Kikosi kingine hatari zaidi cha Wapalestina kimeibuka huko Ghaza kutowa sapoti kwa Hamas.
Hicho ndiyo kikosi kilichoanzishwa zamani na bingwa wa mapigano ya kimkakati "George Habash", kinaitwa PFLP lakini kilijulikana sana kama The Black September kwa utekaji wao wa ndege nne za abiria za mataifa makubwa kwa wakati mmoja. Pia kiliwahi kuteka kijiji kizima cha Olimpiki. Kiliwashirikisha vichwa vikali kama Carlos The Jackal na Lutif Afif na mwana dada wa shoka Leila Khaled.
Kikosi hicho ni hatari sana kwa kuwa kinahusisha siyo Wapalestina tu bali watu kutoka vikundi vyote vikali vinavyotetea wanyonge duniani, vikiwemo Red Brigades wa Italy IRA ya Ireland na vikundi vingine vya Amerika kusini
Kikundi hicho ndicho kilichoibuwa miamba maarufu duniani kama Carlos The Jackal kilikuwa kimya sana miaka mingi sana, kuibuka kwake kunasadikika kuwa kipo hai na kina operate middle east nzima kimya kimya. Kuibuka kwake kunaashiria kuwa hii vita haitoishia Ghaza tu, sasa hivi wakubwa wa nchi zote za Kiarabu zinazishirikiana na mazayuni, kama Saudi Arabia, Jordan, UAE saa hizi mavi debe. Kikundi hicho huwa kinalenga zaidi kwenye shina na mizizi, siyo matawi.