Jerry Silaa: Wabunge tuanze kukatwa kodi kwenye Mishahara yetu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mbunge wa Ukonga Jerry Slaa, amesema imefikia hatua Wabunge waanze kulipa kodi kupitia mishahara yao ili wapate uwezo wa kuwaambia Wananchi na wao walipe kodi.

Silaa ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliowashirikisha wananchi wa Mzinga Ukonga jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo jimboni kwake.

"Mie nimeanza Ubunge juzi mwaka jana mwezi wa 11, kwahiyo nimekuta hayo yanayosemwa mengine yameshapitishwa tayari Bungeni na katika hili niungane na Mbunge wa Kinondoni, Abbas Tarimba kwamba vikiliwa vya Mwali na vya Kungwi viliwe”

“Ni wakati muafaka sisi Waheshimiwa Wabunge ili tupate uwezo wa kuwaambia Watu waanze kulipa kodi na sisi tuanze kulipa kodi katika mishahara yetu, hakuna sababu ya kuwa wengine wanalipa wengine hawalipi ukishakuwa haulipi unakosa ile nguvu ya kumwambia mwenzako alipe”

“Kwahiyo niseme tu kwamba kazi kubwa inayotakiwa tuifanye sisi kama viongozi ni kutowadanganya Watanzania kwamba tunaweza kuiendesha nchi bila Kodi, haitowezekana”-Jerry Silaa

Zaidi, soma


 
Now we are talking We finally, found someone who has the courage to speak it out!

Sasa akaongelee hili swala bungeni ..... Ila nafikiri mpaka sasa atakuwa amepigiwa simu na akina Ndugai kumpiga mkwara!!
 
Namuunga mkono Mh.Mbunge wangu.

It's a waking up call.

Wabunge waanze kukatwa Kodi katika mishahara yao!

#NikoNaMbungeWanguMh.Silaa
#KaziIendelee
 
Back
Top Bottom