Tulimsikia wenyewe, Kamanda wa Polisi wa Dodoma, Gilles Muroto, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, tarehe 9/6/2020, akieleza tukio la kushambuliwa Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Kiongozi wa kambi rasmi bungeni. Freeman Mbowe, kuwa taarifa waliyo nayo wao Polisi ni kuwa watu wasiojulikana wamemvamia na kumkanyaga kanyaga Mheshimiwa Mbowe na kusababisha avunjike mguu wake wa kulia, hata hivyo RPC huyo alieleza kuwa taarifa aliyotoa ni ya awali na Jeshi lake linaendelea na uchunguzi wake na akatoa onyo Kali sana kwa wanasiasa kutotumia tukio hilo kujinufaisha kisiasa.
Lakini cha ajabu, siku hiyo hiyo ya tarehe 9/6/2020 tukashuhudia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Spika Ndugai, wakiligeuza Bunge hilo kama kikao cha CCM, kwa wabunge wake, akiwemo Msukuma, Lusinde, na wengine waliotoka Chadema, na kujiumnga na CCM, akina Silinde na Lijualikali, wakitoa maelezo yanayofanana kuwa Mbowe alilewa chakari na alirudi usiku wa manane nyumbani kwake na ndicho kilichosababisha aanguke kwenye ngazi na kuvunjika mguu wake wa kulia.
Hata hivyo jambo lililotushangaza sana watanzania ni ripoti iliyotolewa Jana na Jeshi hilo la Polisi, wakidai kuwa wameshakamilisha upelelezi wao
Katika ripoti yao iliyoitoa Jeshi hilo la Polisi mkoani Dodoma, kupitia msemaji wake, Daniel Misime, ambayo inaonyesha imeshabihiana sana na vile vijembe vilivyotolewa na wabunge wa CCM kuwa, Mwenyekiti huyo wa Chadema, Freeman Mbowe, alikuwa amelewa chakari na ndicho kilichosababisha aanguke na kuvunjila mguu wakati anapanda ngazi!
Nina mwaswali machache kwa Jeshi letu la Polisi nchini
1. Jeshi la Polisi kupitia msemaji wake mkuu, RPC Gilles Muroto katika taarifa yake ya swali ilikiri kuwa Freeman Mbowe alivamiwa na watu wasiojulikana na kumshambulia Mbowe kwa kumkanyaga kanyaga hadi kusababisha kumvinja mguu, ni kwanini taarifa aliyotoa RPC Gilles Muroto itofautoane sana na taarifa iliyotolea Jana na msemaji wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Daniel Misime?
2. Wakati akitoa taarifa ya awali, RPC wa Dodoma, Gilles Muroto alitoa onyo Kali kwa wanasiasa kutoingilia upelelezi huo wa Polisi. Hata hivyo sijawahi kusikia Jeshi hilo likitoa onyo kwa wabunge wa CCM walioamua kukaidi katazo hilo. Je ni kwanini Jeshi la Polisi halijatoa onyo Kali kwa wabunge wa CCM waliokaidi agizo lao?
3. Kama Jeshi letu la Polisi limechukua siku chache sana kukamilisha upelelezi wao kwa tukio la ku kshambuliwa Mbowe, tena bila ya kupata Maelezo ya Mbowe mwenyewe, ni kwanini tukio la kupigwa risasi mbunge wa Chadema, Tundu Lissu, ambaye alipigwa risasi tarehe 7/9/2017 limechukua muda mrefu sana kutokamilika, ikitoa visingizio kuwa, mhusika mkuu, ambaye ni Tundu Lissu kwa kuwa hayupo nchini na "main witness" mwingine ambaye ni dereva, kwa kuwa hawapo nchini, kwa hiyo Jeshi la Polisi limeshindwa kikamilisha upelelezi wao. Ni kwanini Jeshi letu la Polisi linakuwa na "double standards" katika upelelezi wao?
4. Tunajua kuwa mahali aliposhambuliwa Mwenyekiti Freeman Mbowe Kuna CCTV cameras, je ni kwanini Jeshi letu la Polisi halijazitumia CCYV cameras hizo katika kikamilisha upelelezi wao?
5.Kama Jeshi la Polisi kwa mujibu wa Katiba yetu linatakiwa lisijiingize kwenye sasa, tunaweza endelea kuliamini vipi, wakati vitendo vyake, ni dhahiri vinaonyesha dhahiri, limeegemea upande wa CCM?
Hivi kama sisi wananchi "tuki-conclude" na kuamini kuwa Jeshi letu la Polisi nchini limejiingiza kwenye siasa na kufanya "coalition" na CCM tutakuwa tumekosea kweli?
Ningependa Jeshi letu la Polisi nchini linijibie maswali yangu hayo machache, yenye lengo la.kuleta maslahi mapana kwa Taifa letu