Jeshi la majini kazi yake ni ipi? kwanini hawakuenda kuokoa mwanza??

Jeshi la majini kazi yake ni ipi? kwanini hawakuenda kuokoa mwanza??

Dah, haya mambo yanasikitisha! wazulu walikutana na bibi wa ziwani akawaambia wakome mara moja kuopoa la sivyo wawe tayari kubaki ujinini-wazulu wakatoka na kuandika report kwenda kwa aliyewaomba msaada wakapanda ndege makwao
Shida kabisa na story za kutungwa
 
Kifupi hatuna vikosi vyenye utayari kwa ajili ya uokozi. Police marines ndiyo wenye jukumu la msingi la kulinda raia na mali zao kwenye maji ila bahati mbaya sana hata muundo wake hauko sahihi na pia hawana vifaa vya vya kutosha vya uokozi lakini pia wao hawana mafunzo ya kutosha.

Ilitakiwa iwe unit inayojitegemea sio kuwa kitengo kimoja na zimamoto. Kwa sasa kipo chini ya zimamoto na uokoaji ndiyo maana hata ikitokea mtu kazama pale ferry utawaona wanakuja na gari la zimamoto. Bahati mbaya mno!!!!!

Wanahitaji vifaa vya kutosha vya kisasa ili waweze kufika popote kwa muda mfupi. Na kwa kawaida hakiwi kikosi cha watu wengi sana bali wachache ila wawe sehemu nyingi iwe rahisi kufika kwenye tukio.

Kikosi hiki maalum ambacho hakihitaji siasa wala wanasiasa kuamua au kushauri. Wanahitaji simu moja tu na sio maamuzi kikao cha kamati ya ulinzi na usalama cha mkoa au wilaya.

Navy ni jeshi la wanamaji nao wanatakiwa kufika kwenye tukio kama hao police marines wakihitaji msaada zaidi kwakuwa licha ya kuwa kazi yao ya msingi ni kulinda mipaka yetu kwenye maji lakini linapokuja suala la uhai wa watu wanatakiwa wafike kwenye tukio haraka zaidi kwakuwa wao wana vifaa bora zaidi na weledi zaidi.

Kifupi kama tungekuwa tuko makini na maisha ya watu, tukio hili la kusononesha,watu wengi wangeokolewa sababu limetokea mita chache toka ufukweni lakini limetokea kwenye ziwa ambalo ki jiografia sio korofi na halina kina kirefu.

Nawaza kuna maeneo hayafikiki kirahisi na korofi kama tanganyika nyasa au bahari hindi mbali huko ambako labda hata mawasiliano ya simu hayapo.

Nashauri police marines itenganishwe na zimamoto kwanza.
*Vifaa vya kisasa na waokoaji wenye weledi

Uwekezaji mkubwa kwenye kuepusha ajali za aina hii zisitokee badala ya kusubiri kuwa wepesi wa kuvaa nguo nyeusi!!

Kinga ni bora kuliko tiba!!
 
Back
Top Bottom