Jeshi la majini kazi yake ni ipi? kwanini hawakuenda kuokoa mwanza??

Jeshi la majini kazi yake ni ipi? kwanini hawakuenda kuokoa mwanza??

Kwamba wewe ndiye unajua zaidi kuliko viongozi wa Jeshi, maana andiko limejaa shutuma tu!

Naamini kwa sasa utakuwa umepata taarifa JWT, Kikosi cha Wanamaji, ndicho kinafanya kazi hiyo. Hili ni baada ya kuandaa taritibu husika ili kazi ifanyike kwa umakini.

Tujifunze kuwa na subira katika mawazo yetu kabla ya kuyatoa nje ya vichwa vyetu.
wasubiri utaratibu wakati watu wanaendelea kufa khah......nn maana ya dharura sasa du...........unatetea uzembe da
 
Jamaa aliyapanda ndege kwenda Bondeni kwa Madiba kuazima wazamiaji kufuatia MV BK kuzama atakuwa na majibu sahihi japo kuna watu walimlaumu kwa kwenda Sauzi
nipe dondooo kidogo maana niliwahi sikia interview moja na wale waokozi wa kibongo wakiwashutumu wale wa bondeni kuwa hawakuweza kufanya kitu zaidi wabongo ndo kutoa watu ila wao walishindwa kutokana na lile vumbi chini ya ziwa
 
Hii inapatana akili maana kuna maswali mengi sana ya kujiuliza katika hili tukio... Design kama titanic hivi..

Huenda captain mkuu alijua kitakachotokea akaamua kubaki nchi kavu na kumpa deiwaka?

Wakati deiwaka anaongea na simu, alikua anaongea nini na alikua anaongea na nani?
lakini mkuu i issue haikuzama kisa deiwaka alikuwa anaongea na simu ila ile haraka yetu yakutaka kushuka mapema kuwahi daladala na mwendo kasi hasa kwa wale wa hapa kwetu , nadhani itakuwa vilevile kwa ndugu zetu
 
katika nchi yetu kuna mgawanyo wa majeshi yetu. kuna jeshi la anga, la nchi kavu na jeshi la majini.

hiki kikosi maalumu cha majini makao makuu yake kipo kigamboni hapa Dar es salaam.

hivi kazi yake hiki kikosi ni kupigana vita ya kumwokoa nani au kumlinda nani kama kwenye ajali za majini hawawezi kufanya uokoaji??

sitaki kuamin kwamba hawa hawana vifaa. yaan nawafaham vizur wana kila aina ya vifaa vya majini. iwe usiku mvua jua wako tayari muda wote kukabiliana ndani ya maji. imekuaje tuko kimya kuhoji kazi ya kikosi hiki??

kazi ya jeshi sio kuchimba makabuli . kazi yao kubwa kuokoa, kukomboa, kulinda, kurejesha palipo bomoka. tumeona mara kadhaa wakijenga usiku na mchana madaraja.

yaan katika hili nitahoji kila nitakupopata nafasi ya kuliongelea. sitak kuongelea sijui ya waziri mkuu na mfuko wake wa majanga. hawa huwa siwajadili maana wamejaa bla bla tu. sitak kuamini na jeshi liingie kwenye utendaji wa wanasiasa. wao wakisikia sehem kimenuka wanapaswa kuamsha popo na sio kusubiri hawa wanasiasa.

angalizo kwa wale wanaodhan muda ulikua sio rafiki. yaan jeshi letu lina ndege za kivita. kufika mwanza hata dak 40 wanaweza kufika. kama wataalam wangekua hapa dar wangeweza kufika mwanza hata kuwazid walio hapo mwanza lakn wanatumia magari kutoka wilayani. ila ni kwamba inaonekana kazi ya jeshi ni kurusha ndege kututisha tukitaka kuandamana na siku ya uhuru. yaan napata hasira nikifikiria. sijui nani katuloga!!!
Kwani jeshi la ardhini huokoa kwenye ajali za mabasi? Be careful with your flawed logic. Pia jifunze namna vifaa vya kijeshi vinavyotumika kuliko kutoa maangalizo yasiyo na kichwa wala mguu. Unajua ndege ya kivita ina uwezo wa kubeba watu wangapi? Je, anayepanda ndege hiyo anatakiwa awe na vigezo gani? Kuchamba kwingi kuondoka na mavi!!
 
Binafsi huu msiba umenifanya nijiulize maswali mengi sana juu ya Serikali. Eti Mkuu wa Mkoa anatangazia Umma wamestisha uokoaji sababu giza kimeingua. Really [emoji24][emoji24] Nadhani kwenye list ya wanaotakiwa kuondoka huyu naye anastahili. Wavuvi wanawezaje kuokoa watu arobaini Serikali ikaokoa mmoja. What a Shame!!
Aiseeee,unaweza kumuumiza mtu kwa hasira unajua,.kuna vingine vinafanywa na serikali hii mbuzi hata kwenye giza nene lakini kwenye kuokoa maisha ya watu hawawezi sababu ya giza seriously,?!manyoko zao mfyuuuuuu😏😏
 
Hii inaleta walakini pale itakapotokea tukavamiwa na vikosi vya adui zetu kupitia njia ya majini,tutakwisha.

Eti giza,are we serious?Wananchi tujilinde wenyewe wallah dhidi ya majanga yoyote yale.
Mkuu umenena.
 
kweli mkuu ila hata ka taa zilikuwa dar zingeweza kusafirishwa kwa ndege hata ya kukodi au helkopta maana ni maisha tunaoko, tena ya watu na si mtu mmoja,ila kunauzembe toka kutokea kwa ajali mpaka wokozi, mtu aliyesema zoezi limesitishwa ingelikuwa ni uwezo wangu ningeanza nae ka mfano kwa wengine ili wawe wanajiongeza
Nikweli mkuu ila sidhani Kama tuna hizo taa za kumulika chini ya maji
 
Sidhani ka wale wapo kwa ajili ya uokoaji.... Hi Kazi ilibidi ifanywe na fire wao ndo wahusika 100% Hawa wengine tunawaonea unless Kama waliombwa MSAADA wakazembea.....
 
Hivi Navy ndio kile kikosi cha wavunjiana tofali sio!! Mi kidhungu mwenzenu sijui.
 
Sidhani ka wale wapo kwa ajili ya uokoaji.... Hi Kazi ilibidi ifanywe na fire wao ndo wahusika 100% Hawa wengine tunawaonea unless Kama waliombwa MSAADA wakazembea.....
Acha kupotosha umma mkuu hivi mbaka leo hujui kuwa hao wavunja tofari(jwtz) jukumu lao kushiriki kwenye majanga.
 
Labda tupate mtu atuainishie majukumu halisi ya JWTZ.... Kabla ya kufika huko je majukumu ya jeshi la zimamoto na uokoaji n yapi??? Niyupi anaepaswa kuwa na vifaaa vya uokozi Kati ya JWTZ na zimamoto??? Jeshi la wananchi nadhani wanaombwa pale inapohitajika na Kama sikosei walikuepo au shida ilikua kuwaona watu wa navy??? Je nn tofauti Kati ya mwanajeshi kitengo Cha maji na mzamiaji (diver)?
 
Acha kupotosha umma mkuu hivi mbaka leo hujui kuwa hao wavunja tofari(jwtz) jukumu lao kushiriki kwenye majanga.
Je walishiriki au hawakushiriki????
 
Kwamba wewe ndiye unajua zaidi kuliko viongozi wa Jeshi, maana andiko limejaa shutuma tu!

Naamini kwa sasa utakuwa umepata taarifa JWT, Kikosi cha Wanamaji, ndicho kinafanya kazi hiyo. Hili ni baada ya kuandaa taritibu husika ili kazi ifanyike kwa umakini.

Tujifunze kuwa na subira katika mawazo yetu kabla ya kuyatoa nje ya vichwa vyetu.
Subira wakati watu wanakufa shwain kabsa wewe
 
lakini mkuu i issue haikuzama kisa deiwaka alikuwa anaongea na simu ila ile haraka yetu yakutaka kushuka mapema kuwahi daladala na mwendo kasi hasa kwa wale wa hapa kwetu , nadhani itakuwa vilevile kwa ndugu zetu
Hebu nenda youtube katafute interview za waliosalimika utasikia wanasemaje.
 
Kafara za kila muhula wa raisi
Nimeanza kufuatilia ziara za jiwe Nimeshtuka, katoka ziara lake zone kivuko kimeua, kule Singida askari wetu walipata ajali kwenye ziara yake wakafa Manyoni ,kule Mara Chupuchupu watu wafe.
 
Kwamba wewe ndiye unajua zaidi kuliko viongozi wa Jeshi, maana andiko limejaa shutuma tu!

Naamini kwa sasa utakuwa umepata taarifa JWT, Kikosi cha Wanamaji, ndicho kinafanya kazi hiyo. Hili ni baada ya kuandaa taritibu husika ili kazi ifanyike kwa umakini.

Tujifunze kuwa na subira katika mawazo yetu kabla ya kuyatoa nje ya vichwa vyetu.
Acha kutokujielewa mtoa maana upo sahihi sana
 
Jiwee uchawii hakosiii kabisaa...!! Yani alikubalii kabisaa Uokoaji usitishwee kisaa Gizaa??? Kwenda kuokoa watu mpaka kamati ikaee mama....eee yulee mzee uchawii hakosiii
 
Back
Top Bottom