Jeshi la majini kazi yake ni ipi? kwanini hawakuenda kuokoa mwanza??

Jeshi la majini kazi yake ni ipi? kwanini hawakuenda kuokoa mwanza??

tikatika

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2011
Posts
2,330
Reaction score
4,121
katika nchi yetu kuna mgawanyo wa majeshi yetu. kuna jeshi la anga, la nchi kavu na jeshi la majini.

hiki kikosi maalumu cha majini makao makuu yake kipo kigamboni hapa Dar es salaam.

hivi kazi yake hiki kikosi ni kupigana vita ya kumwokoa nani au kumlinda nani kama kwenye ajali za majini hawawezi kufanya uokoaji??

sitaki kuamin kwamba hawa hawana vifaa. yaan nawafaham vizur wana kila aina ya vifaa vya majini. iwe usiku mvua jua wako tayari muda wote kukabiliana ndani ya maji. imekuaje tuko kimya kuhoji kazi ya kikosi hiki??

kazi ya jeshi sio kuchimba makabuli . kazi yao kubwa kuokoa, kukomboa, kulinda, kurejesha palipo bomoka. tumeona mara kadhaa wakijenga usiku na mchana madaraja.

yaan katika hili nitahoji kila nitakupopata nafasi ya kuliongelea. sitak kuongelea sijui ya waziri mkuu na mfuko wake wa majanga. hawa huwa siwajadili maana wamejaa bla bla tu. sitak kuamini na jeshi liingie kwenye utendaji wa wanasiasa. wao wakisikia sehem kimenuka wanapaswa kuamsha popo na sio kusubiri hawa wanasiasa.

angalizo kwa wale wanaodhan muda ulikua sio rafiki. yaan jeshi letu lina ndege za kivita. kufika mwanza hata dak 40 wanaweza kufika. kama wataalam wangekua hapa dar wangeweza kufika mwanza hata kuwazid walio hapo mwanza lakn wanatumia magari kutoka wilayani. ila ni kwamba inaonekana kazi ya jeshi ni kurusha ndege kututisha tukitaka kuandamana na siku ya uhuru. yaan napata hasira nikifikiria. sijui nani katuloga!!!
 
Hata hapa mwanza pembeni ya ziwa kitengo cha navy force sijui ni cha police TRA au JWTZ kipo naonaga wana speedboat moja ila na mimi na shaangaa kazi yao nini na ni lini? Kwasababu kutoka mwz hadi ukerewa kwa speed boat ya navy ni takribani kama dakika 25 tu....mbona hawakufanya wakati ketengo kina fungu? Ila tusilaumu sana kupanga ni kuchangua nasi tulichangua hivo.
 
Unless otherwise it was a planned mission. ..

Kuna msemo mmoja unasema kwamba" Ukiona tukio lolote la maafa limetokea na serikali haijajihusisha ubruptly kwa kufanya juhudu zozote ,basi huenda a warning sign was directed kwa taasisi maalumu inayohusika na uokoaji isifanye juhudi zozote prior to the onset of the scenario...""

ni maneno ya mwana falsafa mmoja kutoka Mitchigan Forest...
 
Inaonekana magendo kwa njia ya maji yanatumika sana nchii ndio maaana sishangai tonnage za unga na silaha kwenda nchi Jiran zinapita sana ktk bahari yetu. Ni wakati sasa kujisahihisha navy iwe na vifaa
 
Napatwa na kauvivu fulani hivi kufuatilia hizi inshu.
Kipi kipya wakuu hamjui uchawi Na ushirikina ni sifa ya viongozi Na serikali za Afrika.?
Kwanini wasitishe uokozi kisa Giza? Inaingia akilini hii..
Kwanini asiende kwenye msiba mkubwa kama huu??
A lot of Qns.
BTW kila MTU aamini kile anachofahamu Na kua mini
Ongeeni Na wazee mtapata ABC..
 
Binafsi huu msiba umenifanya nijiulize maswali mengi sana juu ya Serikali. Eti Mkuu wa Mkoa anatangazia Umma wamestisha uokoaji sababu giza kimeingua. Really [emoji24][emoji24] Nadhani kwenye list ya wanaotakiwa kuondoka huyu naye anastahili. Wavuvi wanawezaje kuokoa watu arobaini Serikali ikaokoa mmoja. What a Shame!!
 
Kipi kipya wakuu hamjui uchawi Na ushirikina ni sifa ya viongozi Na serikali za Afrika.?
Kwanini wasitishe uokozi kisa Giza? Inaingia akilini hii..
Kwanini asiende kwenye msiba mkubwa kama huu??
A lot of Qns.
BTW kila MTU aamini kile anachofahamu Na kua mini
Ongeeni Na wazee mtapata ABC..
Sibishi mkuu itakua kweli, ila swala la kustisha zoezi wanasema taa zilizopo zinamulika juu ya maji tu ila ukizama chini ni kiza kwahiyo wasingeweza kufanya kitu istoshe miili ilikua chini ya maji na sio juu
 
Kitengo cha majini yale ya Sheikh Yahya??
 
Hii inaleta walakini pale itakapotokea tukavamiwa na vikosi vya adui zetu kupitia njia ya majini,tutakwisha.

Eti giza,are we serious?Wananchi tujilinde wenyewe wallah dhidi ya majanga yoyote yale.
 
katika nchi yetu kuna mgawanyo wa majeshi yetu. kuna jeshi la anga, la nchi kavu na jeshi la majini.

hiki kikosi maalumu cha majini makao makuu yake kipo kigamboni hapa Dar es salaam.

hivi kazi yake hiki kikosi ni kupigana vita ya kumwokoa nani au kumlinda nani kama kwenye ajali za majini hawawezi kufanya uokoaji??

sitaki kuamin kwamba hawa hawana vifaa. yaan nawafaham vizur wana kila aina ya vifaa vya majini. iwe usiku mvua jua wako tayari muda wote kukabiliana ndani ya maji. imekuaje tuko kimya kuhoji kazi ya kikosi hiki??

kazi ya jeshi sio kuchimba makabuli . kazi yao kubwa kuokoa, kukomboa, kulinda, kurejesha palipo bomoka. tumeona mara kadhaa wakijenga usiku na mchana madaraja.

yaan katika hili nitahoji kila nitakupopata nafasi ya kuliongelea. sitak kuongelea sijui ya waziri mkuu na mfuko wake wa majanga. hawa huwa siwajadili maana wamejaa bla bla tu. sitak kuamini na jeshi liingie kwenye utendaji wa wanasiasa. wao wakisikia sehem kimenuka wanapaswa kuamsha popo na sio kusubiri hawa wanasiasa.

angalizo kwa wale wanaodhan muda ulikua sio rafiki. yaan jeshi letu lina ndege za kivita. kufika mwanza hata dak 40 wanaweza kufika. kama wataalam wangekua hapa dar wangeweza kufika mwanza hata kuwazid walio hapo mwanza lakn wanatumia magari kutoka wilayani. ila ni kwamba inaonekana kazi ya jeshi ni kurusha ndege kututisha tukitaka kuandamana na siku ya uhuru. yaan napata hasira nikifikiria. sijui nani katuloga!!!
Kwamba wewe ndiye unajua zaidi kuliko viongozi wa Jeshi, maana andiko limejaa shutuma tu!

Naamini kwa sasa utakuwa umepata taarifa JWT, Kikosi cha Wanamaji, ndicho kinafanya kazi hiyo. Hili ni baada ya kuandaa taritibu husika ili kazi ifanyike kwa umakini.

Tujifunze kuwa na subira katika mawazo yetu kabla ya kuyatoa nje ya vichwa vyetu.
 
Back
Top Bottom