Jeshi la polisi chini ya Sirro limeshindwa kuwaweka hadharani wauaji wa muuza chipsi Yusufu Deus, IGP UJAYE TENDA HAKI.

Jeshi la polisi chini ya Sirro limeshindwa kuwaweka hadharani wauaji wa muuza chipsi Yusufu Deus, IGP UJAYE TENDA HAKI.

Sense of responsibility! Huwezi kuzuia makosa yasifanyike lakini unaweza kuchukua hatua yakifanyika.. Utachukua hatua gani! ? Hilo ndio la nuhimu
Kuhusu Yusuf mchungaji Kimaro alishatolea ufafanuzi Kanisani na kwamba polisi walitimiza wajibu wao kikamilifu!
 
Watanzania na sisi sijui nani katuloga yani tunakaa kimyaa mpaka yatupate. Maana leo kwa yusuph kesho hatujui kwa nani.

Polisi yenyewe ndo hao wanaua raia na kupora hela.
Na kesi ya Mtwara polisi watakuwa huru. Sio kwa sababu hawana hatia bali mfumo wa HAKI umeoza
 
Kuhusu Yusuf mchungaji Kimaro alishatolea ufafanuzi Kanisani na kwamba polisi walitimiza wajibu wao kikamilifu!
Wajibu pekee ni wauaji kufikishwa mbele ya mahakama. Kama una rejea ya kesi hii kufikishwa mahakamani weka hapa jukwaani ndugu
 
Kila nchi kuna changamoto kama hizo na hakuna aliyejiuzulu kwakua kujiuzulu siyo suluhisho bali ni kuendelea na uchunguzi.
Siamini kama TPF wamefanya uchunguzi mpaka mwisho bali bado unaendelea.
Ugoro huuu umeandika hapa...
 
Kuhusu Yusuf mchungaji Kimaro alishatolea ufafanuzi Kanisani na kwamba polisi walitimiza wajibu wao kikamilifu!
Januari Mosi 2021 aliyekuwa RPC DSM Mambosasa alisema wanafanya uchunguzi na watautaarifu umma. Leta mrejesho wa umma kutaarifiwa kuhusu tukio hili.

Kuendelea na uchunguzi imekuwa ndio funika kombe kwa jeshi la polisi.
 
Inasikitisha sana ingekua wizi wa simu wangefuatilia ili wapige hela hapa waliona hmna masilahi aibu kwao polisi poleni familia.
 
Shida ya Polisi wetu, mtu ukipata Tatizo ukaripoti kwao, wanakugeuza Mtaji..

Ili upate Haki yako kupitia Jeshi la Polisi ni lazima ulipe Pesa nyingi sana..
 
Kuwajibika kupi unakomaanisha manake matukio ambayo watuhumiwa wanapatikana ni mengi sana kulingana na yale ambayo bado yapo chini ya uchaguzi.
Mengi kati ya hayo ni ya michongo .. Nimefanya kazi nao kwa karibu karibia miaka 20 najua ndani nje nini kinaendelea huko
 
Back
Top Bottom