Jeshi la Polisi: Hakuna ushahidi kuwa Freeman Mbowe alishambuliwa. Alikuwa ametoka kwa Joyce Mukya. Alikuwa amelewa chakari


Kwa maelezo ya polisi kutoka kwa mbowe ni kwamba, mbowe alivamiwa na akapiga kelele kutaka msaada, je kijana wake hakusikia?
Ni kwa nini alienda kwanza kwa joyce mukya badala ya kwenda hospital au police?
Na kwa nini hakumjulisha kijana wake kabla ya kwenda kwa mkya au hospitali?

Je hizo kelele alizopiga kuomba msaada zilikuwa za kiwango cha chini au vipi na kwa nini hazikusikia?
Na ni kwa nini hakuwajulisha majirani badala yake akaona joyce ndo jirani, je hawa anaoishi nao hawana maelewano mazuri?
Je mbowe anajibagua na majirani zake?
Majibu hayo pengine Salary Slip amsaidie mbowe kujibu kwani yeye nado ni mgonjwa.
 
Ndugai na wabunge wa CCM walikosea sana kuzungumzia hili suala huku wakijua fika uchunguzi wa polisi ulikuwa ukiendelea, wanajisahau na kuingiza siasa hata kwenye mambo ya msingi.
 
Nilifikiri wanaleta kilichojiri A to Z ili kuwa umbua polisi kumbe nao wameleta ngonjera...
 
Umemgusa.
 
Na wakishindwa kuwaumbua hakika wataumbuka wao
 
Mkuu tusipende kuwalaumu polisi kwa kila kitu. Linapotokea tukio kisheria lazima polisi waende eneo la tukio. Na moja ya mambo wanayoyakiwa kuhoji ni pamoja na kuhoji wakazi eneo jirani na tukio.

Sasa kama victim anasema alipiga makelele wakati anakanyagwa na komandoo Mashimo,alafu hamna mtu aliyesikia? Polisi waseme nini?
Typing error ya Nkya na Mukya sio sababu ya kuwalaumu pia.

Najua kuna matukio mengi huwa wanafanya uzembe. Lakini kwa hili hata mimi nina mashaka sana. The Chairman was drunk.
 
Katibu Mkuu Taifa Bwana John Mnyika alisema kwenye press conference yake ya pili kwamba Mbowe Hakuwa peke yake!

Huyo mtu mwingine ni nani? Aidha James Mbowe alikua ndani ila Bi Nkya ndio alipewa taarifa kwanza kabla ya mtu aliyekuwepo mita 10? Alipiga kelele kuomba msaada inawezekana James alikua anaangalia TV au amelala hivyo hakusikia kelele hizo?

Unajua kinachoonekana hapa si polisi kuwa upande wa Spika kama wana CHADEMA wanavyodai bali ni technicalities za uchunguzi ndio zilizopelekea matokeo hayo.

MIMI NINAVYOIONA HII KESI
60-70% inaonekana Mbowe ameipika hii kesi sema mapishi kidogo yalitiwa chumvi nyingi hasa hiki sehemu hizi mbili;

1. Kurudi nyumbani saa 7 usiku
2. Kuonekana Royal Village
3. Kwenda kumtembelea Mzazi Mwenzie?

30% inawezekana kweli ameshambuliwa japo hata hiyo nayo ina walakini kutokana na ushahidi wa upande mmoja tu!
 
Unachokisubiri ndo wengi tunakisubiria pia maana Polisi ni Kama wamekusanya taarifa za kina Lijualikalki na Spika na kuziweka katika samary. Hakuna kipya walicholeta na wengi tulitegemea iwe hivyo maana siku hizi hivi vyombo vinafanya kazi kwa kuangalia upepo ukoje

Ilikuwa vigumu polisi wawe tofauti na bunge

Hata hivyo, chadema wakibugi tu na kushindwa kutoa maelezo ya kina yanayoeleweka na yenye ushawishi wa kufuta haya yanayosemwa, hakika wataumbuka
 
Wanacho fanya Sasa chadema ni kuweweseka,kwa aibu hii aliyoifanya mbowe sio kuleta utoto na kuja na majibu mepesi Kama haya
 
Mkuu, mda si mrefu umesema CHADEMA wamewatega Polisi na sasa wanaenda kumwaga mboga, lakini ukisoma hilo tamko utaona ni la kitoto kabisa na hakuna hoja yoyote.

Kaeni kimya kama hakuna la maana
Ni kama mfamaji haachi kutapata,ndio Hali walio nao chadema kwa Sasa hii aibu Ni kubwa sana
 
Swali la Fatma wakili msomi na mtoto wa CCM asilia asiye na hizo njaa za kina Ndugai linahitaji majibu sahihi.
 
Akikujibu nitag
 
Hata sisi tulijua mnataka Mbowe afanane na Lissu ili muwarubuni wajumbe wa mkutano Mkuu . haya mwambieni nae akachukue fomu ya Urais. Au kashaandika barua ya kutia nia kimya kimya? Maana leo ni tarehe 12June 2020
Wewe ulikwapua hela Chadema ukakimbilia CCM lakini wamekupotezea wewe jikite tu kwenye biashara yako ya mama lishe na bar bubu huteuliwi ng'o
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…