AbaMukulu
JF-Expert Member
- Jan 1, 2018
- 2,053
- 3,586
Naamini IGP Sirro anakaribia kustaafu utumishi wake kwenye jeshi la polisi uliodumu kwa zaidi ya miaka 30. Japo amefanya mengi lakini yapo ambayo bado ananyyoshewa kidole kwayo. Japo ni mengi lakini naomba niwasilishe swala hili moja tuu kwa leo. JESHI LA POLISI CHINI YA SIRRO limeshindwa kuwaweka hadharani wauaji wa kijana Yusufu Deus. Kama ambavyo iliripotiwa kabla ya kifo chake kwamba kijana huyu alitekwa kwanza na watu ambao jeshi la polisi linasema hawajafahamika. Baadae alikuja kuachiwa na watekaji hao rejea mahubiri ya mchungaji eliona kimaro.
www.mwananchi.co.tz
Video ya mchungaji eliona Kimaro akielezea tukio hilo
Baada ya kurejeshwa alikuja tena kupatikana akiwa ametegeshwa kama mtu aliejinyonga katika eneo lake la biashara. Kwa mazingira yale ya sehemu alipojinyongea inaonyesha dhahiri aliuliwa sehemu nyingine na mwili wake kuletwa pale. Wauaji wakaufunga kamba shingoni lakini miguu ikiwa inagusa chini kabisa.
Kwa nini ninalilaumu jeshi la polisi chini ya Sirro kwa kushindwa kuwaweka hadharani wauaji wa kijana Deus Yusufu?
Tukirejea wakati marehemu Deus yusuf ametekwa, watekaji waliacha alama za kimawasiliano kati yao na ndugu wa marehemu. Watekaji hao walikuwa wanawasiliana na ndugu wa marehemu kuhusu kupewa kiasi cha hela. Ndugu wa marehemu alionyesha mawasiliano hayo kwa polisi wa kitengo cha cyber pale Mabatini. Askari huyo anaitwa John. Askari huyu na wengine hawakuonyesha ushirikiano licha ya ndugu wa marehemu kuwaonyesha sms ambazo alikuwa anachati na watekaji hao. Askari Polisi walimwambia ndugu wa marehemu aende mwenyewe kwenye eneo walilokubaliana na watekaji halafu kitakachotokea awataarifu askari. Hili haliingii akili kabisa kwa walinda amani hawa kuonyesha kutozingatia maadili ya kazi yao.
Unaweza ukasamehe yote hayo baada ya ndugu yako kupatikana. Lakini siku chache baada ya kuachiwa unakutwa mwili wake ukining'inia eneo lake la kazi. Mazingira yote yakionyesha marehemu hakujinyonga mwenyewe. Mauaji yake yalifanyika eneo lingine na ili kupoteza ushahidi mwili ukaletwa pale tuu ili ionekane amejinyonga.
Kama jeshi lilifanya uzembe wakati wa kutekwa kwake basi hapa lisingetakiwa kurudia uzembe wa awali. Hakuna mtekaji wala muuaji hata mmoja aliekamatwa zaidi ya mama ambae walikuwa wanatumia wote sehemu ya biashara. Watekaji licha ya kutumia namba za simu zilizosajiliwa kwa alama za vidole lakini jeshi la polisi limeshindwa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani wauaji.
Miongoni mwa namba iliyotumika na watekaji hao ni 0629004596. Namba hii ilikuwa imesajiliwa kwa jina la ISACKY RAYMOND KILEO. Lakini sasa hivi usajili umebadilishwa kwenda kwa jina la REMIGIUS REMIGIUS HYERA. Jeshi la polisi liapaswa liuambie umma wa Watanzania huyu ISACKY RAYMOND KILEO ameshiriki vipi kwenye tukio hili. Ni uzembe wa hali ya juu na upuuziwaji mkubwa wa maisha ya mtanzania.
Ni vyema IGP ajaye aiitishe uchunguzi mpya kwenye swala hili. Kwanza la mauaji ya kijana huyu na pili uzembe wa watendaji wa jeshi la polisi kwenye kuokoa maisha ya kijana huyu.
Ninaamini kama jeshi la polisi lingeonyesha ushirikiano kwa ndugu basi watekaji hawa wangepatikana na INGEWEZEKANA KUNUSURU MAISHA YA KIJANA YUSUF DEUS.
Mchungaji asimulia utata wa kifo cha muuza chips aliyekutwa amejinyonga
Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Kijitonyama jijini Dare s Salaam, Eliona Kimaro amesimulia kifo cha utata cha muuza chipsi, Yusuf Deus aliyekutwa...