Jeshi la Polisi: Aliyedaiwa Kutekwa aliuza gari alilokodi Ili kulipa madeni ya harusi.Uchunguzi unaendelea kubaini Alikopotelea

Jeshi la Polisi: Aliyedaiwa Kutekwa aliuza gari alilokodi Ili kulipa madeni ya harusi.Uchunguzi unaendelea kubaini Alikopotelea

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Jeshi la Polisi limetoa ushahidi wa awali kuhusu kupitea Kwa bwana harasi mara baada ya kumaliza harusi.

Polisi wanadai ushahidi wa awali unaonesha bwana Masawe aliyepotea Aliuza gari aliyokodi Ili Kulipa Madeni na kwamba Polisi wanaendelea kukusanya taarifa Ili Kubaini kama bwana Masawe alijipoteza au ikoje.

Polisi wanadai taarifa zaidi zitatolewa.👇👇

View: https://x.com/millardayo/status/1868976028665663785?t=h7Pm-jybGVTfa2j6gCB6ig&s=19

Ni utata, ndivyo unavyoweza kueleza kuhusu taarifa za kupotea bwana harusi, Peter Masawe ambaye Jeshi la Polisi linaeleza uchunguzi wa awali umebaini alikuwa na madeni na ameuza mali za watu.

Mbali ya taarifa ya Polisi, baadhi ya marafiki wa Masawe anayejulikana zaidi kwa jina la Vincent, wanaeleza wakionyesha wasiwasi kutokana na mzunguko waliotumia walipomtafuta tangu alipopotea.

Victor Mawalla, akizungumza na Mwananchi leo Desemba 15, 2024 amesema alipigiwa simu na Vincent ambaye ni rafiki yake akamweleza alikuwa Mbezi na kuna magari mawili yanamfuatilia, moja alilitaja ni Toyota Land Cruiser (Hardtop).

Amesema alimpatia ushauri aingie kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa taarifa.

"Nilivyomwambia hivyo alikubali akinitajia namba za gari lililokuwa likimfuatilia lakini baada ya kufuatilia ikabainika gari alilolitaja limepaki eneo la Ilala," amesema Mawalla.

Amesema baada ya kufuatilia Jeshi la Polisi lilikamata gari na mmiliki ambaye alifika Dar es Salaam akitokea Kahama mkoani Shinyanga kwa ajili ya manunuzi ya vifaa vya magari ambaye alikuwa hafahamu chochote kuhusu kinachoendelea.

Kutokana na taarifa iliyokuwa imetolewa kwenye mitandao juu ya kupotea kwa bwana harusi Jeshi la polisi limetolea taarifa

na taarifa inathibitisha kuwa bwana harusi huyo aliuza gari alilokodi kwa ajili ya harusi huku akimtumia mkewe pesa nyingine apunguze madeni .

My Take
Polisi tunaomba Haki itendeke Kwa matukio yote Ili kuondoa hofu na mashaka kwenye jamii.

Mambo ya kutekana hayafai.
Screenshot 2024-12-15 171340.png



Updates
Kumbe Jamaa alijiteka Ili kukimbia madeni ,akutwa amejificha Pemba 😂😂👇👇

View: https://www.instagram.com/p/DDra5I2sPGp/?igsh=NjhwcndpZ3F0OGJ0
 
Polisi wanaendelea na uchunguzi kufahamu kama Mtu aitwae Vincent Peter Massawe wa DSM amejipoteza mwenyewe kwa makusudi ama la, ikiwa ni siku kadhaa toka Ndugu zake watangaze kupotea kwake.

Taarifa ya Polisi imesema Jeshi hilo lilipokea taarifa za kupotea kwa Vincent siku chache baada ya harusi yake ambapo imebainika amekuwa akidaiwa zaidi ya Tsh. milioni 65 na Watu tofauti, hivyo wanachunguza kama amepotea kweli au amejipoteza sababu ya madeni.

“Kufuatia taarifa hii inayosambazwa katika Mitandao ya Kijamil, Jeshi la Polisi lingependa kutoa ufafanuzi kulingana na ushahidi uliokusanywa kupitia kwa Watu mbalimbali na kupitia uchunguzi wa kisayansi uliokwisha fanyika hadi sasa, ni kweli taarifa za kupotea kwa Vincent Peter Massawe zilifikishwa Kituo cha Polisi Kigamboni Noveember 19,2024 na Mke wake” - Polisi.

“Upelelezi ulianza mara moja na kuthibitisha kuwa ni kweli alikuwa na harusi November 16,2024 na baada ya harusi alitafuta gari ya kuwarejesha Ndugu zake na Wageni wengine Moshi Mkoani Kilimanjaro, ushahidi mwingine uliopatikana ni kwamba wakati wa maandalizi aliazima gari ( T 642 EGU Toyota Ractis) kutoka kwa Jamaa yake ili imsaidie katika shughuli za harusi lakini hakulirejesha gari hiyo kwa Mwenyewe na badala yake November 18,2024 ambayo inadaiwa alikuwa anafuatiliwa na gari ambayo alikuwa anaitilia mashaka ndiyo siku hiyohiyo aliuza gari hiyo kwa kiasi cha shilingi milioni 9 na akalipwa milioni 8 ikabaki milioni moja “

“Taarifa iliyopo inaonyesha kuwa siku hiyohiyo alimtumia Mke wake kiasi cha fedha ili alipe madeni mengine yaliyotokana na harusi ikiwepo Coaster aliyokodisha kuwarejesha Wageni wake Moshi, gari hilo aina ya Toyota Ractis limefuatiliwa na limekamtwa, ushahidi mwingine unaonyesha huyu Vincent Peter Massawe pia anadaiwa na Watu wengine wawili mmoja kiasi cha milioni 53 na mwingine milioni 16, ukweli wa tukio hili utafahamika muda si mrefu kama amejipoteza au laah kulingana na mtiririko wa ushahidi ulivyo na hili linategemea hasa tukipata ukweli kutoka kwa Mke wake kwani inadaiwa anao ufahamu mkubwa wa jambo hili, mwisho Umma utajulishwa taarifa zilizo sahihi kuhusu Peter Masawe” ——— Polisi.
 

Attachments

  • 1734277710270.jpg
    1734277710270.jpg
    264 KB · Views: 2
Back
Top Bottom