Trump hakusema "wana Headaches tu". Tuweke taarifa sahihi. Tusipotoshe!
Trump alizungumza kitu hiki, nanukuu;
"I heard that they had headaches, and a couple of other things, but I would say, and I can report, it's not very serious,"
Hizo ni taarifa alizopewa kisha naye kuziwasilisha katika vyombo vya habari. Unahitaji nikutafsirie kwa Kiswahili?
Kuthibitisha kauli ya Trump kuwa "it's not very serious", wengi wa wanajeshi hao wapatao 110 wameripotiwa kurejea katika majukumu yao ya kawaida baada ya matibabu.
Kama hizo takwimu ni za uongo je, za ukweli ni zipi?
Kama Idara ya Ulinzi ya Marekani yenye dhamana ya kuzisimamia taasisi zote zinazohusu masuala ya kijeshi na kiulinzi nchini Marekani imekuwa ikitoa takwimu za uongo, je, takwimu za kweli ni zipi? Ziko wapi hizo takwimu?
Ushahidi wa kitafiti juu ya uongo wa takwimu hizo uko wapi? Ukweli ni upi? Usiishie tu kusema "ni kawaida kutoa takwimu za uongo".
No research, no right to speak....!!