Jeshi la Guinea-Bissau lachukua madaraka baada ya Uchaguzi wenye utata

Jeshi la Guinea-Bissau lachukua madaraka baada ya Uchaguzi wenye utata

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,775
Reaction score
2,891
Maafisa wa Jeshi nchini Guinea-Bissau wametangaza kuchukua “udhibiti kamili” wa serikali leo siku ya Jumatano (Nov 26, 2025) wakisitisha mchakato wa uchaguzi na kufunga mipaka, zikiwa ni siku tatu tu baada ya taifa hilo maskini la Afrika Magharibi kufanya uchaguzi wa wabunge na rais ulioibua utata.

Saa chache baada ya milio ya risasi kusikika mchana karibu na Ikulu ya Rais, kikundi cha maafisa wanaojiita "Uongozi wa Juu wa Kijeshi kwa Urejeshaji wa Utulivu" kimetangaza kuwa kimetwaa udhibiti wa nchi hadi taarifa itakapotolewa.

Hatua hiyo ya kuchukua madaraka inakuja siku moja kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais na bunge uliofanyika Jumapili, Novemba 23.

Dakka chache kabla ya kutangazwa kwa mapinduzi ya kijeshi, Rais anayemaliza muda wake, Umaro Sissoco Embaló, aliripoti kukamatwa kwake akiwa Ikulu ya Guinea-Bissau.

Mgombea wa upinzani, Fernando Dias da Costa, ametoa wito kwa jeshi kubaki nje ya mchakato wa uchaguzi.

Rais Embaló alisema kuwa alikamatwa majira ya mchana siku ya Jumatano, akiwa ofisini kwake Ikulu, na maafisa wa jeshi pamoja na Mkuu wa Majeshi, naibu wake, na Waziri wa Mambo ya Ndani.

Mchana, jeshi lilitangaza kwamba limechukua udhibiti kamili wa Guinea-Bissau na kusimamisha mchakato wa uchaguzi.

Katika taarifa iliyosomwa na msemaji wa jeshi, Dinis N’Tchama, jeshi limesema hatua hiyo imefuatia kugundulika kwa mpango wa kuvuruga nchi uliowahusisha wanasiasa kadhaa wa kitaifa, wafanyabiashara wa dawa za kulevya, na majaribio ya kupindisha matokeo ya uchaguzi. Inaripotiwa kuwa hazina ya silaha nzito za kijeshi ilikamatwa na Huduma ya Taifa ya Ujasusi.

Kamandi Kuu ya Kijeshi kwa ajili ya Kurejesha Usalama wa Taifa na Utulivu wa Umma pia iliamuru kufungwa kwa taasisi za serikali, kusimamishwa kwa shughuli za vyombo vya habari, kufungwa kwa mipaka ya nchi kwa njia ya nchi kavu, baharini na angani, pamoja na kuwekwa kwa kutotoka nje kuanzia saa 3:00 usiku hadi 12:00 asubuhi.

Wakati huohuo, Fernando Dias da Costa, mgombea anayeungwa mkono na chama kikuu cha upinzani PAIGC na anayedai ushindi katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais wa 23 Novemba, ametoa wito kwa jeshi kubaki nje ya mchakato wa uchaguzi.

Katika video iliyoshirikiwa kwenye mitandao ya kijamii, amehimiza umma kubaki watulivu huku akisisitiza ushindi wake.

Milio mizito ya risasi iliripotiwa adhuhuri karibu na Ikulu ya Rais na ofisi za tume ya uchaguzi. Matokeo rasmi ya awali, ambayo yalitarajiwa kutolewa Alhamisi, sasa yamesitishwa.

====
Military officers in Guinea-Bissau declared they had seized "total control" of the government on Wednesday, suspending the electoral process and closing borders just three days after the impoverished West African nation held contested legislative and presidential elections.

The dramatic takeover unfolded as gunfire erupted near the presidential palace in the capital, Bissau, with soldiers in uniform blocking the main thoroughfare to the compound. Military personnel delivered their announcement from army headquarters, according to journalists from Agence France-Presse who witnessed the scene.

Troops from the presidential guard and an elite gendarmerie unit secured the now-deserted area around the palace after heavy shooting subsided midday Wednesday. Hundreds of residents had fled on foot and in vehicles as the gunfire rang out, seeking safety from the violence.

Source RFI & APA News
 
Screenshot_20251126_180538_X.jpg


Huko Guinea Bissau Wanajeshi wamefanya yao kuliepusha Taifa kuingia kwenye machafuko.

Baada ya Uchaguzi uliogubikwa na wizi wa kura,Wanajeshi wamemuweka kizuizini aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Bw. Umarro Sissoko.

Wanajeshi wamefanya hili kulinda Raia wao na kuiepusha Nchi yao na Machafuko pamoja na mauaji ya raia.

Kilichofanyika nchini Guinea Bissau ni funzo tosha kwa Chawa Mkuu anaevaa magwanda Generali Jacob Mkunda.


Kushindwa kwake kuchukua hatua kulinda Wananchi na mipaka ya Nchi kwa kuendekeza uchawa kulifanya Samia, DGIS na IGP kuingiza marcenaries kutoka Zanzibar, Uganda na Msumbiji na kuua maelfu ya Watanganyika. Sasa na yeye ni sehemu ya Watakaoozea jela ICC.

kwa Wazalendo wachache mliobaki JWTZ, MLmsiache kujifunza kwa wenzenu wa Guinea Bissau na Madagascar.
 
RAIS WA Guinea Bissau , kwanza

-akakizuia Chama Kikuu pinzan kushiriki Uchaguzi MKUU
👉Kisha akamfunga Mpinzan wake Mkuu
👉Ufisadi unaongezeka na umasikin ukaongezeka
👉Biashara ya Dawa za kulevya ikatamalaki, huku viongozi wa Serikali yake wakiongoza biashara hiyo.

Masaa KADHAA yalopita wakafanga Uchaguzi.

Upinzani ukatangaza kushinda.
RAIS alipo akatangaza kushinda.


Katika kuepusha Mauaji, JESHI LIMECHUKUA UDHIBITI WA NCHI.

Kwann Jeshi?? Kwa sababu wakati wa Uchaguzi Huwa hamna Rais .


Sisi hapa kwetu, huyu Pumbavu Mkunda, akakubali Nchi kudhibitiwa na Wahuni, matokeo yake wameua zaidi ya watu 100000.

MKUNDA UTATUJIBU TU HAPO BAADAE.
 
View attachment 3507914

Huko Guinea Bissau Wanajeshi wamefanya yao kuliepusha Taifa kuingia kwenye machafuko.

Baada ya Uchaguzi uliogubikwa na wizi wa kura,Wanajeshi wamemuweka kizuizini aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Bw. Umarro Sissoko.

Wanajeshi wamefanya hili kulinda Raia wao na kuiepusha Nchi yao na Machafuko pamoja na mauaji ya raia.

Kilichofanyika nchini Guinea Bissau ni funzo tosha kwa Chawa Mkuu anaevaa magwanda Generali Jacob Mkunda.


Kushindwa kwake kuchukua hatua kulinda Wananchi na mipaka ya Nchi kwa kuendekeza uchawa kulifanya Samia, DGIS na IGP kuingiza marcenaries kutoka Zanzibar, Uganda na Msumbiji na kuua maelfu ya Watanganyika. Sasa na yeye ni sehemu ya Watakaoozea jela ICC.

kwa Wazalendo wachache mliobaki JWTZ, MLmsiache kujifunza kwa wenzenu wa Guinea Bissau na Madagascar.
Media za Tanzania zitapita hapa kama zinaaga maiti kamwe haziwezi kutoa taarifa hii!
Screenshot_20251113-171829~2.png
 
Huyu anahusika kwa mauaji ya raia wa Tanzania
View attachment 3507924
Watu wenye mashavu makubwa kama haya huwa wana mushkeli kichwani halafu wanapenda kula kula hovyo.

Kuna lijamaa tulikuwa tunasoma nalo lina mashavu sana, basi linajamba jamba hovyo na kucheka cheka. Kwa kweli ni mtihani.

Usimuamini mtu mwenye mashavu kuvimba a.k.a MASHAVU KUNOGA.
 
Gen Mkunda you took an envelope,they took your voice, they took your strength, they took lives of your people, you lost your dignity.You sold your people with an envelope. Your envelope was a blood transaction. Augustino Polepole advised you to return the envelope. If another opportunity comes please betray the transaction and save Tanganyika.
 
Back
Top Bottom