Moronight walker
JF-Expert Member
- Aug 3, 2021
- 3,103
- 4,704
Makundi ya waasi ya congo wanasiraha za KAWAIDA tuu mkuu.Huwa siwaelewi watu humu kulinganisha uwezo wa nchi dhidi ya nchi kwa kulinganisha performance ya nchi dhidi ya waasi.
Uturuki hii hapa ina makundi ya kigaidi kama YPG na PKK ila huwezi taja jeshi lolote la Afrika linaloweza ipiga Uturuki na Uturuki imeshindwa kuyamaliza hayo makundi.
Israel ina makundi hasimu kama Hezbollah na Hamas haijawahi wamaliza ila huwezi sema inazidiwa na labda Greece au Jordan kisa hazipambani na makundi ya wahuni.
Russia hii imewapiga ISIS na waasi wengine ila miezi zaidi ya tisa haijamalizana na Ukraine ambayo waasi wa Donetsk na Luhansk waliishinda.
Uwezo wa jeshi dhidi ya jeshi haupimwi tu kwa performance dhidi ya kundi la waasi. Kuna sababu nyingine tofauti.
Ukitazama defense procurement ya majeshi ya West Africa kama Chad na Mali miaka ya siku hizi unaona kabisa ni anti terror weapons ndio wananunua. Nigeria hao kwenye budget ya 2023 Buhari ashasaini Army ipewe fixed wing aircrafts pamoja na kwamba Air Force yao ilipinga vikali sanaView attachment 2429213
Hii ni bada ya kuona Air Force ina ndege nzito kama JF-17 ambazo ni unnecessary na zina high cost of maintenance na pia coordination inachelewa.
Wale washagundua huwezi pigana na gaidi kwa vifaru na masilaha mazito sana. M23 hawana air base au meli au kambi yenye majengo eti ndio ukapige hivyo unahitaji silaha nyepesi zinazobebeka kupigana nao. Silaha zinazotumika na mbinu kwao ni tofauti sana na zitakazotumika ukiambiwa kutoka Ngome andaa shambulizi kwenye bandari ya Mombasa kuharibu meli inayoshusha silaha.
Marekani imelazimika kutengeneza ndege nyingine ya ground attack inayotumia teknolojia waliyotumia mwisho vita ya pili ya dunia. Wanatengeneza Sky Warden, wameona ni gharama kubwa kutumia A-10 Warthog sijui F-16 kwenda kupiga kibanda cha mbao cha gaidi jangwani.
M23 au waasi hapo DRC hakuna mwenye MANPADS, hakuna anti tank rifles wala missiles, hakuna heavy machine guns sanasana utakuta waliambulia kuiba PKP Pecheneng chache ndio wanajidai nazo. Utawaona na RPG chache, yani wako local sasa ukiwatumia kama mlinganyo wa uwezo wa jeshi dhidi ya jeshi utajidanganya.
Counter terrorism na counter insurgency ni tofauti mno na high intensity warfare ambapo unakutanisha peer to peer enemies. Kama mtu hataki na hapa basi aendelee na uzalendo feki ila uzalendo na kujitoa mhanga kwa Wajapani WW2 hakukufua dafu mbele ya uhalisia wa Marekani.
Kama m23 watakua na
Ni AK-47 , LMG PKP, RPG, Labda na Heavy mashine gun kama Dshk au type w85 heavy machine gun, kama wanazo, maana heavy machine gun ni bunduki mzito hata kuzibeba japo sina UHAKIKA maana ni watu wa kuhamahama, na wanazidiwa sana tuu MAPIGANO na kukimbilia polini.
SIDHANI kama wanasiraha zaidi ya hizo. Hila watu wa HUMU ndani wanawapamba hatari,
Jeshi la ya congo kushindwa kupigana NAO ni madhaifu tuu ya kwao huko.