Jerry Silaa: Serikali iweke Tozo ya Tsh. 100 kwenye mafuta yanayonunuliwa Dar ili Kupata Pesa za Kujenga Barabara za Jiji

Jerry Silaa: Serikali iweke Tozo ya Tsh. 100 kwenye mafuta yanayonunuliwa Dar ili Kupata Pesa za Kujenga Barabara za Jiji

Sawa yawezekana ana hoja ya msingi but chanzo chake cha pesa kwaajil ya hizo barabara noooo!! Nadhan zichukuliwe kwanza pesa zote zilizoibiwa toka report ya CAG iliyopita mpaka hii ya sasa, litolewe fungu kwaajil hiyo!!!
Kwa nn hawa wabunge asitoe hoja ya hela zilizopo China, na kwenye account ya plea bargain itumike kwa kazi hiyo, maana makosa yalifanyikia Dar, basi wanufaika wawe wa Dar
 
Kwa nn hawa wabunge asitoe hoja ya hela zilizopo China, na kwenye account ya plea bargain itumike kwa kazi hiyo, maana makosa yalifanyikia Dar, basi wanufaika wawe wa Dar
Yes, yaan wanatoa hoja za kuzid kuwaumiza wananchi wakat kuna pesa nying san wangezichukua na kufanyia maendeleo!!
 
Kuanzia leo naacha kufuatilia mambo ya nchii hii. kila siku linaiibuka jambo jipya na linaniuumiza hadi natamani nihame nchi.

Ila one day mambo yangu yakikaa poa ntaihamisha familia yangu na kun’goa mizizi yangu na kwenda kuipanda ulaya huko.

STUPID GAVAMENTI
 
Sawa yawezekana ana hoja ya msingi but chanzo chake cha pesa kwaajil ya hizo barabara noooo!! Nadhan zichukuliwe kwanza pesa zote zilizoibiwa toka report ya CAG iliyopita mpaka hii ya sasa, litolewe fungu kwaajil hiyo!
Labda uniambie kwanza watafute muarobaini wa wizi ili zikikatwa zitumike kweli..! Gharama unayotumia kwa foleni na kununua vipuri na kuchelewa kazini ni zaidi ya mara 500 ya hiyo sh.100
 
Sh.100 inamuathiri vipi mtu wa Dar wakati Mikoani difference ya bei ya mafuta Dar na Mkoani ni Kati ya sh.300-700?
Unaweza nikumbusha kwa budget ya 22/23 CAG kasema zimetumika vibaya shilingi ngapi?
Hizo Bil 558 za magar mapya kila mwaka wakipunguza zitamuathiri vip mwanachi wa kawaida.... ficha hiyo akili kiongozi
 
Labda uniambie kwanza watafute muarobaini wa wizi ili zikikatwa zitumike kweli..! Gharama unayotumia kwa foleni na kununua vipuri na kuchelewa kazini ni zaidi ya mara 500 ya hiyo sh.100
Kwani wahusika wa ufisadi si wapo? Au ni mabeberu toka nje wameiba na kukimbia? Wabinywe kwanza warudishe hela, zielekezwe kweny maendeleo!!
 
Huwa siwasikii wabunge wakisema kuwa upunguzaji wa matumizi kama chanzo cha kuongeza feddha kwenye bajeti ya Maendeleo.
 
Sawa yawezekana ana hoja ya msingi but chanzo chake cha pesa kwaajil ya hizo barabara noooo!! Nadhan zichukuliwe kwanza pesa zote zilizoibiwa toka report ya CAG iliyopita mpaka hii ya sasa, litolewe fungu kwaajil hiyo!
Trioni mbili unusu zimepigwa Tanroads huu mpago tozo ndio utasababisha tuingie Mabarabarani Nchi nzima.
 
Mhe. Jery Slaa yawezekana amejisahau. Kwenye bidhaa za mafuta ya magari na mitambo, tayari kuna asilimia ya kodi inayoitwa Road Toll ambayo hutozwa kwa kila lita moja ya mafuta. Kuongeza sh. 100 kwa wakazi wa Dar ni kuwabebesha gharama nyingine zaidi.

Kama wazo lake ni hilo, basi awaambie Waziri wa Fedha na Mipango ile fedha ya kodi ambayo inatozwa kwenye mafuta kwa wakazi wa Dar ipelekwe Dar kwa ajili ya kujenga miundombinu ya barabara za Dar.
 
Akichangia mjadala wa Bajeti ya Tamisemi,mbunge wa Ukonga Jerry Silaa Kwa niaba ya Wabunge wa Dar es Salaam amependekeza Kwa Serikali Iweke Tozo ya Shilingi 100 Kwa mafuta yanayonunuliwa Jijini humo Ili kupata Fedha za kujenga Barabara za Jiji la Dar es Salaam.

Jerry Silaa amesema amesema Jiji la Dar es Salaam linatumia zaidi ya Lita milioni 3 Kwa mwaka ambazo zinaweza kuwezesha Jiji la Dar kupata Bil.130 Kwa mwaka ambazo zitatumika kujenga Miundombinu ya Barabara ndani ya Jiji Hilo.

Aidha Silaa amesema Shilingi 100 itakayoongezwa italeta msawazo wa bei na maeneo mengine ya Nchi ambayo yananunua mafuta Kwa bei kubwa sana,akisema formula yake ataiwasilisha Kwa Waziri wa Tamisemi na Wizara ya Fedha.

My Take: Jerry Silaa ana Hoja ya msingi na asikilizwe, nimeipenda ubunifu wake sio Kila kitu kusubiria mikopo.
Jerry Silaa hana hoja bali ni mvivu wa kufikiri. Hatuwezi kuendelea kujaza tozo kwenye petroli kila leo. Hii imekuwa too much.

Tunaponunua Petroli kwa Tsh 3,000 kwa lita ujue kabisa landing cost plus import duty ni Tsh 1,500. Kinachobakia ambacho ni Tsh 1,500 ni tozo mbalimbali kama Ewura, RDL, Road fund etc.

Watanzania tujiulize swali moja; Sasa hivi dunia inakwenda kwenye clean energy kama matumizi ya magari yanayotumia umeme, Je itakuwaje kama tutahamia huko kwa kiasi kikubwa hata sisi?
 
Mawazo mazuri ila akili za Hawa jamaa sometimes sijui Kuna tatizo Gani. Unawezakushangaa Wazo likapita lakini kichefuchefu kikaja kwenye utekelezaji.

Mambo yalianza hivi hivi kwenye tozo za muamala ya kibenki Kwa kauli kupishana wakajikuta wanaita hizo tozo VAT mwisho wa siku akabebeshwa mzigo mwananchi. Yaani unatoa pesa benki, unajatwa gharama, na Bado hiyo gharama unatozwa VAT.
 
Yaani wapige maela zaidi ya hizo kila mwaka halafu eti waseme tozo iwekwe kwenye mafuta kupata hela ya kujenga miundombinu, hivi hawa wabunge wamelaaniwa au...
Jibu lako ni la msingi. Isitoshe Awamu iliyoko madarakani imegubikwa na masuala ya kisiasa zaidi kuliko maendeleo.

Kimsingi, tangu iingie madarakani, miradi inayotekelezwa ni ile iliyoanzishwa Awamu iliyopita kwa kuchelea aibu ingawa imeweka tozo, mikopo na kutembeza bakuri la misaada kwa kuingia mikataba inayoifanya nchi shamba la bibi.
20230418_115034.jpg
 
Huu ni upumbavu kuna hela zinapigwa nyingi kuliko 100 zetu hawaziongelei halafu wanataka hizi 100 nazo wazipige
 
Akichangia mjadala wa Bajeti ya Tamisemi,mbunge wa Ukonga Jerry Silaa Kwa niaba ya Wabunge wa Dar es Salaam amependekeza Kwa Serikali Iweke Tozo ya Shilingi 100 Kwa mafuta yanayonunuliwa Jijini humo Ili kupata Fedha za kujenga Barabara za Jiji la Dar es Salaam.

Jerry Silaa amesema amesema Jiji la Dar es Salaam linatumia zaidi ya Lita milioni 3 Kwa mwaka ambazo zinaweza kuwezesha Jiji la Dar kupata Bil.130 Kwa mwaka ambazo zitatumika kujenga Miundombinu ya Barabara ndani ya Jiji Hilo.

Aidha Silaa amesema Shilingi 100 itakayoongezwa italeta msawazo wa bei na maeneo mengine ya Nchi ambayo yananunua mafuta Kwa bei kubwa sana,akisema formula yake ataiwasilisha Kwa Waziri wa Tamisemi na Wizara ya Fedha.

My Take: Jerry Silaa ana Hoja ya msingi na asikilizwe, nimeipenda ubunifu wake sio Kila kitu kusubiria mikopo.
Azungumzie kushusha posho za wabunge wote ili fedha itakayookolewa huko ndiyo ipelekwe kwenye hayo matumizi
 
Back
Top Bottom