DolphinT
JF-Expert Member
- Mar 9, 2016
- 2,014
- 2,979
Kwanini isiwe kesi ya kuiba gariNaam nakubaliana na wewe.
Umeona polisi wakieleza kupokea taarifa au malalamiko kutoka kwa mmiliki kwamba kuna mteja amekiuka Makubaliano ya mkataba na gari yake hairejeshwi?
Uhai au Hali ya gari ya harusi au shughuli ya harusi unadhani ni rahisi kuiuza Kwa ajili kukata scraper?
Unapokodi gari dereva unakua wewe bwana harusi au unakabidhiwa dereva? Je dereva Yuko wapi kama ni hivyo?
Ina maana alipata wapi fedha ya kukodi gari kama alikua Bado ana madeni ya harusi? Kwanini useme hivyo wewe kuwa ilikua ni Kwa ajili ya scrap na sio vinginevyo?.
Turudi nyuma, Polisi alawli wanasema ilisalia milioni Moja Ili mnunuzi akabidhiwe gari, hapo hapo wanasema gari imekamatwa Kwa mnunuzi! Swali fukirishi zaidi kwako umewahi Kununua au kuuza gari Kwa mtu, kama hapana kaulize utaratibu wa kuuziana gari, sio kama unauziana mbuzi au kuku!
Je mkodishaji alikodisha gari na documents halisi zote?