Tetesi: Jeshi la Polisi kuzuia kikao cha baraza kuu la CUF

Status
Not open for further replies.
Serikali ikimpandikiza msaliti nawe wataka kila mtu afuate ETI ndio ufumbuzi. Wachekesha sana. Tz iliyozisaidia nchi zote kusini mwa Afrika kukataa ukoloni, ukaburu, ukandamizaji na vibaraka akina Muzorewa, Sithole, Urio Simango, Jonas Savimbi etc; ETI leo yashauriwa na Mtz iyakumbatie yaleyale. Nadhani kuna tatizo kubwa laja hapa NCHINI kwetu. Mungu tusaidie. AMEN.
 
Jana Lipumba ALIWAAGIZA police sio tu wazuie mkutano huo, bali wamkamate yule ati "aliyejipachika" cheo cha naibu katibu mkuu wa Chama. Lipumba nae siku hizi anaact kama DC flani hivi. Imebaki tu sasa na yeye aanze kutoa maagizo ya kukamata na kumweka mtu ndani kwa 48 hrs. Kwa press conf yake ya jana, ni kama vile yupo anamlia timing maalim Seif. Atawakomesha huyu kiumbe.
 
Kuna njia Nyingi mbona wanaweza kufanya teleconference na kila kitu kikakaa sawa.
Mkuu nimewaza kama wewe aisee. Kila siku maofsini tunafanya video conference sasa si wajipange tu tuone kama hao policcm wataweza kuvuruga na huko.
 
Matendo haya nayo yako katika orodha ya mambo yanayosababisha ugaidi!
 
Mwenyekiti wa CUF si ni Ibrahim H. Lipumba? hakuna kibaya hapo kama hawakumshirikisha kufanya hicho kikao. Ni muhimu mamlaka iheshimiwe. Bila kuheshimu mamlaka hakuna maana ya siasa.
Yes. Halafu Makao Makuu si yako Buguruni?
 
BAK hawa viongozi wa Tz ni waswahili na mswahili unafki kwake ni kawaida. Juzi Kikwete kaenda kuwasema wa Kenya eti amani iko mikononi mwa Uhuru na Raila, huku akiwaacha CCM na serikali ikiwaswaga wapinzani wapendavyo. Huyu Kikwete alihakikisha Maalim anadhulumiwa Zanzibar na kukizingira kisiwa hicho kwa mitutu.

Hao wengine unasikia wameshapendekeza katiba ivunjiliwe mbali ili Maghufuli atawale maisha yake yote!! Usitarajie lolote kwao hao wanalishwa pensheni kubwa isiyo na mahesabu.

Cairo's
 
Cuf watangazieni wazanzibari kuteremka mtendeni mkubwa kwa mdogo....kulinda mkutano huo.
Msiligee abadan
Tena Maalim waite waje mtendeni walinde mkutano wao halali.
Kama mlinyamaza mkiibiwa kura hii ndio opportunity
 
Kwa hali ilivyo kuna haja ya wapinzani kwenda nje ya nchi kufanyia vikao vyao kwa ajili ya maslahi ya wananchi wote. Mbona ccm wanafanya mikutano na haijawahi kutokea wakazuiwa? Polepole kila kukicha yeye na waandishi wa habari. Inakera na inaumiza sana kuona maadili ya jeshi la police yakiporomoshwa na siasa
 
hivi huko CUF tangu mwaka 1995 hakuna mtu anayefaa kuwa mwenyekiti mpaka leo huu ni usultani
 
Nchi inanung'unika kwa sasa, hata kama mnajifanya hamuoni au hamsikii, nchi inalalamika, watu wanalalamikia demkrasia. Mnataka kutupeleka wapi enyi wakubwa wa kuharibu haki na utengamano wa nchi hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kikao BATILI hicho na maamuzi yake yatakuwa ni batili, maana mwenyekiti taifa hana taarifa rasmi!
 
Natoa ushauri kwa Lipumba na Maalim Seif.,kama ifuatavyo...kwa sasa ni vyema wakaangalia namna ya kutatua huu mgogoro ambao unatishia Amani ya nchi yetu...


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…