Ndugu wana jamvi habali za asubuhi?
Niingie kwenye mada,
Nionavyo mimi ni kwamba hii ajali ya mhe. Mbowe kwa sasa anaijutia na pengine kwa kuwapa mamlaka vijana wake ambao ni special kutoa na kufanya maamuzi juu ya chama kwa ruhusa yake.
Nasema hivyo kwa sababu gani? Kama mh. Mbowe angekuwa na utambuzi mzuri nadhani asingekubali hiyo ajali ihusishwe kisiasa kwa kuwa ni jambo ambalo lingeripotiwa kawaida lisingempa wakati mgumu kama alionao sasa kujibu hoja nyingi ambazo zisinge kuwapo.
Kulingana na taarifa ya Polisi kuwa alikuwa amelewa chakari na pia Daktari wa Bunge kusema hivyo, inatosha kusema kauli za watu wasiojulikana ziliasisiwa na vijana wake bila kumshirikisha na kujua uzito wa maamuzi yao.
Kwa hiyo baada ya kupata utambuzi tayari mambo yalikuwa yamerushwa hewani kwa hiyo hakuwa na namna.
Wangeripoti kuwa amepata ajali baada ya kuwa anatoka kunywa kinywaji wala pasingekuwa na challenge nyingi kwani hilo ni jambo la kawaida tu.
Nimuombe Mbowe apunguze nguvu ya hawa vijana wake ili kutunza heshima yake na chama chake.
Maaana kwa sasa hata ambaye alikuwa hajui kuwa Mbowe ana mchepuko sasa kajua, na hao mabalozi wake sasa watajua kuwa malalamiko ya wabunge kuombwa mapenzi ni ya ukweli maana tayari kianzio kipo.
Pole sana Mr. F Mbowe.