Jeshi la Polisi: Hakuna ushahidi kuwa Freeman Mbowe alishambuliwa. Alikuwa ametoka kwa Joyce Mukya. Alikuwa amelewa chakari

Usiingilie uhuru wa watu kutoa maoni yao. Ni kinyume cha katiba ya JMT. Umetumwa na Bakita kuangalia maudhui humu JF?

Nasema hivi, watu huwa wanasema eti kuna watu wana id zaidi ya moja, mimi nasema haiwezekani kuwa na zaidi ya moja na zote zikawa zinachangia, maana maudhui yatakuwa ni yale yale. Hapa hatutaandikia mate, ngoja niangalie hii na ile zitachangia vipi hapa jukwaani. Hakuna anayekuzuia kuchangia, ila utajua kuwa sisi wengine ni next level.
 
Kwa hiyo ulitaka waseme kapigwa hata hajapigwa. Kama unahakika kapigwa unaweza kuthibitishia umma pia. Maana hao majirani hawawezi kudanganya.

Majirani hawawezi kudanganya? Unajua unachosema?
 
Ripoti ya polisi imeandikwa kwa kujenga dhaba ya kumchafua Mbowe. Bila kujali nafasi yake katika jamii mtu mzima mwenye familia ripoti ile ni kama inamuongelea kibaka.
Kwa Mambo ya kijinga aliyofanya anatofauti gani na kibaka? Mbowe kaanguka hakumwambia mwanae anayeishi nae katika hiyo nyumba kaenda kumpa taarifa Joyce.
Mwambieni anahitajika na TAKUKURU msiie sema anaonewa maana wanahojiwa wabunge 69.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nasema hivi, watu huwa wanasema eti kuna watu wana id zaidi ya moja, mimi nasema haiwezekani kuwa na zaidi ya moja na zote zikawa zinachangia, maana maudhui yatakuwa ni yale yale. Hapa hatutaandikia mate, ngoja niangalie hii na ile zitachangia vipi hapa jukwaani. Hakuna anayekuzuia kuchangia, ila utajua kuwa sisi wengine ni next level.
Ahaaaaa. Nacheka sina mbavu. Yaani maana na maudhui yanafanana na ya Idugunde kwa kila mada. Au una tafuta nini? Maana hoja ni Polisi kutumia Cctv camera footage badala ya watu. Jaribu kujikita kwenye mada. Japokuwa najua mwenyekiti amewakatisha tamaa.
 
Majirani hawawezi kudanganya? Unajua unachosema?
Kwa mujibu wa polisi majirani hawakusikia kelele za mtu kuomba msaada wakati anakanyagwakanyagwa. Victim anasema akipiga mayowe na kelele kuomba msaada. Kwa hiyo majirani wanasema uongo?
 
Ahaaaaa. Nacheka sina mbavu. Yaani maana na maudhui yanafanana na ya Idugunde kwa kila mada. Au una tafuta nini? Maana hoja ni Polisi kutumia Cctv camera footage badala ya watu. Jaribu kujikita kwenye mada. Japokuwa najua mwenyekiti amewakatisha tamaa.

Hakuna uwezekano id zote ziishie na Nde na maudhui yafanane kisha wawe ni wamiliki tofauti. Ngoja nionywe tu mtori nyama nitazikuta chini.
 
Polisi Kigango cha propaganda cha chama tawala. Ulimwona yule kanda aliyevaa magwanda ya jeshi zetu alivyofurahia umbea wake?
 
Kwa mujibu wa polisi majirani hawakusikia kelele za mtu kuomba msaada wakati anakanyagwakanyagwa. Victim anasema akipiga mayowe na kelele kuomba msaada. Kwa hiyo majirani wanasema uongo?

Nasema hivi ushahidi wote upo ndani ya CCTV camera maana hizo haziogopi polisi, usalama wa taifa wala nini. Hizo zinaonyesha kilichotokea kwa uhalisia wake. Kisha zikipatikana hizo, kila mmoja kuanzia Mbowe, polisi, Ndugai& co wataanza kuongea ukweli wao kutokana na kile kinachoonekana kwenye footage. Hilo mbona rahisi sana. Hizo CCTV footage hatuzihitaji kwa bahati mbaya, tunajua kiwango cha uongo na uzandiki wa wazi wa taasisi zetu.
 
Jeshi LA polis linapaswa kufanyiwa marekebisho makubwa sana, limekuwa kama kitengo cha chama tawala.
 
Nasema hivi ushahidi wote upo ndani ya CCTV camera maana hizo haziogopi polisi, usalama wa taifa wala nini. Hizo zinaonyesha kilichotokea kwa uhalisia wake. Kisha zikipatikana hizo, kila mmoja kuanzia Mbowe, polisi, Ndugai& co wataanza kuongea ukweli wao kutokana na kile kinachoonekana kwenye footage. Hilo mbona rahisi sana. Hizo CCTV footage hatuzihitaji kwa bahati mbaya, tunajua kiwango cha uongo na uzandiki wa wazi wa taasisi zetu.
Uzuri kama Chadema hawajaridhika na majibu ya polisi. Sababu zipo wanaweza kutumia wanasheria na zikatumika. Ila ushahidi wa binadamu reliable and best evidence.
 
Boss nasema hivi, CCTV footage ndio kila kitu. Hayo mengine ni mbwembwe tu. Hao wanasheria ingekuwa na maana kama kuna ufuataji wa sheria. Tunaujua vizuri utendaji kazi wa polisi, na kiwango duni cha uadilifu uliopo kwenye vyombo vyetu vya dola. Ni hivi, CCTV footage ndio pekee zenye ukweli wote na sio binadamu yoyote.
 
Unataka kuamini ripoti gani zaidi ya hiyo ya polisi au tayari una upelelezi wako na ripoti uliyoiandaa kichwani,Mbowe aseme hakulewa,uchunguzi wa lissu alimkimbiza dereva kuficha ukweli kama huu!
kipara kipya
Kama hoja ya Polisi kutokamilisha upelelezi wa kupigwa risasi Tundu Lissu ni kwa sababu Tundu Lissu pamoja na dereva wake hawapo, ni kwa vipi upelelezi wa tukio la Freeman Mbowe umekamilika, wakati hawajamuhoji Mbowe?
 
Boss nasema hivi, CCTV footage ndio kila kitu. Hayo mengine ni mbwembwe tu. Hao wanasheria ingekuwa na maana kama kuna ufuataji wa sheria. Tunaujua vizuri utendaji kazi wa polisi, na kiwango duni cha uadilifu uliopo kwenye vyombo vyetu vya dola. Ni hivi, CCTV footage ndio pekee zenye ukweli wote na sio binadamu yoyote.
Kwani mkiweka mwanasheria ili Cctv footage zitumike polisi watakataa? Mbona kila kitu mnaogopa?
 
kipara kipya
Kama hoja ya Polisi kutokamilisha upelelezi wa kupigwa risasi Tundu Lissu ni kwa sababu Tundu Lissu pamoja na dereva wake hawapo, ni kwa vipi upelelezi wa tukio la Freeman Mbowe umekamilika, wakati hawajamuhoji Mbowe?
Uchunguzi umeshafungwa hio ndio ripoti ya uchunguzi,Muulize vizuri chairman!
 
Nchi hii haina jeshi. Ina genge la vibaka kwa ajili ya wanasiasa wa chama twawala ambao wote ni vibaka na wahuni tu. Ripoti ile iliabdikwa Lijualikali na Nduguyai
 
Tulia Wewe!!!!
Sisi Ndiyo Tunaojua.
Tutumie Nini, Wapi
 
Just go with a technologies? Bora uwe unaandika kiswahili tu. Alafu kwa akili yako kati ya ushahidi wa binadamu na Cctv video footage upi una nguvu mahakani? Maana Cctv video footage lazima wataalamu waje wathibitishe kitalaamu kama kweli mlevi anadondoka. Binandu mwenye akili timamu ana sense kwa sensory organs na anatoa direct evidence.Kama hawakusikia mtu akishambuliwa Cctv ndio zitarekodi?

Hapa unaanika ujuha wako tu. Kila mahali tunakutana na CCTV na wala hazihitaji utaalamu wowote kuona kilichorekodiwa. Jinsi mnavyokwepa CCTV footage ndio kila kitu kinakuwa wazi. Safari hii hamchomoki. La Lisu mlizungusha lakini ukweli wote unafahamika. Uzuri Mungu ni mkubwa, hili limekuja kuweka wazi kile mnachoficha kwa Lisu. Hizi nyuzi wamejaa polisi na usalama wa taifa, wanajua hapa kwenye CCTV tumeshika pabaya. Uongo wote umefikia mwisho na unyama wote hadharani.
 
Back
Top Bottom