Nazgur
JF-Expert Member
- Apr 19, 2020
- 3,729
- 2,851
"Tulikuwa na shaka kuanzia siku ya kwanza juu ya Polisi kutumika kupotosha ukweli kuhusu tukio la Mwenyekiti Freeamn Mbowe. Mashaka hayo yamedhihirika kwa kutekeleza maelekezo aliyotoa Spika Ndugai kwao Bungeni kwa kusema uongo uleule uliosemwa na CCM Bungeni," Jon Mrema
"Kama ilivyokuwa tukio la kushambuliwa Tundu Lissu "hadi tukataka wachunguzi wa kimataifa, wamerudia tena utaratibu huo wa kusema uongo. Imekuwa ni kawaida yao kuficha ukweli na kuzusha mambo kama walivyofanya kwa mauaji ya Mwanahabari Daud Mwangosi na Aqulina Aquline "Jon Mrema
"Tunalitaka jeshi la polisi lifanye majukumu yake kwa weledi na sio kujiingiza kwenye propaganda za kisiasa ambazo zitalifanya lisiaminike kwa wananchi.l," Mkurugenzi wa Uenezi, Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje
Kwa maelezo ya polisi kutoka kwa mbowe ni kwamba, mbowe alivamiwa na akapiga kelele kutaka msaada, je kijana wake hakusikia?
Ni kwa nini alienda kwanza kwa joyce mukya badala ya kwenda hospital au police?
Na kwa nini hakumjulisha kijana wake kabla ya kwenda kwa mkya au hospitali?
Je hizo kelele alizopiga kuomba msaada zilikuwa za kiwango cha chini au vipi na kwa nini hazikusikia?
Na ni kwa nini hakuwajulisha majirani badala yake akaona joyce ndo jirani, je hawa anaoishi nao hawana maelewano mazuri?
Je mbowe anajibagua na majirani zake?
Majibu hayo pengine Salary Slip amsaidie mbowe kujibu kwani yeye nado ni mgonjwa.