Jerry Silaa: Wabunge tuanze kukatwa kodi kwenye Mishahara yetu
Mbunge wa Ukonga Jerry Slaa, amesema imefikia hatua Wabunge waanze kulipa kodi kupitia mishahara yao ili wapate uwezo wa kuwaambia Wananchi na wao walipe kodi.

Silaa ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliowashirikisha wananchi wa Mzinga Ukonga jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo jimboni kwake.

"Mie nimeanza Ubunge juzi mwaka jana mwezi wa 11, kwahiyo nimekuta hayo yanayosemwa mengine yameshapitishwa tayari Bungeni na katika hili niungane na Mbunge wa Kinondoni, Abbas Tarimba kwamba vikiliwa vya Mwali na vya Kungwi viliwe”

“Ni wakati muafaka sisi Waheshimiwa Wabunge ili tupate uwezo wa kuwaambia Watu waanze kulipa kodi na sisi tuanze kulipa kodi katika mishahara yetu, hakuna sababu ya kuwa wengine wanalipa wengine hawalipi ukishakuwa haulipi unakosa ile nguvu ya kumwambia mwenzako alipe”

“Kwahiyo niseme tu kwamba kazi kubwa inayotakiwa tuifanye sisi kama viongozi ni kutowadanganya Watanzania kwamba tunaweza kuiendesha nchi bila Kodi, haitowezekana”-Jerry Silaa
View attachment 1864670
Kumbe hawalipi?? Nijuavyo wanalipa ila posho ambazo ndio nyingi hazikatwi ..this is eye opening. Tuanzie hapo
 
Huu ndio uzalendo lol
Hakuna cha uzalendo wala nini. Kama kweli Mh. Slaa amesema hivyo, basi hajui maana ya kodi ni nini kwasababu Wabunge wanakatwa kodi kwenye mishahara yao. Ambacho hakikatwi kodi na hii ni kwa watumishi wote ni marupurupu na posho wanazozipata nje ya mishahara yao. Kama na hayo anataka yakatwe kodi hapo nitaelewa.
 
Tuseme hakuwepo Bungeni wakati wanapitisha Tozo? Wanasiasa watz wasituone watanzania ni wajinga kiasi hiki
 
Hatuwezi kuendesha nchi kwa kutegemea TOZO.mbunge yupo sahihi,lazima Kodi walipe.
Mbunge wa Ukonga Jerry Slaa, amesema imefikia hatua Wabunge waanze kulipa kodi kupitia mishahara yao ili wapate uwezo wa kuwaambia Wananchi na wao walipe kodi.

Silaa ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliowashirikisha wananchi wa Mzinga Ukonga jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo jimboni kwake.

"Mie nimeanza Ubunge juzi mwaka jana mwezi wa 11, kwahiyo nimekuta hayo yanayosemwa mengine yameshapitishwa tayari Bungeni na katika hili niungane na Mbunge wa Kinondoni, Abbas Tarimba kwamba vikiliwa vya Mwali na vya Kungwi viliwe”

“Ni wakati muafaka sisi Waheshimiwa Wabunge ili tupate uwezo wa kuwaambia Watu waanze kulipa kodi na sisi tuanze kulipa kodi katika mishahara yetu, hakuna sababu ya kuwa wengine wanalipa wengine hawalipi ukishakuwa haulipi unakosa ile nguvu ya kumwambia mwenzako alipe”

“Kwahiyo niseme tu kwamba kazi kubwa inayotakiwa tuifanye sisi kama viongozi ni kutowadanganya Watanzania kwamba tunaweza kuiendesha nchi bila Kodi, haitowezekana”-Jerry Silaa
View attachment 1864670
 
Huyu kijana ameongeaa maneno makubwaa mazuri sana sana.

Wakati muafaka mama Samia mkafanye marekebisho ya sheria za bunge Kodi ZIKATWE. Huwezii piga keleele bungeni MAKATO ya tozoo hukuu mnaiibia serikali kwa kutolipa Kodi

Wakati muafakaa Sasa mama yetu mkasikilize sauti ya kijana wetu mkaifanyie kazi.

Imenishangaza kuna WABUNGE wako mule mwaka wa kumi leo hii anapigia KELELE za tozo amesahau anatakiwa kulipa Kodi na kutolipa Kodi WABUNGE ni kuiibia serikali.

Namuomba malaika GABRIEL AKUSIMAMIE AKULINDE MDOGO WANGU JERRY SILAA, VITA HII N YA MUNGU NA UTASHINDA.
 
Rais hapa anatwishwa mzigo ambao sio wake,, Bunge ni chombo huru, ni swala la wabunge wenyewe kuamua..Tuone kama watagusa maslahi yao
Mkuu angalia saini za mama kwenye sheria ZAO

Kuwalima
Kodi hawa lazima waidhinishwe kimaandishi hakuna jinsi

Mamaa awe na MSIMAMO ashikilie hili Kuna vyanzoo vingi TU vya FEDHA mojawapo kadi za WABUNGE wanazotuibia kwakutolipa Kodi hiiii n dhaaaaambikubwaaaaa
 
Kweli kijana ameongea point Namuona Zungu na Ndugai wanakomalia Kodi ya miamala kumbe Wao Wao wanachukua nzima nzima
 
Umelewa ama una utaahira ewe mleta mada? Hujui kuandika rudi shule.
 
Back
Top Bottom