa hilo.
 
Katika hili tukio ambapo waziri wa ardhi Jerry Silaa anaamuru OCD kumkamata mzungumzaji kosa la anayezungumza ni nini?View attachment 3042185
Shida kubwa ya viongozi wa kitanzania hawana uvumilivu kabisa wanaamini zaidi katika matumizi ya nguvu kwakuwa wana jeshi la polisi ambao nao hawajui washike lipi, halafu kila kiongozi anajisikia kufanya linalo mfurahisha yeye na watu wake hata kama linaliuka haki ya mwingine na sio kufuata sheria na haki za wengine. Kifupi viongozi wengi wa tanzania wanapenda sana kutukuzwa.
 
Katika hili tukio ambapo waziri wa ardhi Jerry Silaa anaamuru OCD kumkamata mzungumzaji kosa la anayezungumza ni nini?

Sikiliza vizuri, hakuna mahala Slaa kasema "mkamate", Slaa kasema mchukuwe. Yaani amchukuwe amuondowe hapo, kaja kusaidiwa analeta ujuwaji kuongea hovyo.
 
CLIP IMEREKODIWA KWA KUKATA MATUKIO MUHIMU ILI KUMCHAFUA MH. WAZIRI. ALYEKUWA ANAONGEA NA MH WAZIRI NI MTU ALIYEVAMIA ARDHI
Hata kama kweli angekuwa mvamizi wa ardhi unafahamu kwamba waziri hana mamlaka ya kuamrisha polisi kumkamata mtu??
 
Amuondowe pale alipo Slaa, atajuwa yeye pa kumpeleka.
Waziri hana mamlaka hayo wala hatakiwi kutumia polisi hivyo, ni ukiukwaji mkubwa wa sheria na matumizi mabaya ya madaraka.
 
Waziri hana mamlaka hayo wala hatakiwi kutumia polisi hivyo, ni ukiukwaji mkubwa wa sheria na matumizi mabaya ya madaraka.
Wacha waziri, hata wewe ukiwa na kikao na mkutano wako na kuna mtu humtaki awepo, unayo mamlaka hayo.
 
Hata kama kweli angekuwa mvamizi wa ardhi unafahamu kwamba waziri hana mamlaka ya kuamrisha polisi kumkamata mtu??
ARDHI NI WIZARA INAYOFUATIA KWA UGUMU BAADA YA MALI ASILI NA UTALII. UKITAKA UFUATE KILA KITU KISHERIA KWENYE WIZARA HII, UNAONDOKA WEWE WAZIRI HALAFU UNAWAACHA WAVAMIZI WA ARDHI WANAENEDLEA NA MAMBO YAO. WAKATI MWINGINE INABIDI KUTUMIA COMMON SENSE TU NA SI LAZIIMA IWE SHERIA
 
Hapo kwenye hilo tukio common sense iko wapi??
 
Viongozi wanajisahau sana wanajiona miungu watu...Ebu angalia Chalamila alivyowapiga biti wafanyabiashara simu buku bee na huyo silaa anatoa maagizo jamaa akamatwe wakati anatoa hoja ieleweke vizuri ila jerry hataki kumsikiliza...Yaani viongozi wa kiafrika ni hopeless ndiyo maana wakishatoka kwenye vyeo wanaishia kabisa.
 
juhudi za wazi za kumhujumu mama....kipind hiki uchaguzi unakatibia ndio wanafanya hiv vitu vya kijinga....mama toa hao
 
Back
Top Bottom