Jerry Silaa: Wabunge tuanze kukatwa kodi kwenye Mishahara yetu
Eeh kumbe wabunge hawalipi kodi [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Halafu wanatuletea mambo ya uzalendo
 
Wote wale wale tuuu. Watakubali kukatwa kodi then watajiongezea mishahara na maposho kufidia pale.
Hawa sio wa kuamini hata kidogo.
Nimeanza kumwelewa jamaa yangu alisema usiwe rafiki na politician any more. Mtumie pale unapomhitaji tuu

Hawana wema hawa
 
Mbunge wa Ukonga Jerry Slaa, amesema imefikia hatua Wabunge waanze kulipa kodi kupitia mishahara yao ili wapate uwezo wa kuwaambia Wananchi na wao walipe kodi.

Silaa ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliowashirikisha wananchi wa Mzinga Ukonga jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo jimboni kwake.

"Mie nimeanza Ubunge juzi mwaka jana mwezi wa 11, kwahiyo nimekuta hayo yanayosemwa mengine yameshapitishwa tayari Bungeni na katika hili niungane na Mbunge wa Kinondoni, Abbas Tarimba kwamba vikiliwa vya Mwali na vya Kungwi viliwe”

“Ni wakati muafaka sisi Waheshimiwa Wabunge ili tupate uwezo wa kuwaambia Watu waanze kulipa kodi na sisi tuanze kulipa kodi katika mishahara yetu, hakuna sababu ya kuwa wengine wanalipa wengine hawalipi ukishakuwa haulipi unakosa ile nguvu ya kumwambia mwenzako alipe”

“Kwahiyo niseme tu kwamba kazi kubwa inayotakiwa tuifanye sisi kama viongozi ni kutowadanganya Watanzania kwamba tunaweza kuiendesha nchi bila Kodi, haitowezekana”-Jerry Silaa
View attachment 1864670
Ikijaga kutokea hali hii baas utakua ni uzalendo wa hali ya juu kbs nasi tutashawishika kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa
 
Si wanadai kuwa mishahara yao (wabunge) inatumika kulipia mahitaji ya wapiga kura wao, suala ambalo halina ukweli wowote. Hawana aibu hata kusema wapiga kura wao huwafuata mpaka bungeni kuwapelekea shida zao.
Hii kitu hata Mwl shulen hutoa msaada kwa wanafunzi wake pale tu anapkuja akiwa na shida lakin kodi iko palepale na mshahara wake kidogo.
Pia si wote hutoa hiyo misaada anayojinadi bungeni
 
Jerry, lazima apongezwe na kuungwa mkono kwa hii kauli ya kizalendo.

Kodi kwa wabunge litaiingizia Taifa mapato ya zaidi ya Tshs 3 Billion kwa mwaka!!
 
Nadhani kipindi cha Ndugai ndio bunge limejitungia sheria za kipuuzi. Ukisoma sheria ya Kodi ya Mapato - Second Schedule huoni waliposamehewa kodi. kwa maana hiyo kuna sheria za kitapeli zinapitishwa na bunge halafu zinafichwa, haziwekwi kwenye sheria za kodi. hebu fungua Income Tax Act iliyopo kwenye mtandao wa TRA kifungu husika, hutaona huo msamaha
 
Kwani walikuwa hawalipi kodi?
Na kwanini walikuwa hawalipi?
Serikali kama mwajili na mlipaji Mkuu wa mishahara ya Watumishi ione busara kuanza kutoza kodi kila inayemlipa ili kuondoa matabaka na kukuza uzalendo kwa wengine kulipa kodi.
 
Vipi Posho ?
Waendelee Kulipwa ?, Sababu huenda hilo ndio likawa baya zaidi kwa ustawi wa kodi zetu...
 
Huu ndio uzalendo lol
Mifumo ya kodi nchi hii Mimi naushangaa

Kodi anatakiwa kwanza alipe Rias ndio wengine tufuate

Mtu ulipi kodi hata ya choo kuuza mkojo tsh200 utaweza kuwa na uchungu na pesa za umma ?

Ndio maana viongozi majizi tu.
 
kumbe mishahara yao haipapaswi eeehhh...basi sawa
 
Mwanga umeanza kuonekana walau kwa sehemu
Huyo ni wa kupongezwa
 
Mbunge wa Ukonga Jerry Slaa, amesema imefikia hatua Wabunge waanze kulipa kodi kupitia mishahara yao ili wapate uwezo wa kuwaambia Wananchi na wao walipe kodi.

Silaa ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliowashirikisha wananchi wa Mzinga Ukonga jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo jimboni kwake.

"Mie nimeanza Ubunge juzi mwaka jana mwezi wa 11, kwahiyo nimekuta hayo yanayosemwa mengine yameshapitishwa tayari Bungeni na katika hili niungane na Mbunge wa Kinondoni, Abbas Tarimba kwamba vikiliwa vya Mwali na vya Kungwi viliwe”

“Ni wakati muafaka sisi Waheshimiwa Wabunge ili tupate uwezo wa kuwaambia Watu waanze kulipa kodi na sisi tuanze kulipa kodi katika mishahara yetu, hakuna sababu ya kuwa wengine wanalipa wengine hawalipi ukishakuwa haulipi unakosa ile nguvu ya kumwambia mwenzako alipe”

“Kwahiyo niseme tu kwamba kazi kubwa inayotakiwa tuifanye sisi kama viongozi ni kutowadanganya Watanzania kwamba tunaweza kuiendesha nchi bila Kodi, haitowezekana”-Jerry Silaa
View attachment 1864670
Angalau huyu kaongea kitu kizuri. Waongezeke wabunge kama hawa wanaofikiria vizuri. Sio sabufa ana bwatuka tuu pwaa pwaaa
 
Now we are talking ......... We finally, found someone who has the courage to speak it out!!

Sasa akaongelee hili swala bungeni ..... Ila nafikiri mpaka sasa atakuwa amepigiwa simu na akina Ndugai kumpiga mkwara!!
Kamfunga paka kengere na Mungu amlinde,Sasa yule mbunge alisema mshahara hautoshi akisikia hiki Tena🤣🤣
 
Back
Top Bottom